Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwani unafikiri WANAOKUHUBIRIA DINI wanakupenda sana ndio maana wanajali kwanini wewe hufuati DINI yao?

>> Saturday, March 19, 2011

 .... ni swali  ambalo anayemaindi nani ni MUISLAMU au nani MKRISTO anaweza kujiuliza wakati anahangaikia  kukosoa kwa kuwa kuna wamuaminio BUDDHA  TANZANIA na basi hao kuna kitu wanakosea.


Wakati tunatafakari  pia kuwa  BADO wapo wengi wenye dini zao wasizouzia wengine kama tu   WAKRISTO na WAISLAMU  kama wachawi watunzavyo uchawi usijulikane na kila mtu au WAYAHUDI na dini yao ya KIYAHUDI wasivyoiuza kirahisi kwa wengine  ,...

..ndio wakati tunafikiria hata WAYAHUDI ni miongoni mwa wenye dini zao ambao hawana mcheche wakutaka watu wengine BWELELE wajiunge na dini yao ya KIYAHUDI ili waokoke;....

Swali zaidi:
  • Unafikiria wajalio wengine wanafuata dini gani huwa ni kweli wanafanya hivyo ili kutaka kuwaokoa au kujiokoa wenyewe hasa huku wakijaribbu kujiaminisha kuwa WAAMINIYO ndio sahihi?
  • Kwani hujawahi kustukia wahubirio kuokoa wengine ambao ukikutana na wafanyiayo wengine mtaani  yaonyeshacho ni CHUKI tu juu ya BINADAMU wengine hao hao ambao KIDINI hujifanya wanawapenda na kutaka kuwaokoa?

Ndio ,...
... kuna uwezekano ajaribuye kukuokoa kiimani,..
... hana mpango nawe kihivyo kama tukichunguza anavyo KUJALI kikweli kimengine katika MAISHA mtaani!:-(Ni wazo tu ANDUNJE hili MKUU na wala usikonde!:-(
Hebu Apache Indian alainishe tena kwa -Boom Shak a lakApache Indian aingilie ishu kwa - The IsraelitesAu tu Apache Indian arudishe tu anachojua zaidi tena katika -Arranged MarriageApache indian alainishe zaidi kwa-Dil luteyaAu tu aje na Maxi Priest warudie-Fe real

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Malkiory Matiya 11:10 am  

Kwa hapa Finland Yehova witness wana hii tabia na kwa kule nyumbani, tz walokole ndiyo zao.

SIMON KITURURU 12:44 pm  

@Mkuu M.W.M: Ni kweli kabisa kuna watu wanakuchukia mtaani lakini ukiwasikia wakitetea dini zao utafikiri wanataka kukuokoa kwa kuwa wanakupenda!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP