Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hapo zamani za kale AFRIKA hakukuwa na siku ya JUMAPILI!

>> Sunday, June 26, 2011


Asante WAMISHENARI kwa kutuletea mpaka JUMAPILI,...
....kitu ambacho huathiri mpaka  KISAIKOLOJIA na kufanya kuna watu waamini kuna tofauti kati ya IJUMAA na JUMAPILI,...
....Jumatatu na JUMANNE,...
....au tu na kusababisha tuamini kuna kitu kinaitwa WIKI na kuna siku saba katika WIKI,...
... kitu kiathiricho mpaka VIGEZO vifanyavyo tuamini kuwa hata mwenye sehemu za siri zilizosinyaa bado ni KIJANA kama kikalenda zenye mpaka siku TAKATIFU ya JUMAPILI ,...
... huyo anamiaka MICHACHE.:-(

Swali:
  • SI hata uonekane UMEZEEKA vipi kimuonekano bado ni KIJANA kama kwa kufuata kalenda ifanyayo tuamini tuifikiriayo ni SIKU ya SABATO JUMAMOSI kweli ni JUMAMOSI kisa kalenda isemayo lini ni JUMAPILI ndio tuinukuuyo kutabiri MUNGU wakati anaiumba dunia alipumzika LINI?
  • Lakini si labda ni kweli pia KILA siku ni tofauti na SIKU nyingine?


Ndio,...
.... labda bado ni kweli HAPO zamani za kale bado kulikuwa na KALENDA iliyoruhusu WA KALE wajue nani kijijini ni MZEE kuliko wote,...
... ingawa labda hiyo kalenda haikuwa na JUMAPILI wala ALHAMISI!:-(

Swali:
  • Unabisha?
Asante WAMISHENARI kwa  kufanya IJUMAA isitukuzwe na baadhi ya WAKRISTO kama JUMAPILI,...
... na kwa nyie wengine JUMAPILI NJEMA!:-(
NI wazo tu hili MHESHIMIWA na WALA usikonde !



Au tu Bascom X aingilie tena wazo kwa - Eyes On The Prize



I Wayne aanzishe upya kwa-Life Seeds


I wayne atulize kwa-Cool as the Breeze




I wayne arudie - Need Her In My Arms


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 3:43 am  

Kila siku, ni siku ya kumwabudu na kumtukuza Mungu. Haya mambo ya Jumapili kwa Wakrestu, labda na Ijumaa kwa Waislamu ni ukoloni mtupu wa Bara letu na Wazungu pia na Waarabu kabla ya Wazungu.


Sisi Waafrika wenye kuanzisha ubinadamu, ustaarabu na elimu yote (iliyoigwa na kudaiwa hapo baadaye na Waarabu pia na Wazungu baada yao) hatunabudi la kuanzisha utamaduni na mfumo mpya duniani wa kumwabudu Mungu kila siku.


Tumwabudu Yeye tukiwa kazini; tukiwa katika sherehe; tukiwa tunafanya mapenzi; na katika shughuli zote zile zinaemhusu binadamu; na Jumapili iwe ni siku tu ya kawaida katika mapenzi ya Mungu!

Simon Kitururu 4:30 pm  

@Mkuu Goodman: Hapo umenena!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP