Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Leo katika konspirasi: FREEMASONRY!

>> Friday, March 04, 2011


Katika stori zisikiwazo ambazo kwenye redio za mbao hata na zile zisizo za MBAO,...
.... hasa zijadiliwazo kwa hisia bila DATA za kuhakikisha ukweli wa kitu- kitu ambacho kinaweza kuchanganya MTU  kutokana na jinsi uwezavyo kukuta karibu kila mtazamo wa jambo a.k.a PUMBA na MCHELE vimechanganyika huku karibu  kila MTU maarufu unaweza kukutana na TETESI  au  kuna mahali JINA lake linaoanishwa na swala hilo siku hizi ,....
....ni maswala ya FREEMASONRY na ILLUMINATI.Wakati nafanyia utafiti swala tuangalie FREEMASONRY kiduchu katika:MTAZAMO namba ``A´´


Freemason Symbols and Secrets
Tuendelee....


Freemason Symbols and SecretsTuendelee.....

United Grand Lodge of England

Tuendelee....
United Grand Lodge of England
Tuendelee

Famous Freemasons
MTAZAMO namba ``BE´´Freemasons the most evil cult
Na katika kundi uwezalo kukuta  memba zake ni kuanzia Yasser Arafat, Rev.Jesse Jackson, Nat King Cole, Colin Powell, FORD wa magari ya FORD , .....
.....na vimbulukutu wengine ambao hutegemei ,...
.... kuna watishikao na kuna watiwao moyo labda ndude HII sio mbaya KIHIVYO.


MIMI bado sina uhakika PUMBA ni zipi na MCHELE ni upi bado na ndio maana nalichimba swala.

Na madhumuni ya post HII ni kutaka kukujulisha nafanyia tafiti ndude......
...... ili kujaribu kutawanya PUMBA na MCHELE,....
.... wakati natafakari kuwa:


``HIVI  ule usemi wa - (YASEMWAYO YAPO!)- hivi kila uyasikiayo kwani ni kweli YAPO?´´

SIKU NJEMA na ntaingia ndani kipengele hiki zaidi siku nyingine!:-(

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Swahili na Waswahili 12:29 am  

Nami nasubiri umalizie hizo nafaka@ Kaka Kitururu!

SIMON KITURURU 8:07 am  

@Rachel: Ntafanya hivyo Dada yangu!

Goodman Manyanya Phiri 2:11 pm  

Mkuu asante!

Kama ungejuwa, nami juzi nilikuwa nasoma kuhusu mambo hayohayo, lakini baada ya video uliyeonyesha naona ni ndoto za mwendawazimu kwamtu kutegemea anaweza kupata pumba ni Ipi na mchele ni upi.


Kama nilivyosikia katika hizo video zao hayupo hata mmoja aliyetamka wao eti ni wanautulivu??? (PACIFISTS) au watakatifu. Hata nao watakatifu tunajuwa ikibidi damu wamwage wanamwaga tu.


Sasa kweli jamaani kigumu kuelewa ndio nini?


Hawa ni jamaa wenye nia nzuri (THEIR MORALITY IS IN THE RIGHT PLACE).

Wamejiunga na chama chao hicho ili kwendeleza misingi ya mawazo yao kuhusu ulimwengu....(UMOJA NI NGUVU).

Wanasimamia BROTHERLY LOVE (ujamaa) na kama wewe ukiwa mmoja wao wakati Raisi wa nchi yako naye ni mwanachama ambae hua mnakutanaga huko LODGE ("msikitini"/ "kanisani" lenu la FREEMASONS) je unafikiri hatakwonyesha hiyo BROTHERLY LOVE akisikia matakwa yako?


Mpya lakini kwangu ni kwmamba hata Waswahili nao pia na Waarabu (AMERICAS AND THE MIDDLE-EAST) wanaweza kuwa wanachama. Yapili ni kwamba wanapiga kura ya kusema ukubaliwe au ukataliwe. Nilikuwa sijui.

Nitakwenda kupiga hodi siku moja huko nione nitakubaliwa au kukataliwa; lakini nafikiri kuwa mwanachama siyo jambo la kufanyia mzaha. Hawa watu wanaupenda ulimwengu wao hadi kufa, vilevile wanajiamini wao ni hodari katika mambo yote yale unayeweza kukutana nayo duniani.


Kwakufafanua zaidi na hiyo sentensi: walieleza kwaKizungu hivi: [TO MAKE GOOD MEN BETTER]. Sasa neno "GOOD" linayo maana yapili: "hodari". Na ndio maana kwaKiingereza unaweza kusema; "MR PHIRI IS A GOOD THIEF" ikiwa na maana "ALIKOPITA HUYO PHIRI WATU WANALIA NYUMA YAKE KWA WIZI"

Maana yake, kwa maoni yangu: THE BEST AND THE WORST OF WHAT MAKES US HUMAN YOU WILL FIND IT WITH THE FREEMASONS.

SIMON KITURURU 7:13 pm  

@Mkuu Goodman: nakunukuu: ``THE BEST AND THE WORST OF WHAT MAKES US HUMAN YOU WILL FIND IT WITH THE FREEMASONS.´´´- kuna neno hapo linniwazishalo.

Ila kwenye hili swala utakutana na opposing views na kila mtu anadai anauhakika na ajuacho kitu kifanyacho swala zima la FREEMASONRY ni delicate kwangu kiasi fulani!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP