Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Daktari Mtanzania Julie Makani apokea tuzo kutoka Royal society Pfizer London

>> Wednesday, October 19, 2011

Salam,          

Dr Julie Makani kutoka Tanzania amepokea Tuzo  jumanne tarehe 18 octoba 2011 ya Royal Society Pfizer nchini Uingereza. Dr  Makani amepokea tuzo hii ya utafiti alioufanya katika gonjwa hatari la Sickle Cell (SCD) ambaye makazi yake ya kazi ni kwenye Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi cha Muhimbili katika idara ya Haematology. Kutokana na utafiti wake kumeonekana ushahidi kuwa, chanzo kikuu cha magonjwa na vifo vitokanavyo na sickle Cell nchini Tanzania husababishwa na Arnemia (upungufu wa damu)

Dr Makani pia amefanya mchakato wa matibabu katika majaribio ya Hydroxyure chemotherapy agent inayo gusa Bone marrow katika matibabu ya  Anaemia kwenye  ugonjwa wa Sickle Cell

Ni matumaini yake  kuwa utafiti huu utapelekea kuboresha uchunguzi na matibabu ya ugonjwa huu ili kuweza kuimarisha afya za watu, mfumo mzima wa afya  na jamii kwa ujumla.

Kwa niaba ya Watanzania  wote  Urban Pulse tunapenda kumpongeza  DR Makani kwa mafanikio hayo.

Asanteni

Urban Pulse Creative



Dr Julie Makani akitoa machache

Wageni waalikwa kwenye Royal Society Pfizer Awards London


Kutoka Kulia Balozi Kallaghe, Mama Makani, Dr Makani, MP O'Brien, Naibu Balozi Chabaka na Mr Simba

Dr Julie Makani akiwa na familia yake

Dr Julie Makani Akipokea Tuzo yake


Dr Julie Makani akiwa na Baba yake Mr Bob Makani pamoja na Mama Vicky Makani

Parliamentary Under Secretary of State, International Development Stephen O'Brien. akimpongeza Dr Julie Makani

Dr Julie Makani. akiwa na Cleo, Paul na Frank baada ya kupokea Tuzo.
Nimetumiwa na :
Frank Eyembe wa Urban Pulse Creative


Hongera Dr Julie Makani!
-Simon Kitururu

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 9:32 am  

HONGERA SANA NA KILA LA KHERI!!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP