Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MAISHA YA KUJIPENDEKEZA kwa MSHINDI huishi kufuata ukumbukwavyo USHINDI,...

>> Friday, October 14, 2011

 ... na ushindi ukiisha UMAARUFU  kwa wengi wajipendekezao kwa MSHINDI,...

... humsahau MSHINDI kwakuwa tokea mwnzo  hakuwa anapendwa MTU kama MTU,...
... bali kilichopendwa ni USHINDI  na MTU alikuwa  kitu tu kiwakilishacho KUSHINDA.

Swali:
  • Si unakumbuka kuna  wapendao GARI ambao huonekana hadharani kama wampendaye ni MWENYE GARI?
  • Si kuna wapendao UTAJIRI  na ukiwa TAJIRI hata kama unasura na tabia  kama tako wewe ni BONGE la dili?

Ndio,...
.... kuna idhaniwao ni  WAJIPENDEKEZAO kwa MTU,...
... ila ukichunguza utastukia kuwa hawapendi MTU bali tu kile kiwakilishwacho na huyo MTU kitu ambacho  huweza kufanya apendaye URAIS  akajikuta kama  wadaivyo alivyo Mke wa MANDELA kuwa Rais yeyote hule awe SAMORA wa MSUMBIJI  au tu IDI AMIN   kwake  atakuwa  ndiye afaaye kuwa MME hata kama ni yule Mzee kama MANDELA aliyemshinda WINNIE .:-(


Swali:
  • SI mpenda NYANYA  anaweza akajikuta anapenda zaidi bustani ya NYANYA kuliko ile ya KAROTI?

Ndio,...
... MAISHA ya uwepo wa KUJIPENDEKEZA,...
... labda hauhitaji uwepo wa MTU  kwa kuwa kwa ajipendekezaye ,...
.....sababu za kujipendekeza  kwa MTU labda wala hazina misingi ya kweli ihitajiyo huyo MTU.:-(


Ni wazo tu hili MHESHINMIWA!
Ijumaa na WIKIENDI NJEMA MKUU!

Hebu Mzee Yusuph aanzishe upya kwa-Naksh Naksh



Ali Kiba naye aingile kati kwa - Nakshi Mrembo


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:40 pm  

mmmhhh!!

Simon Kitururu 7:07 am  

@Yasinta: Mmmmmm!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP