Kwa kuwa kuna WAHOFIA hofu!
>> Wednesday, June 08, 2011
Ndio,...
... kiogopwacho kikubwa ni WOGA wenyewe tu yasemekana.:-(
Swali:
- Unafikiri kitishacho katika WOGA sio HOFU yenyewe tu zaidi ya KITU kisingiziwacho kutisha kizalishacho kiogopwacho ambacho ni HOFU?
- Kwani unafikiri huwa unaogopa nini HASA wakati UNAOGOPA?
Ndio,...
... labda KITU husingiziwa tu katika swala zima la KUTISHIKA,...
.... kwa kuwa kitesacho waoga ni HOFU YENYEWE na wala sio KITU hata kama hapa tutageuza hoja iwe ni woga wa jehanamu ambayo hakuna ajuaye kikweli machungu yake !:-(
Ni wazo tu hili MKULU!
Hebu tugewe tena Shikisha na Sipho Hotstix Mabuse
Au tu Sipho Mabuse arudie tu na - Jive Soweto
Simon Mahlathini &The Mahotella Queens wabadili mchezo kwa - Mbaqanga
Kabla Simon Mahlathini & Mahotella Queens hawajamalizia tu kwa-I'm In Love With a Rastaman
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Ahsante kwa soma hil: swali je kuna labda sababu ya mtu kuwa mwoga kwa hajui la kufanya anaogopa kutetea upande mmoja? :-(
@Yasinta
Barabara! " ...sababu ya mtu kuwa mwoga..hajui la kufanya..."
Kwa namna ingine: UOGA NI NDUGU YAKE UJINGA!
Ushauri kwa maoni yangu: Kwanza tukubaliane kwamba siku ya kufa utakufa tu, ikiwa kwa panga, risasi, sumu, vijidudu au virusi fulani.
Lakini, kabla ya hayo yote, kuwa jasiri, tetea haki, fanya kazi kama kawaida yako. Ukiwa mwoga basi wewe mtumwa na mwenye kuharakisha kifo chako kwa magonjwa tele ya nyongeza, kama magonjwa ya akili kama DEPRESSION, PHOBIAS, OBSESSION, HYPOCHONDRIA, PSYCHOSOMATIC CONDITIONS, ETC.!)
Uwoga unajengwa akilini kwa kuzania ubaya utaotokea, na hili linawaathiri wengi hata kupata magonjwa ya moyo!
Juzi juzi tu maeneo ya kwetu kuna watu wamekufa kwasababu ya kusikia mlio wa mabomu yakiangamizwa...sababu kubwa ni hofu!
Swali ni je hofu na uwoga zinakwenda pamoja?
Asanteni wote jamani!
Post a Comment