Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UNAKUMBUKA Mapinduzi ya TUNISIA yalianzishwa na MMACHINGA aliyejichokea na sio WANASIASA au WASOMI wale FULU kujifanya WANAJUA KILA KITU?

>> Sunday, October 23, 2011


WATUNISIA wakibeba picha ya mchoro ya Mohamed Bouazizi(29 Machi 1984 – 4 Januari 2011)




Desemba 17 Mmachinga Mohamed Bouazizi aliyekuwa na miaka 26, alijichoma moto kupinga ukandamizaji katika mji wa Sidi Bouzid na kufia kwenye hospital huko Ben Arous, Tunisia baadaye.

Machinga huyo aliamua kujichoma moto mbele ya ofisi za serikali baada ya kunyang'anywa MATUNDA na MBOGAMBOGA alizokuwa anauza na kunyanyaswa na maafisa wa mji na mgambo wao kwa madai kuwa hana kibali cha kufanya umachinga kitu kilichomfanya aone hakuna haja ya kuishi katika mazingira ambayo kujitafutia riziki kihalali kwa kufanya biashara ndogondogo bado mtu ananyanyasika na kuporwa hata kamtaji.

Kujichoma kwake ndiko kulifanya Wananchi karibu Tunisia nzima kuamua wamechoka na matokeo yake ni mpaka serikali ya Rais Zine El Abidine Ben Ali ikaanguka -kitu ambacho kikaeneza wananchi kudai mapinduzi karibu Uarabuni kote.

MADHUMUNI ya TARALILA hii ni KUKUMBUSHIA TU kuwa:
  • Saa nyingine cheche za mageuzi huanzia usikokutegemea na usishangae kuwa labda si WANASIASA watakao geuza nchi hata ya TANZANIA.
  • Na labda uwadharauo wanaweza kuwa ndio kiini katika ukombozi wako.

Ni angalizo tu hili MHESHIMIWA!
JUMAPILI NJEMA KAMANDA!



Vyanzo vya stori ya Mohamed Bouazizi unaweza kugugo tu au nenda kwa Aljazeera;
...donoa
HAPA,...

....au hata bofya
  HUKU


Hebu MICHAEL JACKSON atutie majaribuni kwa kumsifia KIDOSHO wa KILIBERIA katika-Liberian GIRL



Au tu Michael Jackson azidi kubembeleza kidosho kwa - Give In To Me

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 8:32 pm  

mtakatifu nakuunga mkono kwa falsafa hii ndani ya neno...ni kweli kabisa mageuzi yataleta na kitu tusichokitegemea ingawa ni muhimu kwetu kuendeleza harakati

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP