Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda CHUPI haihusiki na ni kuionea CHUPI kwa kuilaumu CHUPI kisa MHESHIMIWA kaonekana uchi kwa kukaa vibaya !:-(

>> Saturday, March 05, 2011

MOJA YA MBINU ya kujisaidia kujisikia VIZURI,...

.....ni ile ya mtu ya kutafuta vitu vingine visivyo yeye vya KUVILAUMU au tu VILIVYO mtu mwingine  wa KULAUMIWA!:-(

Na kwa kupata cha KULAUMU kingine hata kama ni cha UONGO  ila kiletacho faraja  za kujidanganya kwa Simon KITURURU kuwa  makosa si yake ila ni ya WENGINE TU wasiofanya vizuri,...
.....kwa muda  Simon Kitururu anaweza kujisikia BOMBA yani ingawa moyoni anajua ni yeye wa KULAUMIWA!:-(Na baada ya muda haitasaidia kuondoa ukweli kuwa KILAUMIWACHO hakihusiki hata kama kinalaumiwa vizuri,....
....kwa kuwa bado LAWAMA mara kibao sio TIBA ya TATIZO hata kama tunafarijika kwa kuwa katika HILI kama LILE tunafikiri tumepata WAKULAUMIWA!:-(
Swali:
  • SI unajua  kwa makosa ya CCM  kunauwezekano kwa CCM kupata wakumlaumu asiye husika katika siasa za TANZANIA kama vile CUF au CHADEMA kwa muda  - na katika MUDA HUO inaondoa haja ya CCM kujilaumu?
  • Na serikali si WATU na tukizungumzia SERIKALI ya TANZANIA si ni  tunazungumzia  watu wa TANZANIA na kwa hiyo labda kuilaumu  serikali ya CHADEMA  au tu ya MCHUNGAJI MTIKILA yote ni yale yaleyale ya KUPATA CHAWAKUMLAUMU ambacho labda kinatuondoa katika kuona picha nzima ambayo ni WANANCHI  WA TANZANIA na labda na sisi tukiwemo -kikama tu ya MHESHIMIWA kulaumu chupi na sio kujilaumu yeye  MHESHIMIWA aliyeonwa uchi kwa tabia zake TU MWENYEWE  za kupenda kukaa vibaya?

  • Na si unajua asilimia kubwa ya WAKOSEAO makosa ni yao ila kama tu lile swala la kufeli mtihani au ndoa kuvunjika bado kuna kafaraja kapatikanako kwa kunyoshea kidole MWINGINE au vingine kama ndio sababu  na ndivyo vya KULAUMIWA?Ndio,...
..... kuna uwezekano MHESHIMIWA kuonwa uchi hadharani sio makosa ya CHUPI ,...
... ambayo inalaumiwa kwa kujisweka maeneo ya pembeni zaidi ya sehemu za siri  nakuacha  ENEO anuai wazi kwa wapiga chabo  kidude kukichungulia.:-(

Swali:
  • AU?

NA kulaumu kitu kingine KUTAMU bwana,.....
...... na hicho ndicho kifanyacho kuwa TULAUMUCHO labda kiangaliwe tena kwa kuwa labda wala hakihusiki  KIHIVYO YANI kama tu vile ilivyo mara nyingi ALAUMIWAVYO KIMADA NA MKE WA MTU - labda wala KIMADA  hahusiki  na hafai kulaumiwa na LIMKE la MTU ambalo limeenda kumlaumu na kumsuta kwa udoezi wa mtalimbo,...
.... kwa kuwa lenye kosa LABDA ni hilo LIBWANA lake ambalo KALIACHA NYUMBANI ambalo likiona tu upaja udenda kedekede unalitoka na  ya MKE  na ya  KIDUDE cha mke wake , ada za shule, MSOSI NYUMBANI  au hata GONO na KASWENDE - tukiachilia mbali umri wa KIMADA ulio mdogo kuliko toto lake la mwisho lililoko kidato cha pili SHULE YA SEKONDARI ,...
....  linasahau!:-(Swali:
  • AU?

Ndio,....
....chupi nzuri  kama tu yasiyolalamikiwa yale YALIYOKAA vizuri-  watu hupenda kujihusisha nayo,...
.... na yale nishai a.k.a CHOO a.k.a MABAYA  faraja ipo pia kwa watu katika HAYO  kunyoshea vidole watu wengine au VITU vingine kama ndio vinahusika,...
....INGAWA ukizingatia kuwa katika jamii ambayo MHESHIMIWA kukaa uchi ni jambo la kujivunia ,...
.... kwa CHUPI kutoziba vizuri kidude cha MHESHIMIWA mpaka wapiga chabo wakaona MALIGHAFI zake ,...
... unaweza kukuta pia ni MHESHIMIWA mwenye chupi hiyo ISIYOFANYA KAZI VIZURI  ndio mpaka hadharani  ANAISIFIA!:-(

JUMAMOSI njema MHESHIMIWA na usikonde hili ni wazo tu hata kama LIMEPINDA!:-(
Hebu twende LIBYA kukutana na Rais Mtukufu Muammar Gaddafi atutoe wazo hilo hapo juu nyoko kwa burudani ya kibao chake murua -ZENGA ZENGA
Twende CONGO ili Baloji arudie tena akiwa na KONONO No.1 ndude iliyotuna-KARIBU

Tubaki hapahapa Congo ili Baloji adinye pia -Coup De Gaz


Au Sijui kwanini Baloji na Selah Sue warudie tu live -Coup De Gaz

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 11:35 pm  

Zenga Zenga hiyo babu kubwa! Kesho nakwenda kazini lakini imenipa msukumo hata wa kumaliza wiki kwa mbiu!

Siku hapo watu watapoanza kubeba lawama kwa hiari basi kazi za wanasheria zitakwisha. Na kusema ukweli siyo kitu chema kukubali lawama ki urahisi.

Utamu wa lawama ni kule kumlazimisha mwenye lawama halisi abebe mithili ya kumlazimisha mtoto mchanga kunywa dawa. Siku hapo mtoto atakapofurahia unywaji wa dawa basi dunia itakuwa imekwisha!

SIMON KITURURU 10:04 am  

@Mkuu Goodman:Umeniua na kauli yako: ``Siku hapo mtoto atakapofurahia unywaji wa dawa basi dunia itakuwa imekwisha!´´.

Na labda ni KWELI aisee!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP