Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama utamu wa CHAI ambao kwa wengine sio chai -bali SUKARI!

>> Sunday, June 19, 2011

Kuna wazungumziao kupenda utamu wa CHAI,...
.... ingawa kwenye CHAI kiwanogeacho ni SUKARI tu aiseee!:-(

Swali:
  • Unabisha?

Kwa hiyo  labda kuna wadaio wanapenda MTU,....
.... ila wapendacho kwa MTU na kiwafikirishacho ni mtamu ni MATEGE yake tu,...
kitu kifanyacho ukimkata miguu,...
.... ndio watastukia hawapendi SAUTI yake , anachoongea au hata kwa ujumla,...
....HAWAMPENDI mtu huyo!:-(

Swali:
  • SI kuna wapendao hata mziki kisa wameona video yake na ukiondoa wakumbukavyo video muziki huo kwao sio MTAMU?

  • Na si inasemekana kuna wampigiaye kura mpaka Rais KIKWETE kisa wanampenda sura?


NDIO,....
.... kuna wadaio mpaka kupenda UGALI,...
...ila siri ya kupendakwao UGALI wauitao mtamu ni MBOGA TAMU,...
... na ukiondoa mboga TAMU kwao UGALI si MTAMU!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu Patricia Juste aingilie kati kwa-Sa Poko Anyen



VYBZ Kartel akatizie kwa-The lyricist



SIZZLA amtulize VYBZ Kartel kwa-How U get so brite!








Bado nipo....















0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP