Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

JIHADHARI! Unayebishananaye kwa DHARAU na MATUSI MTANDAONI anaweza kuwa ni MZAZI wako!

>> Monday, October 31, 2011

Stori niliyopewa na MDAU wangu:


Rafiki yangu alinipigia simu jana baada ya MAKUBWA kumkuta.

Basi jana Jumapili alikuwa kaboreka na akaingia mtandaoni kwa simu kuperuzi na kujikuta yuko kwenye mtandao ambao mjadala unaendelea. Kwa spiriti ya kutaka kupoteza muda na pia kucharua mtu akaanza kubishana na ANONYMOUS mmoja mtandaoni  aliyemkera na mpaka matusi akampachika kisa kumchokoza zaidi na pia kwa kuwa alikuwa hapendi misimamo yake.

Baada ya mdahalo kupamba moto na kiu kumpanda akaamua kwenda chumba cha malaji (DINING ROOM)ambako kuna FRIJI ili kupata kimiminika cha aina ya juisi na kumpita BABA YAKE akiwa kakaa SEBULENI naye kazama kwenye simu yake.

Hapo ndio machale yakaanza kumcheza kwa kuwa akawa anastukia kila akituma meseji simu ya Baba yake aliyezama kimawazo kwenye simu na ambaye hakuwa mbali naye inabipu. Na kumbe vilevile BABA MTU kumbe naye machale yakaanza kumcheza kwa kuwa alianza kustukia pateni ya kubipu kwa simu ya BINTI(Mdau wangu) na atumavyo meseji hasa kwa kuwa malumbano  katika tovuti waliyokuwa walibaki watu wawili  wakiendeleza malumbano.

Haikuchukua muda kwa swala kuwa wazi kuwa BINTI ambaye ni MDAU wangu kustukia amtukanaye ni BABA YAKE ambaye anaamini mpaka jana alikuwa anaamini kuwa kalea BINTI na kaleleka kabisaaa kwa tabia nzuri  na kakaa wala sio mbali naye wakati anamtusi .

Na nahisi kilichoendelea unaweza kuhisi hasa baada ya BABA MTU kuwa nauhakika aliyekuwa analumbana naye  ni BINTI YAKE na wala si masaa mengi walitoka pamoja KANISANI .

Na MDAU anadai kuwa anahisi asingekuwa mkubwa angekula mkong'oto jana.

Na sasa hivi hata kumuangalia usoni BABA YAKE anaona haya hasa kwa jinsi alivyokuwa anamtukana na hata pia alivyokuwa anatamba kwa uelewa wake wa mahaba na chakula cha usiku kitu ambacho hata siku moja asingependa hata MAMA YAKE  /Mwanamke mwenzake asikie anayoongea kutoka kwake.

NDIO ! 
HAWAONGEI mpaka sasa hivi naenda MTAMBONI!

------------------_____________________-----------------------------

Kwa hiyo MDAU,..
...jihadari ukiwa MTANDAONI na unayetongozana naye au hata KUMTUKANA anaweza kuwa ni NDUGU yako na hapo ni kama siyo MZAZI WAKO na wakati huo mto chini ya PAA MOJA wakati mnaendeleza mambo zenu hayo hasa kama mchezo ni kujiita ANONYMOUS au tu MAJINA ya UONGO kama ilivyokuwa kawaida ya wengi.

Swali:
  • Si ushastukia  kuna watu  WATOTO unawezafikiria ni WATU wazima MTANDAONI na WATU  WAZIMA ambao tuna mambo ya kitoto MTANDAONI?
  • Na si nasikia  MTOTO na MKUBWA wote wakikosea  bado kiutamaduni wa TANZANIA ni mtoto mwenye makosa kwa kuwa eti ni WATU WAZIMA tu waheshimiwao kihalali na ndio mpaka wawezao toa LAANA ukiwakosea?
  • Na si ushastukia  kuna MIDUME inajiita majina ya kike MTANDAONI na MIDADA ijifanyayo MIDUME?

Ndio,...
... yamtandaoni ya SIRI,...
... yanamchezo wa KUBUMBURUKA  siku nyingine na ANONYMOUS hustukiwa ni NANI kwa hiyo  tahadhari MWANAKWETU  kama unamchezo wa kujiamini  kuwa YAKO ya MTANDAONI  ufanyayo kisiri ,...
... basi hayo MILELE ni SIRI!

Ni hilo tu MHESHIMIWA!Hebu Josky Kiambukuta aanzishe upya kwa - Baby
Turudi Guadeloupe ili FUCKLY arudie-DoudouHalafu Biggie Irie aingilie kati nakuzima kwa- Nah Going Home

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP