Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ANGALIZO KWA WATANZANIA WOTE, UTAPELI HUU UNAANZA KUOTA MIZIZI.

>> Thursday, October 27, 2011

KUNA TAARIFA ZA WANIGERIA AMBAO WAMEWEKA MASKANI MAENEO YA SINZA, SHUGHULI AMBAZO WANAFANYA WANAIGERIA HAWA BADO HAZIELEWEKI, NI TATA.
MUDA MWINGI HASA VIPINDI VYA JIONI WANAPENDA KUSHINDA KATIKA BAA KADHAA AMBAZO ZINA AMBAA AMBAA NA BARA BARA YA SHEKILANGO, KUANZIA MAENEO YA URAFIKI MPAKA BAMAGA.

HIVI KARIBUNI WATUMIAJI WENGI WA SIMU ZA KIGANJANI NA INTERNET WAMEKUWA WAKITUMIWA MESEJI MBALI MBALI ZA KUSHINDA ZAWADI FLANI, MFANO WATUMIAJI WA SIMU ZA KIGANJANI WAMEKUWA WAKIPATA MSG AMBAYO INAWAONYESHA WAMESHINDA ZAWADI KUTOKA KAMPUNI YA NOKIA, WAKATI UNAKUTA ULIOTUMIWA MSG HIYO MUDA HUO UNATUMIA SIMU YA MCHINA AMBAYO HAINA HATA JINA, NA WALE WATUMIAJI WA INTERNET WANAPATA EMAIL ZA KUTAKA WAINGIZE DETAIL ZAO ZA AKAUNTI ZAO ZA BENKI, HIYO EMAIL INAKUONYESHA KAMA VILE ULICHEZA BAHATI NASIBU FLANI.

WATANZANIA WOTE KAENI CHONJO, KAPINGAZ Blog BADO INAWAFUATILIA HAWA JAMAA ILI KUWEZA KUJUA UNDANI WAO, NA VILE VILE TUNAVIOMBA VYOMBO VYA USALAMA NAVYO VIWEZE KUJUA HAWA JAMAA WANAFANYA NINI, HOFU YETU INAWEZEKANA WAO NDIO WANAJIHUSISHA NA UTAPELI HUU AMBAO NAAMINI WATANZANIA WENGI BADO HAWAJAUJUA VIZURI WIZI HUU WA KUTUMIA MITANDAO.


Nimetumiwa HABARI hii na:
Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 7:38 pm  

Ahsante kwa kutujuza hili.

hansom 7:51 am  

Hao jamaa nadhani ndio wanaojaza msgs kwenye email account yangu, kuna siku wamenitumia eti supervisor wangu wa research yupo ughaibuni ana shida na hela, nilipompigia simu yake kujiridhisha Dk. akasema yeye yupo hapa Bongo hajasafiri, washughulikiwe hao haraka sana.

Simon Kitururu 7:48 pm  

Ila mara kibao WANIGERIA wanasingiziwa kwa kuwa shughuli hizi zimebobewa na karibu kila MATAIFA siku hizi.

Ni sawa tu labda na kudai WATANI WANGU WACHAGA ndio WEZI tu Tanzania.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP