Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ile kitu ``FANYA nisemavyo na usifanye NIFANYAVYO!´´- wakati BADO nao ni ushauri!:-(

>> Sunday, March 06, 2011

Wakati USHAURI ni mtamu KWA WENGI  WANAOSHAURI watu wengine  hata kuhusu mengine hata kama ni yale YASIYO shule , BAGIA au HATA nyama ya bata ,....


....katika kuwapa watu wengine USHAURI  hasa kama MTU ashauriyo  sio afanyayo YEYE MWENYEWE ,...
.....inasemekana ashauriye LABDA  ingekuwa bomba kweli angefanya YALE ASHAURIYO wengine yeye MWENYEWE .:-(NA,...

.... kwa kuwa kwa kawaida kama ASHAURIYE WENGINE amefikia kushauri hata mpaka jinsi ya kuhendo utamu wa FIRIGISI iliyochacha ,...
... labda KUNAUWEZEKANO hata kama wakati MWINGINE  anakula firigisi CHACHU  kichachandu  TAMU au anakabili  zile TAMUTAMU firigisi kama ASALI ,...


....tukiachia kuwa TUNAJUA ushauri mwingi  ULIOPO DUNIANI  upo pia na wa kitapeli ,...
...ingawa  huyu TUMUONGELEAYE HAPA wala kitamutamu za KIFIRIGISI SIO tapeli KIUSHAURI ingawa anaendelea kula FIRIGISI zilizochacha,...
....HUYO firigisi anaijua na labda ingekuwa poa kweli kama yeye mwenyewe ANGEACHA kula firigisi zilizochacha azijuazo zinamuumiza tumbo na KULA zile tamu KICHACHANDU au KIASALI kama ashaurivyo wengine!:-(

 Samahani  narahisisha NDUDE!
Kuna watu wanajua SUMU na wakati wanakunywa sumu  KIVITENDO wanaweza wakawa wanakushauri KWA MANENO usiige kunywa sumu kitu ambacho labda ingekuwa BOMBA KAMA WENYEWE wangeacha kunywa SUMU kivitendo kabla hawajaanza kushauri WENGINE kwa maneno tu kuacha kunywa sumu,...
.....ndio maana ya kibwagizo cha hapo juu chenye neno FIRIGISI kila sehemu !:-(
Kabla hatujaanza upya,....


Swali:
  • SI nasikia moja ya sababu UKIMWI hauishi TANZANIA ni kwa kuwa   wengi mpaka kwenye N.G.O za ulaji  zienezazo ushauri wa maneno kuhusu kujikinga na UKIMWI wafanyakazi wake kivitendo INASEMEKANA  ni wazuri kweli katika kueneza ukimwi hasa baada tu ya kumaliza semina na mikutano ya kuelimisha watu  kuhusu kujikinga na VIDUDU  vya UKIMWI hasa kwa kutumia PESA ZA KUHONGEA za mishahara hiyohiyo walipwayo kusitisha  UKIMWI?

  • Halafu si nasikia wengi walalamikiao RUSHWA ni wala RUSHWA au watoa RUSHWA hata kama kisingizio ni kwamba usingetoa kitu kidogo mgonjwa wako asinge hudumiwa au - au TU si inasemekana kuna AMBAYE asinge gawa kidude kidogo kihongo hata  ya ngono  kwa bosi asingepata cheo na watoto wake wangeteseka ndio maana anaendeleza rushwa ya ngono?
Kuna wajuao ,...
... na NASIKIA kama wajuao wakati wanashauri wengine jinsi ya kujikomboa kutokana na UMASKINI Afrika wao wenyewe wangekuwa wanafanya kwa vitendo  na sio kushauri tu kama Profesa LIPUMBA alivyokuwa MSHAURI lakini hata kwenye CUF inasemekana hafanyi kama alivyokuwa anashauri,...
.... haki ya nani tena  labda Tanzania ingekuwa kama KENYA vile- samahani kama CHINA vile kwa kuwa angalau kama bado CHINA  kuna kibano lakini angalau hatua za kwenda mbele  tunaziona hata kama bado wanamatatizo kuwa kuna MIDUME mingi kwenye NCHI yao kuliko WANAWAKE kitu kiwezacho kufanya lazima labda HAPO BAADAYE kuna jamaa za Kchina ambazo ni  NDUME  zitaolewa tu siku moja na MIDUME YENZAYO kama CHINA wakiendelea kwa spidi na SHERIA HII HII waliyonayo ya KUZAA MTOTO MMOJA  halafu karibu kila familia inataka mtoto wa KIUME na sio wa KIKE!:-(
Swali:
  • AU?
Ndio,...
... hata mie huwa nashauri watu kweli mpaka maswala ya watu waache KILAJI,...
... na kusema ukweli KILAJI bado nakigida HUKU NIKIONGELEA KUKIACHA na kila wakati nasogeza  tarehe ya kuacha mbele kidogo,...
... kwa hiyo labda MTU wangu asikonde kama BADO  hajaacha kulamba kamasi!:-(

Tukiachana na hilo:
  • Umechunguza ushaurivyo  wenzako WAVIACHE hata kama hapa hatuongelei NYAMA YA NGURUWE na ni lile swala la kupendelea kusoma udaku na sio vitabu nguli -ni KWELI wewe HUVIGIDI HIVYO UKATAZAVYO WENGINE  hata kama haki ya nani unabonge LA BONGE ya KISINGIZIO?

JUMAPILI NJEMA MHESHIMMIWA na ni wazo tu hili wakati tunakabiliana na ISHU!:-(Katika kubadili  ndude,...

KUMBUKUMBUKUMBUKUMBU
Sugar Hill Gang walainishe kidogo kwa -Rapper's DelightAu tu Grandmaster Flash & The FURIOUS FIVE  warudishie ugumu ngoma pale pale kwa -The message

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Malkiory Matiya 1:00 am  

Mkuu Kitururu naona umeamua kumwaga nondo ya nguvu.Ubin-adamu si mchezo.

Lakini vipi kuhusu ule usemi wa kwenye biblia kwamba usifuate matendo yangu bali yale nikufundishayo!

SIMON KITURURU 2:27 am  

@Mkuu Malkiory:Ubin-adamu ni kweli si mchezo! Na kuhusu huo usemi nahisi ndio kithibitisho tuko wengi washauri tu kwa maneno na sio kivitendo Mkuu!


Si umestukia mpaka ahadi za wanasiasa wetu wakati wanatafuta kura na wakati huo washaurivyo wananchi?:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP