Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mara ya kwanza kuunganisha BUNDI , Nyau mweusi na UCHAWI wa KITANZANIA!

>> Monday, March 07, 2011


Ilikuwa ni SONGEA , mkoani RUVUMA ,...
...kama mwaka tu  mkoani baada ya kutoka MBEYA ambako ndiko nilikuwa naishi na wazazi wangu na kuanzia shule ya VIDUDU,...
....ilipotokea kuwa nimebaki peke yangu na msaidizi wa kazi za nyumbani -NYUMBANI,..
...kwa kuwa WAZAZI walikuwa wameenda kazini na wengine a.k.a MAKAKA,MADADA au tu ndugu na jamaa wengine  hawakuwepo nyumbani hasa ukikumbuka kuwa mie ni mtoto wa mwisho na WAKATI huo ndio nilikuwa dogo zaidi homu na wakubwa KWANGU katika familia wengine walikuwa TAYARI   shule za kuishi hukohuko mashuleni au wameenda tu kwa  BABU na BIBI upareni.:-(

Basi SIKU HIYO nikashangaa msichana wa watu au tu niseme MAMA wa watu ambaye  NI YULE aliyekuwa anatusaidia kazi za NYUMBANI aliyekuwepo nami nyumbani  ili nisiwe  nabaki nyumbani mwenyewe huku akitusaidia shughuli za nyumbani kwa malipo - katoka mkuku kutoka nje ambako alikuwa kaenda kupiga deki kwenye kivaranda /kibaraza cha nje tu ya sebule.

Mie nikatishika  hasa kwa kuona tu sura yake kwa jinsi alivyotishika,..
... na kwa woga ulioniingia kwa kuona tu alivyobadilika sura ikabidi niulize ``Nini tena jamani? au tu swali likaribianalo na hilo,

- na jibu lake lilikuwa ``Kuna bundi mlangoni´´!

Mie kwanza nilikuwa hata BUNDI sijui ni nini - kitu ambacho labda kilichangiwa na UDOGO ingawa nilikuwa kama darasa la pili hivi shule ya MFARANYAKI hapo Songea.

Maswali yakanijia mengi sana TU  kwa kuwa nilitishika kwa jinsi  yule mdada alifunga mlango ilitujifungie na kwa kutishika mpaka analia. Na mimi ilibidi nichanganyikiwe na labda ndio maana nakumbuka mpaka leo stori hii.

Baada ya muda kidogo wazo likanijia labda tumpigie Baba simu na kwa uzuri tulikuwa na simu zile za kumpigia opereta na kuomba uunganishiwe hasa kwa kuwa Wazazi wangu walikuwa wanafanya kazi hospitalini na walikuwa wanahitajika muda wowote ule swala likitokea hospitalini -nahisi ndio maana tulikuwa na simu kwa kuwa nakumbuka enzi hizo hazikuwa kama enzi hizi za VIMOBITELI ambazo usipokuwa na simu unaweza usijue marafiki, ndugu na malaya zako wako wapi.


Basi bwana!

Nilivyompata BABA na alivyosikia tu sauti yangu ya karibu na KULIA akasema anarudi saa hiyo hiyo. Na kwa bahati nzuri tulikuwa tunakaa karibu kabisa na hospitali kuu ya Songea alipokuwa anafanyia kazi. Kwa waijuayo Songea ya miaka ya themanini -tulikuwa tunakaa kwa chini kidogo ya Hospitali KUU kwenye nyumba ambazo zinaangaliana na uwanja wa MEDIKO na ukivuka tu barabara itokayo upande wa SONGEA GIRLS kutokea kutoka kwetu ulikuwa unaingia uwanja huo wa Medical pale pembeni ya chuo walipokuwa wanafunzwa ma- Medical Asisstants.


Basi bwana!

Kabla BABA hajafika katika udadisi nikasikia  stori nzima kutoka kwa mdada ALIYENITISHA kuwa huyu mdudu BUNDI ni wakichawi na haiwezekani mitaa ya saa tano asubuhi awepo mlangoni mwa nyumba ya mtu kama hakuna mkono wa mtu wa kichawi. Na nikasimuliwa stori nyingi za wachawi mpaka nikaamini hakuna vitu vibaya hapa DUNIANI kama uchawi na wachawi na nikashata mkia kabisa na kukaa nisijue ni nini kina aendelea.:-(


Na kwa  bahati mbaya au nzuri , BABA alipofika chakwanza huko huko nje kumbe hata  kabla hajaingia  ndani alimkabili na kumuondoa bundi huko kibarazani na alipoingia  ndani alichosema tu ni tusiogope na hakuna chochote kibaya na kila kitu kashughulikia na akakataa kujibu maswali niliyouliza kuhusu uchawi ni nini na kusema ni upuuzi tu wa washirikina kitu kilichoniongezea msamiati ``ushirikina´´.

Sitaki kudanganya , siku hiyo hata kwenda kucheza nguti na kabumbu uwanja wa mediko na mabesti sikuenda na nikakaa nyumbani nikiwaza tu uchawi na kwa bidii nikisaidia kazi za nyumbani AMBAZO KWA KAWAIDA nilikuwa SIPENDI -kisa niliogopa kukaa mwenyewe -kitu kilichofanya  nizidi kupewa dozi za stori za WACHAWI  ambazo zikafikia mpaka kupapasa maeneo ya kuwa wachawi hula nyama za watu na wanaweza kupenya ukutani bila kutumia mlango na stori nyingine kedekede kama hizo ambazo zilizidi kunitisha.:-(

Basi Bwana!Jioni ikaingia na wazazi  wakawa wamerudi nyumbani na kutokana na UCHAWI kugeuka ni stori ya siku hapo nyumbani- basi stori zikaanza upya hasa kwa kuwa kulikuwa  na binamu yangu hapo ambaye alikuja naye  homu  akaanzisha stori za uchawi KWA LEVO NYINGINE KABISAAA  -na sasa akawa anaingizia MASWALA YA UCHAWI na MAJINI  adaiyo aliyoyashuhudia yeye mwenyewe - ambayo mpaka leo sijui kama ni kweli au alikuwa anatunga palepale kututisha.

 Na mie kwa kuwa nishasikia wachawi hao watu wabaya hawahitaji MILANGO kuingia katika nyumba za watu kuwanga nikawa naogopa kwenda kulala mwenyewe -kitu kilichofanya nijifanye siogopi kusikiliza stori hizo za majini, mashetani na uchawi .:-(

Basi  SIKU HIYO  zikasimuliwa stori za  kuanzia yaliyomkuta binamu wakati ni taxi dereva na ambavyo alimpakia kimwana bomba ila njiani  akastukia kumbe KIMWANA anamiguu ya mbuzi.

Stori za binamu  yangu huyo wakati yuko huko Arusha alipoopoa demu aliyefikiria ni toto la Kiarabu  ZURI mpaka walipofika geto ambako akastukia wakati wako chumbani na anataka kwenda kuzima taa ya sebuleni yule msichana akamwambia atulie halafu mkono wake tu ukaanza kurefuka na kwenda mpaka sebuleni kuzima taa bila ya kimwana kuondoka chumbanni kitu kilicho mfanya apige mayowe kuita watu kwa kuwa kastukia kumbe kigoli alikuwa JINI,...
.....  mpaka stori za  kushuhudia WAFUKUAO  maiti makaburini  , za ukiwa Tanga usipige teke vifuu  maana vinaweza kukuuliza nimekukosea nini kwa sauti ya mtu na  mpaka mambo ya Sumbawanga ya kuwa mvua inaweza ikamnyeshea mtu mmoja tu ALIYELENGWA NA MCHAWI halafu akapigwa radi akafa wakati watu wengine wote wamzungukao hawanyeshewi , hadi vitu ambavyo baadaye ukubwani ndio nikavielewa kuwa maana yake ilikuwa kuna wataalamu wawategao mademu wao na ukiwakatizia denge na kuonja MALIGHAFI ,...
....utanasia KWENYE KIDUDE TAMUTAMU kama vile kinagundi vile mpaka mwenye KIMWANA MWANANA  atokee kukudaka kimfumanio na mengi mengi mengine mengi.:

Kwa kifupi nikikata TARALILA NDEFU short :

Nachotaka kusema katika taralila hii ni kuwa ,...
.... kwangu MIMI ilitokea kuwa ni BUNDI aliyeanzisha kujua kwangu kuwa DUNIANI kuna kitu kinaitwa UCHAWI.


Na nachosisitizia kwenye tararila hii ni kuwa ,...
.... hapa duniani karibu kwa kila MTU mara karibu zote ni kitu KIMOJA TU  huanzisha mfumuko wa taarifa ya ayajuayo mtu KUHUSU MAMBO FULANI hata kama hicho kitu kiwezacho kusababisha unajua kitu wala hakihusiani moja kwa moja na hicho kitu ambacho kilianzisha ustukie kuna KITU fulani hapa duniani haukuwa unakifahamu.


Najaribu tena kuainisha:
Kwangu NI BUNDI aliyeanzisha nijue kuna UCHAWI DUNIANI na mpaka mambo ya  kujua KATIKA USHIRIKINA  kuna  mpaka NYAU wa rangi fulani ambaye eti inaaminika akikatiza mbele yako kuna waaminio ni BALAA,....
...ingawa bado baada ya muda nikagundua BUNDI maeneo kibao ni ndege tu wa KAWAIDA na tena kuna maeneo hapa DUNIANI  bundi ni ndege asifikaye kwa busara kama kwenye nchi za kaskazini ya Ulaya na ni apendwaye tu kama tu ashangiliwavyo PAKA MWEUSI akivuka barabara mbele yako.Swali:
  •  Si unajua labda ni kitu kimoja tu tofauti MAISHANI -kama kuona mtu anakimbia -ambacho kinakuwa kama KATALISTI ya mtu  kuhangaikia mambo mengine- kwa mfano kubuni viatu  ambavyo nni rahisi kwa kukimbia?

  • SI kunauwezekano leo kuna kitu KINGINE kabisa kama vile KIJAMBO au harufu mbaya ya viatu vya NJEMBA  mwenye FANGASI  kwenye gari lililofungwa VIOO ambacho  labda kilisababisha mtu fulani wakati anafungua VIOO  hali ya hewa ibadilike kwa kuwa alikuwa na wasiwasi airkondisheni inaweza kutawanya TU  zaidi msisitizo wa harufu MBAYA ya kama mayai yaliooza ndani ya gari -labda umeanzisha uchunguzi wake wa VIOO vya magari na kunafanya anazidi kuelewa mambo yahusuyo vioo vya magari wakati huu tunaoongea kitu ambacho tunajua kuwa VIOO VYA magari havina uhusiano na KIJAMBO au harufu za miguu ya NJEMBA ?

  • SI inasemekna kuna walioenda KANISANI kusali na kujikuta wanahamu ya kujua gitaa na kufikia kuwa wapiga gitaa wazuri katika miziki ya ndombolo wakati KWENDA KUSALI kwao kulikoanzisha hamu  ya GITAA na gitaa au tu NDOMBOLO kighafla ghafla labda uhusiano wake wa moja kwa moja hauonekani?

Ndio,..
... kuna kitu labda leo ndio kimesha kuanzishia kujua mengine,...
...na hilo labda ni KWELI kama wewe ni mtu wa KUSTUKIA!:-(


NIMEACHA na hili  NI WAZO TU HILI Mheshimiwa HATA KAMA HALIJATOKA STEREO na wala usikondeshwe sana na hii TARALILA NJOMBA -iliyoshushwa ki - UjingaBUSARA!:-(


JUMATATU NJEMA NGULI!:-(Hebu MYSTIKAL aje na NIVEA waharibu  tena  zaidi muelekeo kwa lugha chafu wakati wakionya-Danger (It is been too long)
Mystikal aje na PHARRELL na lugha chafu zilezile katika -Shake it FAST (Shake YA ass)PHARRELL ajaribu kutuliza manyanga  kwa-She is my ANGEL
Au tu Mystikal ang'ang'anie tu kurudi hapa kijiweni safari hii akija na JOE katika-Stutter

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP