Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WASANII MNAVYOKAA KWENYE VIKAO VYENU NA BASATA NA HILI PIA MNALIONGELEA?

>> Thursday, October 20, 2011

Msanii wa maigizo ya vichekesho JOTI akitoa changamoto ambazo anakutana nazo katika sanaa yake hiyo ya maigizo.

Mzee Kipara hii ndio hali aliyofikia hivi sasa.

Mzee Kipara ni msanii wa muda mrefu ambaye alikuwa katika sanaa ya maigizo kwa muda mrefu, kipindi cha hivi karibuni vyombo mbali mbali vya habari vilitoa hali ya afya yake.

Kwa sasa hali yake bado ni mbaya, napenda kuwakumbusha tena wasanii wote msimtupe mzee huyu na mnavyoendelea na vikao vyenu na BASATA pia muweze kumuongelea Mzee huyu, ili kwa pamoja na Serikali mumsaidie. Napenda kuwashukuru wale wote waliojitahidi kumsaidia kwa namna moja au nyingine ili kuweza kumfanya Mzee huyu ajisikie ana watu ambao wanamjali, Mungu atawarudishia.

Nimetumiwa HABARI na:
Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog


UGUA POLE Mzee Wetu!
Na MUNGU akujalie Upone haraka!
-Simon Kitururu

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP