Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa bahati mbaya TUKO WENGI tupendao kumsikiliza au hata KUMSOMA aongeleaye TUTAKAYO tu KUSIKIA!:-(

>> Thursday, October 20, 2011


Na yasemekana UKWELI ni kwamba,...
... kama tayari unajua UPENDAYO kusikia,....
.... labda hayo tayari unayajua kiasi cha kutosha kama ukiyafikiria MWENYEWE kiundani,...
.. na labda wakati huo ingekuwa busara KUSIKILIZA au hata kusoma usiyotaka KUSIKIA,...
... kama nia ni kutaka kuendelea kujifunza kitu KIPYA!:-(

Swali:
  • AU?
Ndio,...
... labda kuendelea kunogewa kusikia utakacho kusikia hata kama hicho ni kuwa WEWE ni MZURI KWELI,...
..... wakati huo yawezekana unajijua TAYARI wewe ni MZURI mwenye sura tamu kama PIPI na huo MUDA uendeleao kuutumia kurudia kusikia sifa zilezile za uzuri wako,...
.... KIBUSARA labda ungekuwa ni wakati wa kujifunza kwa uzuri wako HUO uchuneje buzi KIMALAYA au tu uuficheje ki SISTA wa KIKATOLIKI ili usidoewe na Wakware.:-(

Swali zaidi:
  • AU?

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(


Hebu turudi UGANDA ili PHILLY LUTAAYA aanzishe upya kwa-Ndabye Ennake



Philly Lutaya atukumbushe tena -Tugende e kampala



Kabla tu huyuhuyu Philly Lutaaya hajazima kwa -Entebbe Wala

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Unknown 12:09 pm  

Kuna uzuri wa umbo, uzuri wa sura nao umo, kuna uzuri wa tabia, uzuri wa nyumba/gari/chakula/harufu/sebule. Kuna uzuri mwingi mwingi maeneo tofauti, endelea kuorodhesha na wewe.

Nionavyo mimi kama sio kufikiri: tutakayokusikia mwamuzi huwa ni SIKIO.

Bisha.

Simon Kitururu 12:49 pm  

@Rasta Mcharia: Nabisha kiaina!

Tutakayo kusikia labda muamuzi sio JICHO wala SIKIO,...
... ila ni UBONGO mukichwa!:-(

AU?

sam mbogo 1:20 pm  

Kiuhakika, hakuna mtu asiye taka kusikia yale ambayo anataka kusikia,ikiwa tofauti nahivyo basi wewe mtu/kiumbe siwakawaida. iwapo yakatokea kusemwa ambayo hukutegemea basi siyako na iwe changamoto kwako. wakati unasikia ni akili yako inachuja ukisikiacho/ubongo. mchango wa sikio nimdogo kwa maana utasikia lakini ubongo ndo utakao fanya kazi ya hicho ukisikiacho kama kimekukuna au laa!.,kaka s

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP