Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kujua MOJA kuhusu MTU kunawakoseshwao kujua MENGI kuhusu huyo MTU!

>> Thursday, October 27, 2011

 Kuna MENGI kuhusu MTU,....
.... ambayo  hayaonekani tena kisa WATU wanajua MOJA kuhusu huyo MTU.

Swali:
  • Si  kunawasioona ujinga wa MTU  kisa wanajua MOJA kuhusu huyo MTU ambalo ni MZURI?
  • Na si wasioona MAZURI ya MTU  kisa wanajua moja kuhusu huyo MTU  kuwa ni KIBAKA?

Ndio,...
.... na kuna wasioona UJINGA wa MTU  kwa kuona cheti kimoja tu chake kionechasho  kuna kipengele katika ya WASOMI huyo ni PROFESA kama tu wasahauo  kuona mengine KATIKA MTU kisa kimtazamo wao moja walilostukia ni kuwa MTU  huyo ni MLOKOLE na kwa hilo hawastukii tena  kuwa  huyo ni MAMA MBAYA  kwa wanawe kisa tu huyo tayari anaoanishwa na MAZURI.

Swali:
  • SI unajua labda MOJA ujualo kuhusu MTU labda ni hilo tu MOJA na kwa kujua  moja lifanyalo MTU ni maarufu kwa kucheza mpira  labda hakumaanishi huyo MCHEZA MPIRA ki-BEKHAM  yake mengine  yana umahiri kama hayo ya mpira?

Ndio,...
... labda MOJA mtu ajualo la MUUZA SURA kimodo,.......
....linapofua kustukiwa  mengine ya MUUZA sura  kiulimbwende.

Swali:
  • AU?
  • Na si unakumbuka KUTOKUJUA KITU kuhusu MTU hata kama ni huyo MCHUMBA WAKO  yawezekana ndio kifanyacho WAMPENDA -kitu kifanyacho KUTOKUJUA kuwa ni kitu kizuri pia?
  • Kwani ni mangapi ujuayo yafanyayo uridhike na MTU?

Ndio,...
.... kuna  wenye KUKOSA KUJUA MENGI  kuhusu MTU,...
.. kwa sababu katika MAMILIONI yafanyayo huyo ni MTU moja tu WAJUALO KUHUSU MTU tayari linauwezo kwa wengi  kuwafanya wajisikie ni MAPROFESA wa MASWALA yote kuhusu huyo MTU.:-(

Swali:
  • Unabisha?Ndio,..
....na kituliza kujua LILE usilojua kuhusu KITU,...
.... mara nyingi ni lile ujualo tayari na likakutuliza UDADISIwa KITU.:-(

NI wazo tu hili MHESHIMIWA!

Turudi Afrika Kusini ili Caiphus Semenya aanzishe kwa - Dial Your NumberHapa hapa UGANDA Afrigo Band warudie- Tusiimye Nyo


Hawahawa Afrigo Band warudie tena - Sirina ReverseHalafu hapahapa UGANDA hebu Rudeboy Devoh azime kwa- Kampala

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mcharia 4:07 pm  

Kwa hili ni Busara zaidi.

SIMON KITURURU 7:51 pm  

@Rasta Mcharia: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP