Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Zawadi ya MAUA na WAAFRIKA!

>> Wednesday, October 19, 2011



Baada ya kukuta ZAWADI hiyo hapo  ya UA kwa DADA YASINTA,...
.... nimejikuta najiuliza:
  • Hivi ni kwanini WAAFRIKA wengi UA kwao sio ZAWADI na kwa Wamagharibi ni lini MAUA yalipamba moto kuwa ni ZAWADI MWANANA?
  • Kwako UA ni Zawadi?
  • Kama sio KWANINI na kama ndio -Kwanini?




Nawaza tu kwa SAUTI!

Hebu tubadili wazo kwa kumuachia Wiz Khalifa  katika- Fly Solo



Au Wiz Khalifa azime tu kwa - Black And Yellow


5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:33 pm  

Kwa mimi zawadi ni zawadi sio lazima kiwe kitu cha kula au kuvaa kama wafikiriavyo wengi. Umenikumbusha kulikuwa na mtu mmoja "Mzungu" wakati naishi huko Madaba alikaribishwa chakula cha jioni na nyumbani kwako alikuwa na bustani ya maua akaona akata/chume maua na awapelekee wenyeji wake. Baaada ya siku yule mwenyeji wake akasema "wazungu" bwana eti kaja na maua unadhani mimi nitakula kushiba? nifanye nini mimi na maua?

Simon Kitururu 3:45 pm  

@Yasinta:DUH!

Kunajamaa kanitonya kuwa UMASIKINi na zawadi za maua ni vitu tofauti. Na mwingine kaniambia kama si mchagua zawadi basi wewe si hohehahe kimaisha.

Ila mimi nafikiri ni utamaduni tu wamaua hatuna wengi wetu kitu kifanyacho uthamani wake hauonekani.

Na labda kuthamini ZAWADI kama kitendo cha kujaliwa na MTU kuwa kina thamani zaidi kuliko bei ya zawadi ni jambo lakujifunza. Na unaweza kukuta lahitaji kuanza kufunzwa tokea utotoni jinsi ya kuridhika na chochote tupewacho.

Yasinta Ngonyani 4:06 pm  

nukuu "Na unaweza kukuta lahitaji kuanza kufunzwa tokea utotoni jinsi ya kuridhika na chochote tupewacho." mwisho wa nukuu :-hili ni kubwa zaidi kwa kweli kama umezoea kupewa hata makande siku ya kuzaliwa kwako kama ndio chakula sidhani kama utaona si chakula kizuri. Nimependa kamada haka...

sam mbogo 4:49 pm  

zawadi ni imani/kuridhika.kinacho changanya au kutatiza nimzingira ya utoaji zawadi hiyo.mfano- unaporudi tz likizo ukifikiri zawadi unazotaka kuwapelekea ndugu jamaa na marafiki huwa kazi kwelikweli. unabidi uwe katika nafsi mbili katika mtazamo wa zawadi,kiulaya maranyingi watu huulizana kuhusu zawadi unayo taka. ki tz hupenda zawadi ya kumsapriizi,abayo huna uhakika ka ataipenda au laa watakushangaa utakapo shuka tz na kupa shangzi zawadi ya maua?.kaka s

Yasinta Ngonyani 5:17 pm  

Kaka S.kama alivyosema kaka Simon zawadi inategemea na utamaduni/makuzi yetu. Kumpa shangazi maua utakapo Ulaya utakuwa umemdharau mno...ni kazi sana kuwapa watu zawadi kwani hazilingani na nyumbani...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP