Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Yakinishinda katika kitu LABDA haina maana YATAKUSHINDA na wewe katika hicho KITU!:-(

>> Tuesday, March 08, 2011

Kila kitu  LABDA jaribu kukipima kwa vipimo vyako WEWE,...
... na sio vipimo vya mtu mwingine ,...
... hasa kwa kuwa MTU mwingine sio WEWE,......na:


Kwa kawaida KILA mtu ni KIVYAKE,...
....na njia iliyonishinda,...
... labda bado inaweza kuwa KWAKO ndio njia sahihi KABISAAA ya KUSHINDA hata wewe bila kushikwa KIBINDO kama mimi,...
...hasa   kwa kuwa WEWE sio MIMI.:-(
Kabla hatujaendelea  na mtiririko wa TARALILA :

 • Kwani umeshawahi kuwasikiliza WATANZANIA walioenda JKT  wawili AMBAO  watakusimulia STORI MOJA YA ambavyo walirahisisha maisha ya JESHI au tu HATA YALE YA kutoroka JESHINI bila kustukiwa kwa njia zilizofanana?
 • Kwani hujagundua katika mambo yaleyale hata  hapa tukichukulia mfano wa  NDONDI -huwa sio kila mwanandondi anafanikiwa kama Muhammad Ali?

LABDA Jijue,...
... .. na ukijijua utastukia uwezo wako katika kitu ambao labda unasuluhisho kwenye yamshindayo MWINGINE.

 Swali:

 • AU?

Ndio,...
..... ya WATU wawili tofauti ,...
...yanaweza kuwa ni mawili kiutofauti,...
..hata kama SHUGHULI na mazingira ni yaleyale,...
....na kwa UZOEFU wangu nikuambiayo bado niongeayo ni yangu,....
.... na katika hilo bado kumbuka uzoefu wangu na uzoefu wako ni vitu viwili  TOFAUTI,...
.... na labda pia hata  NGEKEWA zako na zangu katika KITU ni tofauti,...
......na labda TAIMINGI  au muda niingiliao SHUGHULI HUSIKA na uingiliao fani ni tofauti,...


.... kitu kifanyacho kuwa LABDA NI UKWELI  kwa mfano kama biashara ya BAGIA itanishinda MIMI  ,...
... labda kwako WEWE haitakushinda hasa kwa kuwa wewe ni WEWE na weye ni mwenye uzoefu wa mpaka wa kutoka kwenye FAMILIA  ambayo inapenda  BAGIA na katika kupenda huko mpaka wanapika  pia hizo BAGIA ,...
....na kwa hilo  inawezekana gia ya BAGIA kama tu ya  MAISHA  labda kwako ndio njia,...
....na mimi  NA YA MIMI itabidi nibakie na ile ya MAANDAZI ambayo mwendo wake wa maringo  naujulia na TAIMINGI zake a.k.a MUDA wakuliingia SOKO unaniruhusu.

Kwa kifupi nachotaka kusema ni  kwamba,...
... si lazima ni KWELI yanayomshinda mwingine umshuhudiaye ni kweli YANASHINDIKANA.:-(


Samahani namuingizia Rais NYERERE kwenye TARALILA ili baadhi ya watu wafikiri nachoongea kina maana:

...Kwa mataimingi  ya kuingia SHUGHULI na mtu HUSIKA ,..
ni kama tu Rais Nyerere alivyojulia TAIMINGI za kufanya jaribio la Ujamaa na KUJITEGEMEA kwa kuwa MUDA uliruhusu hasa ukizingatia mazingira ya siasa DUNIANI ya wakati huo, ukizingati NYERERE alikuwa NYERERE na sio MTU mwingine ambaye labda shughuli ileile ingemshinda,..

...  NGEKEWA ya kuwepo enzi wasomi wachache BONGO ilikuwepo has ukizingatia HIVI VISOMI ndivyo vyenye mchezo wakubishabisha karibu kila kitu  kwa kuwa vinajisikia VINAJUA,....


Samahani namuingizia na Kikwete kidogo kurembesha kahoja:

..... au kama tu   isemekanavyo Rais KIKWETE na wadau zake eti  ndio waujuliao  vizuri UBEPARI TANZANIA wakati huu hasa kwa kuwa MUDA na mazingira sasa hivi unaruhusu ,...
... halafu KIKUBWA hasa,..
.... ni kwa kuwa ni WAO,...
....na wao sio NYERERE mjamaa.:-(


Kwa kifupi nachojaribu kusema ni kuwa,...
....NYERERE kwa kuwa kwake tu NYERERE kulikuwa na mchango wake  katika aliyofanya ambayo labda mtu mwingine wakati huo huo ambaye ni Mwalimu wa sekondari vilevile kama Nyerere alivyokuwa labda angeshindwa kufanya.

Na Rais Kikwete naye  ni hivyo hivyo  kwa kuwa tunajua ni wengi walitaka kuwa marais lakini aliyechaguliwa na CCM kugombea alikuwa ni KIKWETE kutokana na UKIKWETE wake.


Kwa kifupi zaidi :
Labda hata sasa hivi  ni wewe na uwewe wako ndio misingi ya kushinda kitu UKIJARIBU hata kama sio ushindi wa kuwa Rais kama akina KIKWETE na Nyerere!:-(Swali:

 • Si inajulikana wakati huo wa UHURU wa TANZANIA kulikuwepo walimu wengine ingawa ni NYERERE aliyeweza michezo ya ushawishi   kitu ambacho labda MWALIMU mwingine angejaribu hivyo hivyo angeshindwa?
 • SI inawezekana lakini -labda Rais NYERERE angekuwa BEPARI mzuri labda kuliko alivyokuwa MJAMAA kama angeingilia shughuli KIMOBUTU SESESEKO ?


  • Na si umestukia inasemekana kuna Wabongo wasifikao kuwa  baada ya miezi tu  BAADA YA WAO kuingia tu  UGHAIBUNI walifanikiwa sana  mpaka na Maghorofa walijenga  BONGO baada ya nusu mwaka  - wakati kuna WABONGO wako miaka LUKUKI na hata nauli za kurudi likizo BONGO  KWAO ni kazi KWAO KUPATA ingawa wote waliingia na shughuli hizo hizo za kubeba MABOXI ?

  Na kama utaiga ,...
  ....labda IGA  ukijua vinaigika NA kwa kutumia akili ukijua unachofanya na wakuzungukao UWAIGAO wanachofanya  ,...

  .... na kama huna tako zuri na unacho taka kuiga kinahitaji tako zuri na uwaigao wana matako mazuri,...
  ....labda USIIGE  kwa kuwa unaweza USIFANIKIWE  hayo mambo yakutumia  TAKO kudakia biashara wafanyayo wenzako utakao kuwaiga BIASHARA!:-(
  Swali:

  • AU?

  Ila kikubwa  katika nijaribucho kusema ni kuwa WEWE ni WEWE,...
  ... na kwa kuwa wewe,...
  ... tayari kunajambo KWAKO  wewe labda ni rahisi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote kuwa bonge la MTAALAMU!:-(


  Swali:

  • Unabisha?

  Ndio,...
  .. kunauwezekano hii ndude niliyoandika hapa LABDA  ni kweli AISEE!:-(


  BADO ni wazo tu hili  lenye mtiririko dhaifu MHESHIMIWA WEWE unayenisoma na unaye -HESHIMIWA!:-(
  Jumanne NJEMA Mkuu!
  Hebu Cesaria Evora a.k.a The barefoot DIVA katika kurudisha ustaarabu hapa KIJIWENI aturudishe Cape Verde kwa ngoma ya lizombe -Angola  Cesaria Evora aingizie na MADUNGURUDU kwa -Miss Perfumado
  Au tu LUCIANO abadili mchezo na aingizie kigunzi kwenye kuziba tobo kwa ndude-Ulterior Motive

  0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

  Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


  Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

  Partner

  save mt. Kenya campaign
  In partnership with africapoint.com

  Taswira BANANGENGE

    © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

  Back to TOP