FARAJA ni kitu chochote KILE mazingira na halihalisi IKIRUHUSU !
>> Tuesday, October 25, 2011
Chochote kile huweza KUFURAHISHA mtu,....
.... na LABDA inategemea tu MTU ana hali gani yuko kwenye mazingira gani na anajisikiaje ,...
... na ikibidi unawezashangaa ni kwa jinsi gani KITU cha KAWAIDA TU kiwezavyo kufariji MTU.
Swali:
- SI umestukia kuwa hata kitu kidogo kama KUMBIKUMBI kiwezavyo kufanya mpenda KUMBIKUMBI ajisikie vizuri sana kisa kaonja kumbikumbi ughaibuni na ghafla anajisikia kifaraja yuko KWAO Bukoba?
- Na si ushawahi kuona waridhikao sana hata kwa kusikia tu FULANI kafa?
- Na simpenda TOGWA huweza kurizika na Cocacola ikibidi?
Na yasemekana kama umewahi kuangalia WATOTO wakicheza,...
... utagundua chochote kile kinafaraja ya kimchezo hata kama kichezewacho ni KIJITI TU,...
... na kwa kuwa yadaiwa kwa MTOTO kukua haimaanishi kutoweka kwa asilimia mia kwa vimfarijivyo MTOTO,...... kwa hiyo hata MTU MZIMA bado kama mtoto tu arizikavyo na mdoli wa kitambaa au gari la migomba,...
... mazingira yakiruhusu kitu kutafsirika kama FARAJA katika UBONGO wa MTU,...
.... chochote kile hata usichokizania kama choo cha shimo kwa aishiye kwenye vyoo vya maji /kuvuta wakati maji yenyewe ya mgao ,.......huweza geuka FARAJA ya MTU aiseee.
Ni wazo tu hili MKUU!
Hebu turudi Kameruni ili Sam Fan Thomas arudie tena-African Typic Collection
Sam Fan Thomas aongezee tena dozi kwa -Zimo(To Nelson Mandela )
Au tu Sam Fan Thomas zime tu tena kwa - Noa
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Hahaha ha haaaa! mweh, hilo la kumbukumb u umenistukia kweli maana ni kweli siku hiyo nilijikuta nipo mitaa ya Peramiho sokoni...halafu nikajikuta kama hamu ya kucheza lizombe vile:- Ahsante kwa wazo hilo linafikirisha kweli:-)
Post a Comment