Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LABDA huwezi KUPONYA HOFU YA NANIHII au tu YA unachokihofia bila KUKIKABILI unachokihofia!

>> Saturday, March 26, 2011

Kwa hiyo LABDA  kama uogopacho ni NYOKA,  mende, KUTUKANA  au tu KUNYA -samahani-  kujisaidia vichakani,....

.... DAWA NI,...
....kumkabili  huyo NYOKA ,...
......huyo MENDE ,......kufanyia mazoezi  KUTUKANA kwa kutusi MTU angalau kiadoadao ,....
.....na kwenda tu  KUJISAIDIA  mara moja moja vichakani mpaka uzoee,....
... kama nia yako ni  kweli kuponya HOFU ya  UNACHOHOFIA.:-(

Swali:
  • Unabisha?
Kwahiyo LABDA tafuta PAKUANZIA kukabili uyaogopayo,...
....mkabili hata kwa  angalau hata kwa KUMSABAHI basi  umpendaye ambaye kumtongoza bado UNAHOFIA,...
....fanya mazoezi hata kwenye blogu yake na sio uso kwa uso KUMTUKANA utakaye kumtukana TOKEA SIKU NYINGI kwa kutumia jina lako halisi NA KAMILI  ikiwa bado kufanya hivyo uso kwa USO unahofia,....
.....au tu  jifunze kumkabili MUNGU hata kwa maombi kama ndiye UNAYEMHOFIA,...
...isije kufanya UMUOGOPE TU ingawa inasemekana ni MUNGU wa upendo na apenda watu kwa hiyo labda sio wa KUHOFIA.:-(Swali:
  • Si hata MAJAMBAZI na MAFISADI labda huanza kuua hofu ya kuiba kwa KUPATA PAKUANZIA KUONDOA HOFU -pale kwenye wizi mdogomdogo kabla hawajafikia kukosa hofu katika WIZI mkubwa uhitajio watu wafe kwa kupigwa risasi au tu kwa kuwa dawa za hospitali  YA SERIKALI ambazo zingewaponya BOSI kazitumia kumjengea kimada nyumba ya pili?

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
SAMAHANI!

Hebu SAMY DIKO aingilie shughuli ghafla kwa- Je Vous AimeAu tu Samy Diko aendeleze tu mpekecho  kwa -EYAE'E EYA

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Malkiory Matiya 1:07 am  

Kitururu: Yasemekana hofu ni matokeo ya kazi ya shetani. Je wewe wakubaliana na imani hiyo au la?

SIMON KITURURU 1:12 am  

@Mkuu M.W.M: Lakini si nasikia MUNGU ndio muweza yote na ndiye aliyeumba yote mpaka huyo SHETANI?:-(

Ila kikubwa ni kwamba ,...
.... kama ni IMANI,...
.... basi tena ya imani ninkama kikombe cha BABU cha LOLIONDO . Aaaminiye huwezi kumshawishi kuwa aaminicho sio halihalisi kwa kuwa IMANI inamchezo wa kutafsiri halihalisi ni nini.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP