Wakati MTU halisi UNAYEKUTANA NAYE na AKUCHEKEAYE kajificha nyuma ya KITU!
>> Wednesday, March 30, 2011
Kuna wajifichao nyuma ya UREMBO,....
.... na kama ni wajinga utachelewa kujua kwa kuwa UREMBO ndio uustukiao.:-(
Kuna wajifichao nyuma ya HARAKATI,...
..... na wanachofanya ni kufanya uoanishe UTU wao na HARAKATI zao wakati wao kama WATU kuwa ni ambalo hawataki liwe ni jambo listukiwalo.
Na kuna wajifichao katika DINI,...
....na wanaweza kuwa wafanyalo ni kutumia DINI na hata MUNGU ili kukurusha kustukia yao BINAFSi ambayo yanatisha kama yakiwa ndiyo moja ya ambalo USTUKIALO
Kuna wajifichao nyuma ya KAZI,...
..... na ukitaka kuwaudhi ruka kutamka ni MAMENEJA wa kitu fulani kwa kuwa ukiondoa UMENEJA WAO na UONGOZI wao wa CHAMA labda hakuna lao BINAFSI kama WATU BINAFSi wajivunialo.:-(
Kuna wajifichao nyuma ya SHULE zao,...
.... na ni tusi kwao kutowaita MADAKTARI hata kama NI UDAKTARI WA KUPEWA kwa kuwa hicho ndio kithibitisho tu kuwa pamoja na yao yakijinga angalau waliwahi kwenda SHULE au wanaheshimiwa KISHULESHULE ingawa labda ni vigumu kwenye hilo kama ni BUSARA za USOMI wao ndilo kustukia ulengalo .:-(
Kuna wajifichao nyuma ya WATOTO , mme au WAUME zao,...
.... kwa kuwa yao ili wajisikie MAISHA yana maaana ni WAUME, watoto, WAZAZI au WAUME zao waaminikao kuna kitu wamefanikiwa ndio watakalo liwe listukiwalo.:-(
Swali:
- Umeshawahi kukutana na mtu ambaye hatumii kitu KUJIFICHA nyuma yake ili angalau kukujengea jinsi UMTAFSIRIVYO?
Ndio,...
.... labda kila mtu kajificha nyuma ya kitu fulani ,....
... na ukijua ukweli juu ya MTU ,...
.....kiutu labda MALAYA ndiye MLOKOLE na MLOKOLE ndiye MALAYA !:-(
NI wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu ghafla Loketo waingilie shughuli kwa -Extra Ball
Las-Ketchup wahamishe mashambulizi kwa -Asereje
Au tu Don Omar arudie - Danza Kuduro
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment