Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Stori za :``Nachofikiria kuhusu UNACHONIFIKIRIA!´´

>> Friday, June 10, 2011

Hapo zamani za kale kulikuwa na KUKU,...
.... anayefikiria MBWA wamuwindao wanafikiria yeye ni BATA.

Basi kila akifukuzwa na MBWA,...
..... alilalamika sana ni kwanini MBWA hawastukii yeye hafai KULIWA kwa kuwa yeye sio BATA,...
... paka siku moja alipofukuzwa akiwa na BATA na wote wawili kugeuzwa kitoweo cha MBWA.:-(

Swali:

  • Si unajua MTU anachofikiri kuhusu MTU mwingine anavyomfikiria kuna hatari ya kumfanya ajijibu jibu lisilo sahihi?

  • Si inawezekana afikiriacho kuku kuhusu afikiriacho MBWA kinaweza kuwa kina jibu la KIKUKU na sio jibu la KIMBWA?

Ndio,...
.... labda akufikiriavyo MTU mwingine,...
... na ufikiriavyo ni jinsi UNAVYOFIKIRIA kunaweza kuwa na utofauti wa hata rangi ya chupi!:-(

Ni wazo tu hili BINGWA!:-(





Hebu Kassav waingilie kati kwa-Zouk la ce sel




Au tu na Eduardo Paim akatizie denge kwa - Xinguila


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 3:20 am  

Muziki umekuwa mtamu sana, nimeufaidi kwelikweli.

Lakini sina uhakika kuku kwa kujiona yeye ni bora kuliko bata (yaani hawezi kawindwa na mbwa) tafsiri yake ni kama hivyo ulivyoweka, Mkuu.

"Dhana" au "mawazo" yake kuku hapa sio tafsiri ya hadithi; bali "maringo" yake kuku ndio tafsiri barabara!

Ukweli ni kwamba: 'mawazo' ya viumbe vyote yana chemchemi moja tu. Kwa hiyo mawazo ya watu yako sawa kwa mara nyingi kuliko yalivyokuwa tofauti. Hiyo itakuwa ndiyo ukweli hata ikiwa "nyeupe" yangu ni "nyekundu" kwako! Kivipi? Tukitizama rangi ya tambala moja tutakuwa wote wawili wenye makubaliano juu ya rangi yake tutakavyotamka hiyo rangi!

Nawaza tu, Mkuu; labda nimekosea!

o'Wambura Ng'wanambiti! 8:08 am  

Mt. Simon: si wajua waweza kuwa unawaza kupata juice ya ukwaju kumbe kitamaniwacho ni supu ya pweza katika ati kunogesha mahanjamu na kuondoa mning'inio wa ze kiburu ya jana ktk mkao wa lakuchumpa? :-(

Simon Kitururu 2:04 pm  

@Mkuu Goodman: Madhumuni ni ya taralila hii ni kufanya mtu awaze kitu fulani kwa hiyo hakuna kilichokosewa!

Ila kuhusu mawazo ya viumbe vyote yana chemchem moja tu,....
.... labda basi kata ya kuchotea wazo kwenye hiyo chemchem hutofautiana na ndio maana kwa mwingine ukimsalimia anafikiri unajipendekeza wakati wewe kwa kumsalimia hivyo unafikiri unamtakia mema jirani yako mwema!:-(

@Kadinali Chacha: Duh!:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP