Kama tu KITU kizuri tusivyoridhikanacho na kukitafutia KASORO,....
>> Friday, March 25, 2011
....katika KUFANYA yawezekanayo ambayo HATUYAFANYI ,...
......labda wengi wetu tutafutacho ni VIZINGITI na VIPINGAMIZI!:-(
......labda wengi wetu tutafutacho ni VIZINGITI na VIPINGAMIZI!:-(
Na wakati ili tupate NGUVU ya kuchukua HATUA na kuanza KUTEKELEZA,....
.....tufikiriacho KUFANYA,....
......tutakacho KUFANYA,....
......labda kihitajikacho ni MTAZAMO chanya na MATUMAINI katika ya dalili za WEZEKANO na yawezekanayo na kuanza kufanya kwa kuwa LABDA hakuna chochote ambacho kitakosa VIZINGITI na kitakosa VIKATISHAVYO TAMAA kuanza kama ukivisaka hivyo,....
.... hasa kwa kuwa kwa kuwaza tu sana KIMTAZAMO HASI na woga wa nini ni pungufu katika HALIHALISI YA MTU kabla YA KUFANYA ,.......yaweza kuwa ndio kitengenezacho KIZUIZI kikubwa cha kutatua matatizo ya mtu na ambacho ndicho hasa BREKI ya cha kufanya kitu ili kujikomboa- KIPINGAMIZI!:-(
Swali:
- Au?
- Kuna mangapi unafikiri HUFANYI kwa kuwa umejitafutia tu mwenyewe VIZINGITI na vipingamizi na labda hata UDHAIFU ili kuhalalisha HAVIWEZEKANI hata kujaribu KUANZA pambano la kujikomboa?
Ndio,...
... labda kitu KIZURI ,....
... wengi wetu tunakitafuta KASORO na udhaifu ili kujizuia kitu,....
.... na kwa bahati mbaya labda hakuna kitu ambacho ukikichambua ili kusaka KASORO na ,....
..... utakosa udhaifu na KASORO!:-(Swali:
- Si unajua hata MREMBO usiyemuona kasoro kwa kuwa ananukia vizuri bado ukimsachi mpaka utumboni bado utamkuta anatembea na mavi kwenye utumbo?
.... kama unataka KUFANYA kitu ,...
... ukitaka kupata vizingiti na vipingamizi vya kufanya hivyo vitu ,...
.... utavipata tu MHESHIMIWA!:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA lilengalo WOTE wenye MAAIDIA ya kufanya MAVITU babu kubwa ila WANASITA kuchukua hatua ya KUANZA KUFANYA MAVITU hayo MAKUBWA!:-(
Hebu TATUNANE waanzishe vita mpya kwa-Msewe
Tatunane waendeleze...
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment