Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati hapo zamani za KALE Afrika KUSINI iliwahi kuwa MWENYEJI wa KOMBE la KABUMBU la DUNIA!

>> Wednesday, March 09, 2011

Muda unakimbia jamani,...

... unaweza kusahau ni juzijuzi tu AFRIKA KUSINI  waliandaa kombe la DUNIA na kulikuwa na MAVUVUZELA yaliyokuwa ndio ishu kwa wayapendao na wadaio yanaharibu MASIKIO!:-(


Na unaweza kushangaa eti  HUU ni mwezi wa TATU  jamani,...
... wakati ni juzi juzi tu watu walisherehekea MWAKA MPYA na  kujiahidi mambo kibao kuwa ndio watafanya mwaka HUU hata kama halikuwepo kwenye AHADI ZA MWAKA HUU la ahadi ya Rais KIKWETE mwaka huu  kujitoga SIKIO!:-(

Swali:
  • SI unaweza kujistukia mwaka umeisha na MTU FULANI umjuaye alichofanya kwa uhakika ni kunya tu na kulala kwa kuwa hata kuwa na uhakika na msosi ni jambo ambalo MWAKA HUU kama TU mwaka jana bado kwa uhakika hajalifikia na kufanikisha?
Muda  unakimbia jamani,...
... na  haki ya nani ni kama ukifumba tu macho na ukifungua ni mwezi na mwaka MWINGINE kama una mipango mingi!:-(


TUOMBEANE mafanikio JAMANI!
NAWAZA tu hapa kwa sauti  MHESHIMIWA!:-(


Hebu Dr Sakis aingizie tu - Les InfirmieresTshala Muana akatizie denge na kushambulia kwa - Tshikuna Fou
Au tu hebu The Brecker Brothers wakiwa na Horace Silver wabadili ambiansi.....kwa ngoma -Liberated Brother

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Swahili na Waswahili 12:38 am  

Nikweli itabaki story!!!!!Miaka,miezi,wiki,siku zinakatika kweli,bola usiweke Ahadi kwani ni Deni!!.

SIMON KITURURU 1:20 am  

@Rachel:Ila sijui kwanini naogopa kweli kutoweka ahadi kwa kisingizio itakuwa ni deni mwenzio!:-(

emu-three 7:57 am  

Mkuu umenena vyema, nafasi kama hiyo kupatikana Afrika sijui ni lini. Je tulipoipata hiyo nafasi tuliishawishi vipi dunia kuwa nasisi twaweza? Au ni utaalamu wa kupuliza mavuvuzela tu
Kwa ujumla tunaweza, basi kama twaweza, tuonyeshe kimichezo, timu ziamuke na kulisakata kabumbu...
hapa bongo mavuvuzela ndio mtindo wa kushangilia sasa...hilo tumeliiga kwa sana, labda tusubiri bahati nyingine wakija Brazili , huenda tutafungwa kidogo

Goodman Manyanya Phiri 10:34 am  

Vuvuzela lazima Waafrika kwao ipendeze kwani nasikia mababu zetu enzi za kale walikuwa wanausikiliza mlio kama huo (wa kutengenezwa na pembe) kuhakikisha Mfalme kama ameitisha kikao.

Lakini nakubali nami kwamba masikio yanaumia; na juzijuzi tu sijui kikundi gani katika MAMELODI SUNDOWNS, PIRATES, CHIEFS au MOROKA SWALLOWS walicheza (mpira) hadi kama saa 5 usiku na jamaa jirani huku Atteridgeville Pretoria akapuliza ile vuvuzela lake NILITAKA NIMMEZE KWA HASIRA ZANGU!


Kuhusu mwaka unaokimbia kwa kasi kiasi cha kukufanya hujui umefanikisha nini, nakushauri angalau ujifunze lugha moja au nyingine ya Kiafrika kabla ya mwezi Disemba (http://ndimiafrika.blogspot.com/)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP