Labda CHUPI haihusiki na ni kuionea CHUPI kwa kuilaumu CHUPI kisa MHESHIMIWA kaonekana uchi kwa kukaa vibaya !:-(
>> Saturday, March 05, 2011
MOJA YA MBINU ya kujisaidia kujisikia VIZURI,...
.....ni ile ya mtu ya kutafuta vitu vingine visivyo yeye vya KUVILAUMU au tu VILIVYO mtu mwingine wa KULAUMIWA!:-(
Na kwa kupata cha KULAUMU kingine hata kama ni cha UONGO ila kiletacho faraja za kujidanganya kwa Simon KITURURU kuwa makosa si yake ila ni ya WENGINE TU wasiofanya vizuri,...
.....kwa muda Simon Kitururu anaweza kujisikia BOMBA yani ingawa moyoni anajua ni yeye wa KULAUMIWA!:-(
Na baada ya muda haitasaidia kuondoa ukweli kuwa KILAUMIWACHO hakihusiki hata kama kinalaumiwa vizuri,....
....kwa kuwa bado LAWAMA mara kibao sio TIBA ya TATIZO hata kama tunafarijika kwa kuwa katika HILI kama LILE tunafikiri tumepata WAKULAUMIWA!:-(
Swali:
- SI unajua kwa makosa ya CCM kunauwezekano kwa CCM kupata wakumlaumu asiye husika katika siasa za TANZANIA kama vile CUF au CHADEMA kwa muda - na katika MUDA HUO inaondoa haja ya CCM kujilaumu?
- Na serikali si WATU na tukizungumzia SERIKALI ya TANZANIA si ni tunazungumzia watu wa TANZANIA na kwa hiyo labda kuilaumu serikali ya CHADEMA au tu ya MCHUNGAJI MTIKILA yote ni yale yaleyale ya KUPATA CHAWAKUMLAUMU ambacho labda kinatuondoa katika kuona picha nzima ambayo ni WANANCHI WA TANZANIA na labda na sisi tukiwemo -kikama tu ya MHESHIMIWA kulaumu chupi na sio kujilaumu yeye MHESHIMIWA aliyeonwa uchi kwa tabia zake TU MWENYEWE za kupenda kukaa vibaya?
- Na si unajua asilimia kubwa ya WAKOSEAO makosa ni yao ila kama tu lile swala la kufeli mtihani au ndoa kuvunjika bado kuna kafaraja kapatikanako kwa kunyoshea kidole MWINGINE au vingine kama ndio sababu na ndivyo vya KULAUMIWA?
Ndio,...
..... kuna uwezekano MHESHIMIWA kuonwa uchi hadharani sio makosa ya CHUPI ,...
... ambayo inalaumiwa kwa kujisweka maeneo ya pembeni zaidi ya sehemu za siri nakuacha ENEO anuai wazi kwa wapiga chabo kidude kukichungulia.:-(
Swali:
- AU?
NA kulaumu kitu kingine KUTAMU bwana,.....
...... na hicho ndicho kifanyacho kuwa TULAUMUCHO labda kiangaliwe tena kwa kuwa labda wala hakihusiki KIHIVYO YANI kama tu vile ilivyo mara nyingi ALAUMIWAVYO KIMADA NA MKE WA MTU - labda wala KIMADA hahusiki na hafai kulaumiwa na LIMKE la MTU ambalo limeenda kumlaumu na kumsuta kwa udoezi wa mtalimbo,...
.... kwa kuwa lenye kosa LABDA ni hilo LIBWANA lake ambalo KALIACHA NYUMBANI ambalo likiona tu upaja udenda kedekede unalitoka na ya MKE na ya KIDUDE cha mke wake , ada za shule, MSOSI NYUMBANI au hata GONO na KASWENDE - tukiachilia mbali umri wa KIMADA ulio mdogo kuliko toto lake la mwisho lililoko kidato cha pili SHULE YA SEKONDARI ,...
.... linasahau!:-(
.... linasahau!:-(
Swali:
- AU?
Ndio,....
....chupi nzuri kama tu yasiyolalamikiwa yale YALIYOKAA vizuri- watu hupenda kujihusisha nayo,...
.... na yale nishai a.k.a CHOO a.k.a MABAYA faraja ipo pia kwa watu katika HAYO kunyoshea vidole watu wengine au VITU vingine kama ndio vinahusika,...
....INGAWA ukizingatia kuwa katika jamii ambayo MHESHIMIWA kukaa uchi ni jambo la kujivunia ,...
.... kwa CHUPI kutoziba vizuri kidude cha MHESHIMIWA mpaka wapiga chabo wakaona MALIGHAFI zake ,...
... unaweza kukuta pia ni MHESHIMIWA mwenye chupi hiyo ISIYOFANYA KAZI VIZURI ndio mpaka hadharani ANAISIFIA!:-(
JUMAMOSI njema MHESHIMIWA na usikonde hili ni wazo tu hata kama LIMEPINDA!:-(
Hebu twende LIBYA kukutana na Rais Mtukufu Muammar Gaddafi atutoe wazo hilo hapo juu nyoko kwa burudani ya kibao chake murua -ZENGA ZENGA
Twende CONGO ili Baloji arudie tena akiwa na KONONO No.1 ndude iliyotuna-KARIBU
Tubaki hapahapa Congo ili Baloji adinye pia -Coup De Gaz
Au Sijui kwanini Baloji na Selah Sue warudie tu live -Coup De Gaz
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Zenga Zenga hiyo babu kubwa! Kesho nakwenda kazini lakini imenipa msukumo hata wa kumaliza wiki kwa mbiu!
Siku hapo watu watapoanza kubeba lawama kwa hiari basi kazi za wanasheria zitakwisha. Na kusema ukweli siyo kitu chema kukubali lawama ki urahisi.
Utamu wa lawama ni kule kumlazimisha mwenye lawama halisi abebe mithili ya kumlazimisha mtoto mchanga kunywa dawa. Siku hapo mtoto atakapofurahia unywaji wa dawa basi dunia itakuwa imekwisha!
@Mkuu Goodman:Umeniua na kauli yako: ``Siku hapo mtoto atakapofurahia unywaji wa dawa basi dunia itakuwa imekwisha!´´.
Na labda ni KWELI aisee!:-(
Post a Comment