Salam,
Dr Julie Makani kutoka Tanzania amepokea Tuzo jumanne tarehe 18 octoba 2011 ya Royal Society Pfizer nchini Uingereza. Dr Makani amepokea tuzo hii ya utafiti alioufanya katika gonjwa hatari la Sickle Cell (SCD) ambaye makazi yake ya kazi ni kwenye Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi cha Muhimbili katika idara ya Haematology. Kutokana na utafiti wake kumeonekana ushahidi kuwa, chanzo kikuu cha magonjwa na vifo vitokanavyo na sickle Cell nchini Tanzania husababishwa na Arnemia (upungufu wa damu)
Dr Makani pia amefanya mchakato wa matibabu katika majaribio ya Hydroxyure chemotherapy agent inayo gusa Bone marrow katika matibabu ya Anaemia kwenye ugonjwa wa Sickle Cell
Ni matumaini yake kuwa utafiti huu utapelekea kuboresha uchunguzi na matibabu ya ugonjwa huu ili kuweza kuimarisha afya za watu, mfumo mzima wa afya na jamii kwa ujumla.
Kwa niaba ya Watanzania wote Urban Pulse tunapenda kumpongeza DR Makani kwa mafanikio hayo.
Asanteni
Urban Pulse Creative
|
Dr Julie Makani akitoa machache |
|
Wageni waalikwa kwenye Royal Society Pfizer Awards London |
|
Kutoka Kulia Balozi Kallaghe, Mama Makani, Dr Makani, MP O'Brien, Naibu Balozi Chabaka na Mr Simba |
|
Dr Julie Makani akiwa na familia yake |
|
Dr Julie Makani Akipokea Tuzo yake |
|
Dr Julie Makani akiwa na Baba yake Mr Bob Makani pamoja na Mama Vicky Makani |
|
Parliamentary Under Secretary of State, International Development Stephen O'Brien. akimpongeza Dr Julie Makani |
|
Dr Julie Makani. akiwa na Cleo, Paul na Frank baada ya kupokea Tuzo. |
Nimetumiwa na :
Frank Eyembe wa Urban Pulse Creative
Hongera Dr Julie Makani!
-Simon Kitururu
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
HONGERA SANA NA KILA LA KHERI!!
Post a Comment