Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati nimerudi tena KIJIWENI kutoka kwa BABU pale LOLIONDO,...

>> Wednesday, March 16, 2011

... ingawa labda wala sikuondoka KIJIWENI,...
.... kama KUTOKUWEPO na  uwepo wa mtu MAHALI ukiangaliwa vizuri !:-(
Swali:
  • Si unajua kuwepo MAHALI  sio lazima uwe MAHALI hasa ukizingatia uwepo wa mtu ndani ya mtu unaweza kuwepo tu vizuri KIMAWAZO TU kama tu uwepo wa mtu CHOONI labda   hauashirii KIUHAKIKA kimawazo mtu huyo yuko CHOONI?

  • Na si unajua kuna mtu UNAYEFIKIRIA NDIYE uongeaye naye ambaye wala hayuko na wewe hapo umuongeleshapo kwa kuwa hata awazacho wakati upo naye  UKIMUONGELESHA sio wewe wala uongeayo-hata kama hapa sizungumzii UWEZEKANO  kuwa PIA kunauwezekano mpaka hata mtu unayengonoka naye labda kimawazo hangonoki nawe kwa kuwa MAWAZONI ANAMUWAZA MTU MWINGINE na  akitaja au kupayuka jina kwa bahati mbaya wakati wewe unashughulika kumpa tamutamu inaweza kustukiwa na mpaka majirani WAPENDAO KUWASIKILIZA mkiwa kwenye yenu ya UNYUMBA  kuwa atamkalo jina kitandani, MKEKANI, kwenye meza chafu jikoni, kwenye sofa  au tu migombani sio jina  lako ?
  • Unauhakika ni WATANZANIA wangapi hawakuwepo LOLIONDO angalau kiduchu hivi karibuni hata kama ni kimawazo tu? 
  • Kwani unauhakika mie MTAKATIFU Simoni MKODO Heriel Kitururu nimerudi kutoka LOLIONDO  kwa BABU kikweli ?Ndio,...
... labda kuna  HATA  kingunge ambaye anafikiri kuwa anaushahidi yuko na mume wake chumbani,...
... ambaye ukweli ni kwamba MMEWE wakati huo bado yuko ofisini na MREMBO sekretari anatomasatomasa!:-(Swali:
  • Si unajua  haya maswala ya UWEPO na KUTOKUWEPO kunibishia RUKSA?
Ndio,...
....nimerudi KIJIWENI hapa ,...
......na hili ni wazo tu MHESHIMIWA !Hebu Mighty Shadow aanzishe upya mkuno  tofauti  KIWAZO  kwa - BassmanMighty Shadow ATEKENYE tena na -Feeling the feeling
Mighty Shadow aendelee na -Tan TanShadow asisitizie-Swing de tingAmalizie tu tena na -Whats wrong with me?

11 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:02 pm  

nanukuu "Ndio,...
....nimerudi KIJIWENI hapa ,..." mwisho wa kunukuu. Ni furaha kuwa tupo pamoja tena Karibu sana Inaonekana kama ilikuwa umepotea mwaka vile:-(

emu-three 3:11 pm  

Kweli mkuu unaweza ukawepo kimwili lakini kimawazo haupo, au unaweza ukawepo kimawazo lakinii kimwili haupo! Au sio unamuwaza nanihii mpaka unafikia hatua isiyotarajiwa lakini nanihii hayupo!

EDNA 3:51 pm  

Karibu tena mheshiwa SIMON tulikukosa sana.

SIMON KITURURU 3:54 pm  

@Yasinta: Asante mtu wangu kwa kunikaribisha tena!

@M3 aka Papaa wa mastori nguli: Si ndio hapooooo!:-(

@Edna mutoto ya Stockholm: Asante mtu wangu!

Mbele 5:08 pm  

Niseme ukweli. Picha zako huwa zinanifurahisha na pia kunichekesha kwa jinsi unavyoshika kilauri (yaani glasi) kwa heshima na taadhima :-)

SIMON KITURURU 5:11 pm  

@Prof. Mbele: Huwa nakumbuka msemo ``Pombe si chai!´´:-)

Nafikiria sana kuacha lakini hii sumu lakini!:-(

Malkiory Matiya 8:25 pm  

Mambo yako safi sasa nadhani baada ya kumwona babu. Hahahaha

SIMON KITURURU 9:04 pm  

@Mkuu M.W.M:Mambo safi kabisa na unajua imaniikiwandogo mambo yako palepale!

Mkuu Malkiory umewahi kufuatilia historia ya madawa Uingereza enzi za Victorian Era? Kwa maana mambo yanao tokea Tanzania ya jaribujari na imani itakuponya nayafananisha sana na yakipindi Pharmacy inazaliwa enzi hizo kwakuwa watu huko ukifuatilia historia walikuwa wana BIHEVU kama BONGO enzi hizi yani!:-(

Fuatilia tu uone mwenyewe!

Swahili na Waswahili 10:47 pm  

Nimefurahi kaka kwa kurudi salama!

maana tulikumithii sana!.Je hawajambo huko?

Nimesikia/kusoma kumbe wewe mtoto mpole na mwenye aibu sana!

pia karibu unaoa!

Ubarikiwe kaka.

Mcharia 8:00 am  

Kila jambo na wakati wake, kama ndio dhamira yako kuacha kilauri utaacha tu tena kiulainiiii kama kinywaji kinavyotelemka kwa kasi ya speed kuelekea kwa tumbo.

Mimi nilikuwa nimekubuhu kwenye uvutaji waaa mar*****ana wakati nilipokuwa nimebobea kwenye urastafarian ilifika wasaa nilianza ijiwa na mawazo ya kuacha, mtu mmoja tena mdada akaniambia kila jambo na wakati wake, utaacha wakati ukifika, akaniaombea bwana!!.

...hakika hatmaye ilikuwa hivyo. Niliona tu sina tena thirsty ya hiyo kitu na hata yale mawazo ya ngoja nika pige pafu za kutafakari yakatoweka mara nikaishia kuacha kabisa.

Cha msingi, kwa kuwa umeshaonesha dhamira ya kuacha KILAURI a.k.a KiRoRo tutamkabidhi Mungu hilo jambo halafu utaona matokeo wakati atakao uamuru yeye ukifika.

JAH BLESS YA MAN.

SIMON KITURURU 12:08 pm  

@Rachel:

Asante kwa kunikaribisha mtu wangu!

Na ni kweli mie mpole wee na na aibu kweli na labda tukikutana walasitaongea kwa aibu!:-)


Kuhusu swala la kuoa na lile la kutengeneza mtoto nafanyiakazi swala bado!

Si nasikia vimwana wazuri wote kwa kawaida huwa wanakuwa washadakwa na wajanja?:-(

@Mkuu Mcharia:

Umenitia moyo sana kwa kauli yako hiyo Mkuu yani wee acha tu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP