Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Jela kuna kitu kuwa INSTITUTIONALIZED!

>> Friday, June 03, 2011

Hebu kabla sijaendelea MORGAN FREEMAN anisaidie kuelezea namaanisha nini kwa kuwa -INSTITUTIONALIZED






Kabla sijaanza,..
...nanukuu:

``Ustaarabu ni utumwa, na ushenzi ni uhuru´´-Kamala J Lutatinisibwa






Naanza UPYA:

Ukikaa sana KIFUNGONI,...
... hamu ya kuwa HURU huanza KUTOLETA maana,..
... na kitokeacho wabongao UMOMBO hudai kuwa umekuwa tayari INSTITUTIONALIZED na kuwekwa ndani ndio ishakuwa KAWAIDA na kuachiwa huru ndio hugeuka kitu kisichotarajiwa.:-(


Ndio,...
.....kuna WATUMWA hufikia kutokuwa na HAMU ya kutolewa UTUMWANI kwa kuwa wajuacho ni UTUMWA,...
... na ukiwatoa UTUMWANI hawajui la kufanya na UHURU wao.:-(

Swali:
  • Kwani unafikiri kila MTU anajua cha kufanya na UHURU wake wakati unajionea mwenyewe jinsi watu wengi wajaribuvyo KUJICHUNGA wenyewe hata katika uhuru wao wa KUONGEA wanayoyafikiria kuhusu NYERERE au KIKWETE?

  • Kwani unafikiri kila MTU anajua jinsi ya kuwa huru wakati hata kuna MAMBO ya kujiuliza kuhusu MUNGU ambayo tayari yameshawazwa kuna watu ni vigumu kuyatamka HADHARANi kwa kuhofia KUKUFURU?

Ndio,...
.... ukizoea kukosa UHURU hata kwa kujikosesha UHURU mwenyewe,...
... kitokeacho ni kuzoea kutokuwa na UHURU!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
IJUMAA na WIKIENDI NJEMA!:-(


Hebu Andrew Ashimba aongelee-Maisha




Andrew Ashimba na Nakaaya warudie - Yaya



Au tu Samba Mapangala aingilie kati kwa-Vunja Mifupa

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 3:53 am  

Uhuru wa mtu ni mkono wake wa kushoto. Naam, nao ni muhimu sana katika maisha yake (kwa mifano ili aendeshe gari vizuri au ashike shoka kwa ukakamavu), lakini mtu anabaki hoi nao ikiwa mkono wake wa kulia umepata ajali au kilema.


Wajibu ndio mkono wa kulia; na tungekuwa wote duniani tunawajibika kama inavyostahili kwa kila moja wetu hata neno "uhuru" lisingekuwepo katika kamusi ya lugha yoyote ile. UHURU WOULD BE TAKEN FOR GRANTED! [Ask not what your country has done for you; rather ask: what have you done for your country?]


Kifupi, uhuru wamtu unaweza ukachukuliwa tu; na mtu akaishi kwa furaha hivyo hivyo ili mradi anangojea kwa hamu jua likichomoza atafanya shughuli gani; lakini mnyang'anye mtu uwezo wa kuwajibika ndipo umemmaliza kabisa,kwani umemfanya mtumwa ili yeye mwenyewe ajinyime uhuru bila wewe kusumbuka naye: UMEMPA DEPENDENCY SYDROME AU MAISHA YA OMBAOMBA KWAKO!


Tatizo sasa tabia yetu hatupendi kuwajibika. Tunapenda tu kula jasho na matunda yaliopandwa na wengine; na wakijaribu kudonoa nao kidogo matunda hayo tulieyataifisha kutoka kwao, TUNAWATIA MBARONI TU!:::::


:::INSTITUTIONALIZED!!!

Simon Kitururu 3:39 pm  

@Mkuu Goodman:Umenena Mkuu! Ila kwa watumiao mkono wa kushoto zaidi kama akina Obama wanaweza kugeuza hoja yakopia!

Kwa ujumla umeniwazisha upya hoja hii Mkuu!

Unknown 12:26 am  

Nilikuwa adimu kidogo ajili ya majukumu, sasa safari inaendelea kama kawa.

@Simon.
Kuhusu "INSTITUTIONALIZED!." Ndio maana kwa wale wanaobahatika kutoka hufanya uhalifu ili warejeshwe tena Jela aisee.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP