Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mahojiano Maalum kati ya Mh Waziri Mkuu na Urban Pulse kurushwa na STAR TV

>> Tuesday, October 18, 2011

Mh Waziri MKuu Akifanya mahojiano na Baraka Baraka


Salam,
Urban Pulse Creative wakishirikiana na Star tv wanakuletea Mahojiano Maalum na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipofanya ziara nchini Uingereza hivi karibuni. Mahojiano haya yalikuwa yamelenga zaidi kupata ufahamu na uchambuzi wa namna serikali yetu ya Tanzania inavyofanya kazi pamoja na changamoto zake.
Mbali na hapo tulijadiliana kuhusu Majukumu ya Waziri mkuu, Chakula, Nishati, Jumuiya ya Afrika Mashariki na mchakato wa katiba Mpya kuelekea kuazimisha miaka 50 ya uhuru.
Mahojiano haya yalifanywa na Baraka Baraka  Kutoka Urban Pulse na yatarushwa Hewani kupitia  kituo cha Star TV Jumapili ijayo Tarehe 30 octoba 2011 kuanzia saa 10.30 katika kipindi cha Medani za siasa.
Tafadhali usikose kuangalia kipindi hiki ili upate kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Tanzania na Serikali yetu.
Asanteni,
Urban Pulse Creative.Nimetumiwa na:
Frank Eyembe wa Urban Pulse Creative

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP