Kuna tofauti,...
>> Friday, June 17, 2011
....kati ya KUONGELEA kitu,....
....na KUFANYA kitu.:-(
Swali:
- AU?
Lakini KUONGELEA kitu,...
....kwa wengine,...
....huko ndio KUFANYA kitu!:-(
Swali:
- Kwani leo umekumbuka kujaribu kufanya unachoongelea?
Ndio,...
.... labda kama unaongelea tu,...
.... jaribu kufanya ili uone,..
...labda KUNA TOFAUTI aisee,...
...na ndio maana WAONGELEAJI wengi huishia KUONGEA tu na mchumba wamuongeleaye kwa kawaida hupewa mimba na WAFANYAO.:-(Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu Dwele atusaidie-What's Not To Love
Slum Village na Dwele warudie- Tainted
Au tu Slum Village wa- Raise it up
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mkuu tupo, mambo safi kabisa, hii ya leo imenikumbusha jamaa mmoja anayependa kuongea sana, na kila akimaliza anasema `fuata matendo yangu usifuate maneno yangu...' kwasababu anaongea mengi ambayo hayatekelezeki!
em3! Yaani huyo jamaa anasema kweli kabisa maana kuna wengi ambao wana maneno mengiiii lakini utekelezaji hakuna. Ahsante kwa leo na Ijumaa njema kwa wote.
Hili ni somo zuri kwetu sote - na hasa wanasiasa. Daima njia kati ya azimio na kitendo ni ndefu na kuvishonanisha pamoja vitu hivi mara nyingi ni kizungumkuti !
Hili ni somo zuri kwetu sote - na hasa WANASIASA. Daima njia kati ya azimio na kitendo ni ndefu na kuvishonanisha pamoja vitu hivi mara nyingi ni kizungumkuti. Hata mababa watakatifu kama Mtakatifu Kitururu wanajua !!!
Nimechoka kushika pembe wakati wengine wanamkamua ng'ombe maziwa. Ni mabadiliko ya kifikra yanatakiwa kujibadili kutoka kwenye maneno matupu hadi kwenye utendaji usionenwa.
Post a Comment