Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda kila kitu ni NYOKO- ila ni aina mbalimbali tu za NYOKO!:-(

>> Monday, March 07, 2011DUNIANI ,....
.... wakati MTU MMOJA  anafikiria labda afanye kitu fulani ili atimize magoli fulani ambayo anafikiria yatamletea maana ya MAISHA na FURAHA maishani,....

... unakuta kuna mwingine kashafikia hapo apalengapo mtu MWINGINE na yeye hapo HARIDHIKI napo na afanyacho ni kulenga kitu kingine ili ajisikie maisha yanaleta maana FULANI au tu  ANAISHI kwa furaha!

Unaweza kukuta Mesenja wa BENKI anataka awe karani wa BENKI , ....
....Karani wa BENKI anataka awe Meneja wa BENKI, .....
........Meneja wa Benki haridhiki na Umeneja na anataka awe Mbunge, ....
............Mbunge haridhiki na ubunge tu kwa kuwa anataka awe Waziri , .....
..................Waziri anafikiria Urais, Rais anafikiria awe Padre au Shekhe,........
.......................Padre ana muonea wivu DJ na kushangaa uhuru wake DJ  katika yale Padre wa Kikatoliki akatazwayo,..........


Swali:
  • SI unajua kuna uwezekano hakuna BINADAMU aliye hai ambaye KARIDHIKA?

  • Na kama kila mtu yuko kivyake kimaisha na labda KUANZIA Mtoto wa shule ya Msingi mpaka Profesa, kuanzia mfagizi wa choo cha stendi ya UBUNGO mpaka kwa Rais Kikwete Ikulu- bado kila mtu anahangaikia kubadili kitu fulani maishani ili maisha yake yawe mazuri zaidi au tu aelewe mambo vizuri zaidi - hufikirii labda yote DUNIANI ayakabiliyo BINADAMU ni NYOKO ingawa nyoko zenyewe zina majina tu TOFAUTI?


Ndio,....
... kuna wadaio hakuna BINADAMU apataye faraja kamilifu DUNIANI hata kama kuna wadhaniwawo kuwa hapa DUNIANI wanaishi kama PEPONI!


Na kama unaishi,...
... LABDA lazima kuna NYOKO fulani unaikabili ambayo inakukumbusha hapa DUNIANi sio MBINGUNI!:-(


Ni wazo tu hili KIKORE!:-(Hebu Joe na Nas walainishe kwa - Get to Know meAu tu The last Poets wabadili mkao na kunyuka swala katika -Niggers Are Scared Of Revolution!The Last Poets waongezee dozi- Surprises


Au tu Gil Scott Heron amalizie tu kwa - Inner city blues

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 1:07 pm  

Sidhani kuwa binadamu anaridhika, hata kama angepewa hela akaambiwa hizi zitakutosha kula maisha yako yote, angedai kulishwa, angedai zaidi ya hizo, hata kunyang'anya, kwani mafisadi wana hela ngapi mpaka watake `kumfisidi mlalahoi!
Tatizo ni kutokuridhika!

SIMON KITURURU 2:24 pm  

@Mkuu M3:Ndio Hapoooo!:-(

Fita Lutonja 2:45 pm  

Kaka hata wanasaikolojia kama vile Rogers na Abrahim Maslow waliwahi kusema hakuna binadamu ambaye anaridhika. Kwa mujibu wa "Maslow's Hiarachical Theory of Human Needs" anasema binadamu anamahitaji mengi sana ambayo yamepangwa kulingana na mahitaji ya muhimu; kwanza kuana Physiologica needs ambapo anahitaji kama vile chakula nk, pia kuna security needs, social needs, self esteem needs na ya tano ni Self actualization needs ambayo sasa binadamu anahitaji kuonekana na kuheshimiwa kwa kutaka mambo makuu zaidi.

SIMON KITURURU 2:57 pm  

@Mkuu Fita: Ni kweli nahisi ! Ila hii kitu inashtua kidogo hasa kama unaipitia kikweli kivitendo halafu unaiona jinsi igeuzavyo mpenda keki na mwenye keki atamani Viazi vitamu alivyowahi kukivikimbia kwa kufikiria keki kwenye KICHENI PATI ni zaidi na ujanja kuliko kulisha wajanja waendao kujishebedua kwenye KICHENI pati VIAZI vitamu MURUA vya kuchemsha na Magimbi tuli kwa pembeni bila kusahau Mihogo a.k.a CHIPSI dume yenye kachumbari swafi na togwa kwa mbali ambayo wasela wakilalamika unaitonyesha kwa kuimwagia gongo kidogo ili wapate ridhimu.:-(

Yasinta Ngonyani 5:21 pm  

Binadamu tuna yetu haturidhiki kabisa na chochote kile.

SIMON KITURURU 5:23 pm  

@Mtoto mzuri Yasinta: Si utani!


Haki ya nani ni kweli mie nahisi usemacho!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP