Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika WOGA wa waogopao zaidi huo `` WOGA´´ kuliko kitu kingine- LABDA hata bila kustukia !

>> Thursday, March 17, 2011

Woga kwa KUJITEGEMEA unavigezo vyote vya kutisha,...
...na ,....

....kuna watishikao na WOGA huohuo wenyewe,...
..... na UKICHUNGUZA utastukia wala wakihofiacho katika WOGA huo  sio KITU HATARI zaidi ya  KILE ambacho kimetengeneza  , kinauwezo zaidi wa kutengeneza au kiko nyuma ya woga ambao wanauogopa!:-(



Swali:
  • Unabisha?


Ndio,...
... inasemekana MTU anaweza kuwa ni MUOGA wa kuogopa tu  ,...
.... mpaka WOGA wa kuogopa ukawa ndio uwaogopeshao kuliko kitu kilicho tengeneza WOGA wauogopao.

Swali:
  • SI inasemekana kuna waogopao  mpaka woga wa kupata mimba  kutokana na woga wa matatizo ya mimba waliyoushuhudia kwa aogopaye  ambao labda woga huo ni woga  zaidi ya waogopavyo matatizo yenyewe ya kikweli ya Mimba?
  • Umeshawahi kusikia usemi wa Kindengereko wa``There is nothing to FEAR but FEAR itself´´?

Ndio,....
... labda kuna woga wa WOGA tu pia,...
....na katika KUOGOPA ,...
.....kiogopwacho kinaweza kuwa wala sio kistahilicho WOGA  wa MTU  aisee!:-(



Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(



Mighty Shadow aingilie kati tena kwa - Yuh Lookin Fuh Horn





Denyse Plummer atawanye swala kwa - Nah Leaving




Sugar Aloes ashikeshike swala katika - Reflections




Baron amwage tu naye tena -Mother Earth Crying

9 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:55 am  

Woga, hivi woga ni nini kwanza?

Simon Kitururu 12:03 pm  

@Yasinta: Woga ni hali mtu anayojisikia katika mkandamizo wa mawazo unaosababishwa na mtu akikuliacho kama kitisho.

Kwa ung'eng'e:

Fear is a distressing emotion induced by a perceived threat.

Kwa Kindenereko rahisi kimifano :

Woga wa uchungu wa Klorokwini ni anavyojisikia mtu kabla hajaweka klorokwini mdomoni kwa kuhofia uchungu kama anavyoufikiria na sio kwa anavyouonja.

Woga wa msichana kuhusu uume mkubwa ni kielelezo chake ni jinsi anavyohaha msichana kwa kutarajia itauma kabla hata hajaguswa na uume wa mvulana wake.


Umenielewa?

Yasinta Ngonyani 12:22 pm  

Nimekuelewa Kaka Simon na ahsante kwa ufafanuzi lakini....basi naacha

Simon Kitururu 12:25 pm  

@Yasinta: Mbona nahisi ulichotaka kusema umeachia katikati?

Sema tu mtu wangu , kosoa tu , elimisha tu Yasinta na wala usisite!

emu-three 2:03 pm  

Woga ni hali ya kuwa na wasiwasi kuwa utadhurika, au utapata kitu ambacho hukutegema, ni kuingiwa na muwashawasha wa kuwa na wasiwasi. Na uwoga mbaya ni ule wa kutegemea kitu hasi/au kibaya!
Mkuu umenikumbusha visa vya kale ple mtu alikuwa mwoga mapaka akawa anaogopa kivuli chake mwenyewe, anakimbia huku anakitazama kwa nyuma, na matokeo yake akatumbukia shimoni!

Rachel Siwa 6:41 pm  

Hahahaha @kaka Kitururu umefanunua mpaka Da yasinta naye kapata Woga!!

wakatimwingine mtu anaweza kuona Woga kitu ambacho mwingine hakiogopi akamuona mjinga!

Kumbe kila mtu anacho akioneacho Woga!.

Wapo wanaogopa kuoa/kuolewa kwa sababu wanayoysikia/kuyaona, kama Kukung'utwa na mengine mengi sana!.

@Kaka Kitururu wewe ni muoga wa nini?.

Yasinta Ngonyani 11:25 pm  

Rachel afadhali wewe si mwogw maka umemwuuliza kaka yetu ni mwoga wa nini nami nasubiri kuona atajibu ni mwoga wa nini?

Unknown 8:22 am  

Huyo ana aibu tu labda inayopelekea labda kuhisi ana uoga, ngoja. Sijui yeye anasemaje zaidi kwa hilo @ Kitururu S.

Simon Kitururu 12:18 pm  

@M3 : Unajua nilikisahau kisa hcho cha woga mpaka mtu anakimbia kivuli chake!:-)

@Rachel +Yasinta : Mimi ni muoga wa kuumwa na scorpions nafikiri ni Ng'e kwa kiswahili . Na Centipedes nimesahau jina kidogo kwa sasa hivi kwa kiswahili.

Basi halafu nilipokuwa nasoma Dodoma walikuwepo kibao. Basi kuanzia kuvaa viatu au tu kuingia chini ya blanketi ilikuwa kasheshe kutokana na mimi kuhisi wanaweza wakawa wamejibanza huko.

Basi ilikuwa fulu kukung'uta viatu na mashuka.

Cha ajabu ni kwamba mpaka leo sijawahi kuumwa na Nge wa centipede.

Yani woga ulitokana na stori tu nilizopewa utotoni na umeshika mpaka leo. Na wajuao siri hiyo hunishangaa nikicheza na nyoka au vidubwana vingine waviogopavyo.


Halafu kunakipindi nilikuwa naogopa majini na nafikiri hicho ni miongoni mwa mpaka kilichonifanya niokoke kwenye mikutano ya Moses Kulola. Unajua tena udadisi wa maswala ya mashetani na majini baada ya muda mambo yakanitisha ingawa woga huo haukunikaa zaidi ya miaka miwili wakati wa Scorpion na Centipedes nahisi upo mpaka leo ingawa sijakutana nao hao wadudu kwa muda kupima.

@Mkuu Mcharia: Lakini kweli kuna wachanganyao AIBU na WOGA!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP