Ukifanikiwa ambayo MTU ANAKUDHARAU wakati unayaanza LABDA anaweza kutaka kujifanya alikuwa anakusapoti halafu wewe ni RAFIKI yake watu wakiuliza baada ya WEWE kufanikiwa!:-(
>> Sunday, March 06, 2011
Kuna wasubiriao MTU awini wajihusishe na ushindi a.k.a KUWINI kwake!:-(
Swali:
- Si unajua LABDA sasa hivi tunavyoongea kuna MTU anasubiri uwini ILI ajipendekeze?
- Si unajua kuna wakudharauo kisa hawajastukia kuwa biashara yako ya chipsi mayai kama tu ya KUCHEKEA wajanja itakuwa kubwa siku moja DUNIA nzima kama tu ya McDONALD'S au KUBWA kama ya mke wa Rais Mandela mwenye rekodi za KUCHEKEA -samahani- ya kuolewa na MARAIS a.k.a WAKUBWA tu?
MAISHAAAAAA!
Na katika maisha kuna wadandiao TRENI njiani,...
... na kumbuka kuna wamdharauo na kumzonga mtu LABDA kama MIMI na WEWE hasa wakati unahenya bado na hawakioni ukihenyeacho ,....... HASA WAKATI HAWAELEWI mtu ANALENGA NINI katika ahangaikiayo yafanyayo wanaleta dharau hata KWA kisiri,...
.....LAKINI na yote huisha akiwini tu ndude MTU wangu!
Swali:
- Au?
Kwahiyo,...
... labda tusikate tamaa MTU wangu!
- Au?
NI HILO TU na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Hebu Cee Lo Green aingilie kati kwa -Gettin' Grown
Au tu Outkast wazime kibatari taratibu kwa - Git Up, Git Out
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Naam! Hayo ndio kabisa maisha!
@Mkuu Goodman: Kweli kabisa!:-8
Post a Comment