Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MSAADA: RENATHA BENEDICTO

>> Wednesday, June 08, 2011

Kutoka kwa Mubelwa T. Bandio:Ndugu.

Kwa mara nyingine nawakilisha ombi la kunisaidia kutangaza (wakati wowote upatapo nafasi) kuhusu Dada mdogo RENATHA BENEDICTO ambaye tumepoteana kwa takriban miaka 12 sasa.  

Renatha alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar kati ya mwaka 1998 - 2001 na baada ya hapo alienda Songea TTC kujiunga na masomo ya ualimu.    Pia alikuwa kati ya wahanga wa ajali mbaya ya Tawfiq iliyotokea tarehe kama ya leo mwaka 1999 ambapo alikuwa msaada mkubwa saana kuokoa maisha yangu. (Maelezo kamili yako http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/04/namtafuta-renatha-benedicto.html)

Niliwasiliana naye kwa miaka miwili iliyofuata mpaka alipoenda chuoni Songea nami nikaondoka nchini mwaka 2003 na kwa miaka mingi sasa nimekuwa nikijitahidi saana kumtafuta bila mafanikio.   Naomba kama anaweza kusoma ama kuna anayesoma na kumfahamu anisaidie kuwasiliana naye.

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 12:15 pm  

Twazidi kusisitiza kuwa kama umemuona, au ...una tetesi wasiliana na jamaa zake kwani ndugu, na udugu sio mchezo!

Yasinta Ngonyani 12:53 pm  

Yeyote anajua wapi Renatha yupo TAFADHALI awasiliana na kaka Mubelwa Bandio.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP