Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ngojea tumfuatilie anachowaza MWANAMKE MMOJA tunayefikiria alitongozwa akakubali !

>> Thursday, March 10, 2011

Ilikuwa ni jumapili jioni na kama kawaida Binti Khalufani alikuwa njiani ,..

.....kwa kuwa ndio ilikuwa  wakati wake wakwenda kuchukua maziwa mtaa wa jirani ambako wana ng'ombe wa maziwa na Mzee Khalufani  ambaye ni  baba yake binti kaweka bili ya maziwa.

Ghafla kwa mbele Binti Khalufani akamstukia yule mkaka ambaye hata sijui ni kwanini tokea amuone kwa mara ya kwanza akipita mbele ya nyumba yao wakati anachagua mchele kibarazani - amekuwa akimuwaza sana.

Na ni mchana  wa jana yake tu wakati yuko chumbani mwenyewe akijiangali kwenye kioo kabla ya kuvaa nguo baada ya kutoka tu kuoga , aliingiwa na wazo lililomtisha kidogo,  kwa kuwa wakati anajiangalia matiti kama bado yana ncha kali kiupana au yameanza kulala kidogo kutokana na umri kuanza kuvuka ukigoli  -  huyu mkaka alimjia akilini kifikira  na kwa ghafla akajikuta kapotea katika mawazo kwa kuwaza siku itakavyotokea kuwa huyu mkaka akafanya kweli na angalau kushikashika nyonyo zake hizo mwanana ambazo bado ni saa sita huku akitamka sentensi  tukufu ile ya aina ya :´´I  love U na nataka uwe wangu wa maisha!´´


``Wee Binti Khalufani njoo usaidie kazi  huku jikoni´´ - ni sauti ya mama yake Binti Khalufani iliyomtoa katika ndoto hizo za mvulana za  mchana   na kukurupuka utafikiri kafumaniwa tayari na kuvuta kitenge kilichokuwa pembeni yake kwa spidi ya radi ilikufunika mwili wake mwanana ambao bado umetawaliwa na matone ya maji  ambayo hakujifuta vizuri bado baada ya kutoka kuoga yafanyayo ameremete miali ya jua ikimmulika na kufanya unono wa mwili wake  uwe ni dhahiri  hata kwa  wafanikiwao kumpiga chabo za adoado  kama yule hausiboi wao ambaye anapenda kufyeka majani kwa nje ya dirisha la Kimwana Binti Khalufani kila apatapo nafasi ya kustukia kuwa Binti kaenda kuoga.

Ndio alijifunika  baada ya kusikia sauti ya mama yake kwa  kitenge utafikiri kama vile mtu aliingia huko chumbani na kustukia au kushuhudia kuwa alikuwa anawaza maswala ya  mkaka wa watu ambaye hata jina lake halijui masikini!

Basi siku hii ya Jumapili  alijikuta kimwendo anajikanyaga na jasho linazidi kumtoka  huku mapigo ya moyo yakiongezeka kwa kila hatua zifanyazo huyu Mkaka asogee zaidi karibu yake. Akilini  mambo kibao yakamuingia ikiwa ni pamoja na wazo la  kugeuza safari ili tu  kumkwepa Mkaka ambaye leo imetokea yuko mbele yake na anakuja upande wake. Na Binti Khalufani alivyostukia Mkaka anamuangalia ndio jinsi alivyostukia hata hatua zake zinavyokuwa nzito mpaka akajisikia kama atazimia -na kilichomzindua ilikuwa ni sauti ya kibezi kama cha sauti ya nne kwenye kwaya ya Mkaka ikimsabahi ``Habari yako Binti Khalufani´´ . 


``Loh kumbe Mkaka ananijua mpaka jina´´ ni wazo ambalo Binti Khalufani hana uhakika alilitamka kwa sauti au kuliwaza tu. Na jingine  lililomjia akilini ghafla  ilikuwa ni kukimbia kitu ambacho sio kabisa tabia yake-hasa ukizingatia kuwa  Binti Khalufani anajulikana mtaani kwa ugumu  na UKALI  na sio kukimbia.

Kitu kifanyacho ni maarufu sana  kwa kufyonza Wakaka wajaribuo kumsabahi au hata kuwasuta wamkome -swala ambalo siri yake ilijulikana tu alipojieleza  siku moja kwa shoga yake ambaye alikuwa anataka kumuunganishia  kidume fulani dili hilo la totoz  alivyodadisi kwanini Binti Khalufani kwa kunema hawezekani lakini ni mkali hivyo kwa wanaume -  na Binti akakiri kuwa hiyo ni staili yake ya  kujihami kabla WAKAKA hawajamwaga shambulizi la mtongozo hasa kwa kuwa tokea avunje ungo ni muda mwingi kweli autumiao kitandani kuwaza wanaume kitu ambacho anawasiwasi kinaweza mpaka kumfanya amkubalie mwanaume yeyote  yule ili yaishe kama hatajihami kwa ukali kwa vidume vitokwavyo udenda kwa hata sketi yake ichezavyo vizuri akitembea kwenye maungo yake ya mwili mwanana ambayo kwa lugha ya kitaalamu huitwa matako.

Na akakiri zaidi kuwa hali hii  imefikia pabaya kwa kuwa anahisi kawaza kimaelfu tayari mpaka jinsi siku ya kwanza atakapojikuta inabidi amvulie mtu nguo - ni kwa staili gani atahakikisha taa inazimwa kabla- na jinsi gani atahakikisha hapigi makelele kwa sauti  hata kama tamu - ingawa atakuwa na dawa za maumivu kwa kuwa kasikia pia  kuwa kwa mara ya kwanza kufanya tendo la ndoa huwa kuna kawaida pia kwa wadada wengine ya kitendo  cha kubingirishana  kufanya kidude  kiume!

Wait a minute!

Swali :
  • Hivi umesoma KICHWA cha HABARI hii ni kuwa  tunafuatilia MTU anachokiwaza?

Ningependa kuendeleza hii STORI MPAKA IFIKIE pale ambapo huyu mvulana ambaye Binti Khalufani tunajua anampenda tayari  na ambaye tunafikiria hata kabla hajaongea Binti khalufani alijisikia kumkubalia  na alijua atamkubali - anakula ngoma ambayo ni dhambi ya uasherati .

Na  ningependa kuendeleza stori hii mpaka pale  jinsi kwa  aibu ghafla hata kabla hajakubali ``AANGUSWAGE TU´´  alijikuta anavuta majani pembeni ya barabara wakati huyu mkaka ambaye baadaye  Binti Khalufani alijua jina lake  ni Hassan Kabasele ya Mpanya mutoto ya Zaire -baada ya  mkaka kujitambulisha jina na kabla tu ya kuhamishia mashambulizi katika kumuomba urafiki na kuhakikisha wanakutana kesho yake akamnunulie Pizza na  pia kumalizia shambulio lenye kikamilishi  kishambulizi kwa Binti Khalufani  kuombwa unyumba a.k.a mchezo wa kibaba na mama,...


... ila stori nzima hii ni ya kutunga  kwangu tu  ni nini kilichokuwa kinaendelea kichwani  mwa Binti Khalufani kwa kuangalia tu ni scenario gani inaweza kudaka uwezekano wa nini kilizaa mahusiano yake Binti Khalufani  na Hassan ,...


..... wakati  kihalihalisi kiendeleacho kichwani mwa mtu -MTU mwingine afanyacho ni kubunia tu kama akijifanya anaelezea kitu  KISICHO MUHUSU kama vile MAHUSIANO ya WATU WENGINE - kitu kigeuzacho stori hii imuhusuyo  Binti Khalufani  labda kama sio Binti Khalufani mwenyewe ndiye msimulizi,..


... basi stori hii ni ya KIZUSHI iunganishwayo tu na vipengele vichache  AMBAVYO KWA KAWAIDA ndivyo vihitajikavyo tu  ili STORI YA KIZUSHI  ifikiriwe ni ya kweli -ambavyo katika stori hii vilivyohitajika ni uwepo wa  Binti Khalufani, Mkaka Hassani  na kuwa wanakauhusiano tukaonako tu kwa kuwa tumeshuhudia wakitembea wameshikana mikono,...
... kitu ambacho katika kujazia stori mtu unaweza kutunga chochote  kile na kikawa kina stori ya aina ya porojo murua kabisa  IAMINIKAYO ambayo ni ya KUBUNI iunganishayo tu vitu hivyo VICHACHE tuvijuavyo..:-(


Swali:
  • SI unajua kuna mabingwa hapa DUNIANI wa kujifanya wanajua kila kitu mtu awazacho kwa kudhania wanajua mazingira ya kitu na aina ya mtu kwa hiyo wanafikiri wanajua anavyofikiria?
  • Na si unajua ni vitu vichache tu VINATOSHELEZA stori ndefu ya kidaku ambayo inatolewa kama ndio kweli tupu?

  • Na si inawezekana si kirahisi hivyo kwa MWANAMUME yeyote kujifanya anajua MWANAMKE anawaza nini kwa kuwa labda hakuna kiumbe ajuaye kiumbe mwingine anawaza nini?


Ndio,...
... kwangu mimi kusimulia yaliokuwa yanaendelea kichwani mwa Binti Khalufani na Kidume Hassan ambaye katika Taralila hii ndio alikuwa anamendea kigoli,....
.... lazima stori itakuwa ni chumvi tu kwa kuwa ni Binti Khalufani ajuaye stori za Binti Khalufani kwa uhakika na ni Hassani ajuaye kwa uhakika nia na madhumuni ya Hassani ya kumfukuzia Binti Khalufani  mtoto wa Kizaramo -wakati tayari nyumbani ana Khadija  mtoto wa Kihaya ,...
....kitu Binti Khalufani ambacho anachojua pia..-(Swali:
  • Si inawezekana anachofikiria Rais GADDAFI ni Rais Gaddafi mwenyewe ndiye kwa uhakika ndiye ajuaye na maswala ya wasimuliao wengine kuhusu Gaddafi mengi yao ni yakuunganisha tu vipengele wavijuavyo na stori ndefu ili tu kujaribu kuhalalisha kuwa ni kweli wawazayo kuhusu GADDAFI ambayo  yamejaa KUBUNIA tu?

  • Kwani unafikiri ni nani ajuaye yote unayowaza sasa hivi kwa uhakika kama sio wewe tu mwenyewe ?
Ndio,...
.... ni vipengele vichache sana waunganishavyo watu kuhalalisha Rais NYERERE hakuwa fisadi katika stori zao kama tu labda ni vipengele vichache sana labda vihalalishavyo stori zitolewazo kama vile ni za uhakika na ni kweli tu  kuwa Rais Mkapa ni fisadi,...
... kitu ambacho kinaweza kuibua uwezekano wa kuwa ni vitu vichache sana kuhusu wewe ambavyo vyahitajika na MBUNIFU WA STORI za kuunganisha  kukuchafulia jina kwa stori za kubuni ambazo WADAKU watachukulia kuwa ni kweli tupu!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

Mr Scruff aingilie shughuli kwa - Donkey Ride


Mr Scruff aendele kwa bezi kubwa lililonuna katika - Bang The Floor


Au tu mdada Speech Debelle apindishe muelekeo kidogo kwa - The Key
Au tu The Streets waweke nukta  tu kipengele kwa - Lets Push Things Forward

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 11:55 am  

Stori nzuri inatia hamasa, ikanifanya nianze kujiuliza mengi katika kuiendeleza kichwani.
Na kweli inawezekanaje kujua kilichoko kichwani mwa mwenzako, kabla hajakwambia, labda awe mganga wa kienyeji ambaye anaweza kukuambia kuwa mchawi wako ni mnene mwembamba kidogo, akimeza meza maneno ili umalizie wmeyewe kwa yule unayemhisi.
Siri ya kichwa ni mkichwa mwenyewe!
Poa mkuu, umtunzi mzuri, hebu imalizie hiyo stori, tuone `mtoto akivuliwa' kwa mara ya kwanza...!

Goodman Manyanya Phiri 2:11 pm  

Mara ngapi, Wakuu, mlikwenda kwa rafiki au kumpigia simu ili kumweleza stori fulani kwa wakati uleule naye alipokuwa anajiandaa kuwapigieni simu juu ya stori hiyohiyo?


Mimi naamini wapo watu wenye uwezo wakueleza kinachoendelea kichwani cha mtu mwingine. Tena kadiri wanavyokuambia unawaza nini ndivyo nawe utakuja kubali ndio ukweli (au utabadilisha mawazo yako yaende sambamba na hiyo PROPAGANDA juu yako!)


Si ndio hivyo Muafrika alipokuja kutawaliwa na Waulaya kwa kuambia historia yake ikweje na anawaza nini mpaka maandishi tele mabovu kuhusu Mswahili lakini hadi kesho kutwa nao "wasomi" waAfrika wanaamini ile PROPAGANDA ya Ulaya juu yao ndio ukweli kabisa?

Binadamu tunapenda sana kufikiri mawazo yetu ni siri, lakini siku ipo karibu tutasikia HAMNA HATA SIRI MOJA DUNIANI!

Kuhusu sasa huyo binti mwenye shauku ya mapenzi mimi amenivunja mbavu kabisa. Si wanasema kipenda roho hula nyama mbichi? Lakini nilikuwa sijawahi kusikia hata "mpanya" utampenda ili mradi roho ikimpenda!!!! (LOL!!!)

Malkiory Matiya 3:23 pm  

Emu:)"mtoto akivuliwa"

Mimi nipo katikati ya Emu-three na Phiri. Si kila mtu amejaliwa kuwa na uwezo wa kujua kila jambo afikiriacho mtu mwingine. Lakini pia kuna wenye kipaji aidha cha kusomea au kupewa na mungu kuweza kujua kile afikiriacho mtu mwingine. Nadhani hapa wana- saikolojia mtaniunga mkono.

SIMON KITURURU 3:39 pm  

Mimi naamini kuna vitu unaweza kubunia na ukapatia katika nini kipo MAWAZONI mwa mtu kama unavyoweza kupatia namba za bahati nasibu tu.Lakini bado inakuwa ni baadhi tu ya VITU na sio mawazo mazima kitu kifanyacho stori nyingi za nini anafikiria mtu mwingine hujaa zaidi UBUNIFU tu .

Kwa mfano unaweza kubunia ukimuona mtu kaenda kwa mama ntilie kuwa aliwaza kwenda kula hapo na ukawa umepatia.

Ingawa labda huyo haendi hapo kula tu kama kigezo kikubwa ila anaenda hapo kwa kuwa mawazoni anamuwaza mtoto wa shule wa kidato cha kwanza na kwa kumvizia mtoto wa shule HUYO ajuaye akitoka shule kwa engo ya eneo auzalo chakula Mama Ntilie ndio amuonavyo vizuri akitoka shule na kujua jinsi ya kumkatizia denge watu wasistukie- ndio hasa awazacho ingawa CHAKULA cha mamantilie ili watu wasistukie kipo kwenye bajeti kama kichembe fulani tu cha wazo.


Ila nachoamini zaidi ni kuwa stori nyingi wasimuliazo watu kuhusu ya wengine ni ya kuunganisha tu vitu vichache ambavyo vinaweza kutoa bonge la stori ambalo ni rahisi kuaminika hasa na wale ambao kisiri walianza kuhisi kihivyohivyo asimuliavyo mbuniaji wa udaku.


Ila ndio hivyo tena hapa tunazungumzia KICHWA na UBONGO wa mtu unavyofanya kazi kitu ambacho ni complicated!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP