Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wengine WAKUZUNGUKAO inawezekana sio tena WATU bali ni LUNINGA ,kompyuta na MAGAZETi ya UDAKU.

>> Wednesday, October 19, 2011

 Wengine WAKUZUNGUKAO ,....
... yawezekana ndio waathirio YAKO  UFIKIRIAYO na yakuzungukayo sasa hivi,...
... hata ki uyatafsirivyo.

Swali:
  • Kwani unafikiri WENGINE kwako bado NI WATU au tu  ni  VITU tena vya wengine hasa katika DUNIA HII ya leo ambayo VITU na MALI vyajaliwa kuliko UTU ? 
  • Si umeshawahi kusikia kuwa kuna watu kibao hata nchi zilizoendelea  WANYAMA kama Mbwa au paka na WATU  hakuna tena tofauti  kiwawafikiriavyo?
  • Na si  pia ukitaka kupima thamani ya MTU na KITU labda chunguza ni kwanini KIBAKA anaweza kutolewa roho  kwa kosa la kuiba  ndizi kitu kifanyacho labda MTU na NDIZI  au hata tukiita kidhaniwacho KIBAKA kakwapua ni POCHI - kwa watu wengine kiuthamani  UHAI  na KITU hakuna tofauti au kwa kuwa KIBAKA huuawa basi UHAI haunathamani kama KITU?

Ndio,...
... labda ukifikiria,...
.... WENGINE wakuzungukao na kuathiri ufikiriavyo,....
..... sio WATU tena moja kwa moja kwa kuwa UTHAMINICHO labda wala sio MTU.

Katika kumbukumbu:
  • Unakumbuka  msemo HAPENDWI MTU pochi lako tu!?:-(
Ndio,...
.... kwa wengine MTU  na KITU ,...
.... labda kiuthamani  hakuna tena tofauti kitu kifanyacho KITU kuthaminiwa ZAIDI.:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

Hebu  tupitie tena TOGO ili Afia Mala amwage - Baila Mi Musica


Afia Mala aongezee dozi kwa - Ten HomteHalafu hapahapa TOGO hebu tena Afia Mala azime kwa- Segne


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 10:01 am  

Ulichosema ni kweli kabisa nimependa sana wazo lako la leo ni BONGE la wazo...Na kuna kitu nimejifunza AHSANTE SANA KAKA SIMON:-)

SIMON KITURURU 3:50 pm  

@Yasinta: Tuko Pamoja!

Yasinta Ngonyani 4:10 pm  

Daima Simon!!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP