Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Maisha ya HABARI kwenye Televisheni!

>> Saturday, March 12, 2011

Maisha ya habari za kwenye LUNINGA yangu  kwa ufupi yanizingua!

Hasa hizi HABARI ziletwazo na vyombo vya kimataifa vya habari kama BBC ,.....

.... CNN  nakadhalika!

DARFUR huwa ni habari mpaka HAITI wapigwe na mikasa na kufanya maisha ya habari za DARFUR kwenye habari zisikumbukwe.

Ivory Coast na akina Laurent Koudou Gbagbo ni HABARI mpaka  Misri wamuondoe Muhammad Hosni Sayyid Mubarak na kugeuza maisha ya habari za Ivory Coast yasahaulike na mambo yote uyaonayo yageuke kuwa ni Tahrir Square!

Swali:
  • Kwani tokea JAPAN wakumbwe na mkasa kwenye habari zilizotawaliwa na Libya na Gaddafi unazisikia tena?

  • Kidhaniwacho ni HABARI ni  kitu cha ajabu  sana,...
.... na sijui ni hulka za binadamu kupoteza hamu ya kufuatilia vya zamani ndio kisababishacho kirahisi tu habari ya zamani huachwa  kufuatiliwa na  vyombo vyombo vya habari?

  • Na si inakumbukwa kuwa kasheshe HAITI linaendelea na labda wala hakuna anogewaye kufuatilia tena kwa kuwa mambo yote kihabari  ni UARABUNI  ambako kuna chokochoko la kisiasa na Japani ambako kuna bonge la dizasta?

  • Na sininasikia HABARI ya BABU wa LOLIONDO Tanzania imeua maisha ya stori za habari za DOWANS na hata maandamano ya CHADEMA?
Ndio,..
... maisha ya HABARI MUHIMU  kwenye LUNINGA ni mafupi kweli,...
.... na  stori yako MUHIMU ya  watu fulani wenye ukoma wenye KANSA  au tu ya jinsi YESU atakavyorudi  inaweza isisikike kisa kuna stori mpya ambayo inaweza tu kuwa MVUTO wake ni kuwa MALKIA wa UINGEREZA kaonekana chupi na watu fulani kwa mara ya kwanza ,...
... na hiyo ndio hugeuka GUMZO la MJI  na VYOMBO vya HABARI kwa kuwa ni gumzo la mji huifanya ndio HABARI YA SIKU MUHIMU hata kama unauhakika ni ya KIJINGA.:-(Nawaza tu KWA SAUTI!


Hebu DEAD PREZ wabadili wazo kwa - The Beauty Within
Dead PREZ waingizie chobisi na-Happiness


Habari mchanganyiko...Habari mchanganyiko...

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Swahili na Waswahili 8:35 pm  

Babu mchungaji yuko juu sasa,kila kona babuuuuuuu,haya sijui kinatokea nini sasa ilibabu azimwe,mara myingi habari zinakuwa mbaya/masikitiko zaidi kuliko za furaha, kwangu mimi nikifuatilia habari mwanzo mwisho hudhuni nyingi sana,hasa za Afrika yale mabaya ndiyo yanaongoza BBC/CNN ........,Hivi kwanini au ndiyo zina mvuto kwao?

ok kaka ngoja nikuache ujiandae kwenda huko kwa babu lakini foleni bado kubwa sana tutakukosa hapa @kaka Kitururu! akikubari take away unichukulie hhahaahaaaa!

chib 11:52 am  

Wanahabari wako sawa duniani kote. Nakubaliana na swahili ...., kwana hata Tz, Babu wa Loliondo kashika chati hadi masuala aya Dowans yamesahaulika.
Simon, ukiwa unakunywa kikombe cha dawa ya Babu, uwe unanikumbuka na kwa imani nami nitapata dozi ya kinga auuu :-)

SIMON KITURURU 12:50 pm  

@Rachel +Chib: Ee bwana foleni ni ndefu kweli yani na na kilometa kadhaa yani bado ilinifike kwa Babu!

Ntaangalia uwezekano wa take away kwako Rachel na kwa CHIB nnikipata kikombe ujue na wewe umepona kwa imani!:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP