Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda kuna MAMBO ni mpaka UYAISHI ndio utajua kwanini labda kwenye familia izalishayo WALOKOLE nako kuna aliyekua na kugeuka MCHAWI!:-(

>> Friday, June 24, 2011

Ndio,...
.... labda kuna MAMBO ,...
...hayaeleweki kama  cha wengine UJIHUSICHACHO nacho ukweli ni kuwa  kwa kuwa ni cha wengine,...
...wewe HAUHUSIKI!:-(

Ndio,...
..... labda MTU  kujifanya anaelewa sana ya WENGINE mambo,....
.... kama yale ya WADAIO wanajua MTU  kisa kuna kitu wanafananisha na wakijuavyo kikiwagusavyo maishani MWAO ,...
... wanaweza kusahau kuwa swala la   kujifanya wanajua kwa uhakika lile la ni kwanini MALAYA kawa MALAYA wakati  ni mtoto wa ASKOFU labda ni KUJIDANGANYA kwa kuwa labda  HATUA zimfanyazo hata MWIZI kugeuka MWIZI hata kama ni mtoto wa SHEKHE ni VIGUMU kuzijua kama katika maisha ya MHUSIKA  hao wanyosheao mtu kidole kikuhusika HAWAHUSIKI.:-(

Swali:
  •  SI ya wengine hata kama huyo mwingine ni mtoto wako kujifanya unajua kila kitu kwa kuwa ni mzazi -labda ni KUJIDANGANYA?
  • Kwani ukifikiria kisawasawa si utastukia kuwa hata nyumba moja  huzalisha  tabia na mielekeo tofauti ya wanafamilia hata kama wasomayo ni BIBLIA ileile moja?
  • Si inasemekana ni rahisi kuhukumu ya wengine  kwa kuwa si yetu na kivyetu ni vigumu kuelewa hao watu imetokeatokeaje  wametumbukia kwenye kibano ambacho kwetu ni cha kijinga?
  • Si inasemekana kama hujatembelea kiatu cha mtu ukapata kusikia joto alikabilio  labda usihukumu MTU au angalau  harufu mbaya za kiatu cha mtu ?

Ndio,...
.... labda  kuna MAMBO,...
.... ni mpaka UYAISHI wewe mwenyewe ndio utapata jibu la swali ``KWANINI?´´

Swali:
  • AU?

Ndio,...
... labda kuna sababu MAPACHA waliozaliwa tumbo moja na kulelewa sawasawa ,....
... mmoja akawa JAMBAZI asiyependa MALAYA na mwingine akawa MALAYA asiyependa MAJAMBAZI,...
... kutokana tu na KUHUSIKA na yasiyotuhusu na tusiyoyajua  ,....
... kitu kifanyacho kama tutajaribu kutoa jibu la uhakika la ``KWANINI?´´ kisa tunajifanya tunajua jibu ,...
.... labda tutakuwa tunajidanganya!:-(


NI wazo tu hili MHESHIMIWA!
Ijumaa na WIKIENDI njema!

Hebu Angie Stone aingilie kati kwa - No More Rain




Angie Stone Aendeleze- Wish I Didn't Miss You



Au tu sijui kwanini ila ngojea Angie arudie tena -No more Rain

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 7:20 am  

Kwanini natembelea kibaraza chako, Mkuu Simon; wakati mara nyingi nakupinga?


Haya, basi! Kwanza tujenge misingi miwili kabla ya kujadiliana na kuvutana kwa undani kabisa kuhusa mada ya leo.


1. ULOKOLE NI KITU KIZURI SANA; NA MLOKOLE ALIEBOBEA KATIKA IMANI YA UKRESTU AWEZA KABISA KUITINGISHA DUNIA KWA UWEMA SIO UBAYA. Ombi langu hapa ni kwamba tusiunyanyase ulokole, na hapo pia sijengi dhana kwamba Mkuu Simon ameunyanyasa. MIMI MWENYEWE MANYANYA NAJIHESABU KAMA MLOKOLE!! Naomba niishie hapo katika ULOKOLE lakini ninamengi kichwani na isingekuwa msiba ninayehudhuria saa kumi hapa Pretoria ningeandika ZAIDI ("GAMAHELE", kama angesema Dada Yasinta).



2. Naomba sasa nije katika SAYANSI au ujuzi. Moja ya sababu aliepatia Mwanasayansi Isaac Newton wa Uingereza heshima zake ni kule kugundua kwamba eti: "KWA KILA NGUVU ZA KUSONGEA MBELE, KWA WAKATI WATENDO HILO-HILO LA KUSONGA MBELE, LAZIMA ZIPO NGUVU SAWA-SAWA ZILIESABABISHA TENDO LA KWENDA NYUMA KWA KIWANGO KILE-KILE CHA KWENDEA MBELE". ("for every action there is a reaction of equal strength only in the opposite direction").


MISINGI NIMESHANJENGA, MKUU SIMON!


SASA NI KUJADILI NAWE!



Mimi nilisoma shule ya sekondari ya Tembeka (Zulu/Swazi/Xhosa/Ndebele: "Kuwa-Mwaminifu", lakini wao wanaandika 'Thembeka'), mji wa Nelpruit Afrika Kusini na sio mbali na Msumbiji, na siwadai ada yoyote! Kama mwalimu wako wewe Simon hakula ada yako bure shuleni... eti ulisema shule ya sekondari wapi tena, Mkuu Simon...?


"....Basi, kama mambo yalikwenda kama kawa shuleni kwako ya sekondari LAZIMA UKUBALIANE NAMI KWAMBA SI LAZIMA UYAISHI MAISHA YA MTU ILI KUELEWA MAZINGIRA YAKE!!!



Naam! Katika familia ya walokole watakuwepo wachawi! (Naam, katika familia ya maprofesa na wenye udoktareta wengi lazima vichaa wapo tu ila wanapenda kuficha!).


Hiyo ni sheria ya kisayansi. Hata Mkuu Simon wewe mwenyewe ukichunguza kwa Wapare ukoo wako, na Wajita (wajomba zako) UTAWAKUTA VICHAA KADHAA WALIOKARIBIANA NA FAMILIA YAKO, KAMA WEWE NI MSEMA-KWELI!


Mimi Manyanya hapa wengi tangu utotoni wangu walidai ninazo akili nyingi. Haya basi: UPANDE WA BABA, VICHAA NI WATATU (mmoja Afrika Kusinni mmoja Tanzania na watatu Malawi), NA WOTE WAMEKWISHA KUFA KUTOKANA NA UGONJWA WAO. Upande wamama: KICHAA MMOJA NAYE PIA ALIIFARIKI DUNIA MIAKA KAMA KUMI ILIEPITA!


Nini somo katika mandhari yako, Mkuu Simon?


NAOMBA NIPENDEKEZE JAWABU: "SOMO NI HILI HAPA: KILA TUNAPOPATA UWEZO WA KUIMULIKIA DUNIA, KUYIONYESHA UKWELI NA MAMBO HALISI YA MAISHA YA BINADAMU, KUYIELIMISHA, KUYIONYESHA UPENDO, KUPIGANIA HAKI, KUJITOA MHANGA NA MAMBO YOTE YALE KUMFANYA BINADAMU AENDELEE NA USTAARABU; hayo yote sio kwa ujanja wetu wala nguvu zetu, bali ni nguvu za Mwenyezi Mungu alietupatia kipaji hicho badala ya laana ya uwendawazimu au ugonjwa wa akili.. sisi tunawaakilisha familia zetu, ukoo wetu, kabila letu, Uafrika wetu pia na ubinadamu wetu! VILEVILE KILA TUKIWA WALOKOLE, TUSIWANYANYASE WATENDA-DHAMBI, BALI TULE NAO SAHANI MOJA ili tuwaonyeshe upendo na nguvu zake Mwenyezi Mungu.

Mimi nawe Simon hatunatofauti na vichaa. Na mlokole pia hana tofauti na mchawi...


... ISIPOKUA KWA HURUMA ZA MUUMBA TU!

Simon Kitururu 8:03 am  

@Mkuu Goodman: Kama ukisoma Blogu yangu kwa kuanzia Kichwa cha habari na mazagazaga yote,...
... unaweza kustukia inaneno JUU kabisa ``MAWAZONI na kuna FALSAFA ndani yake``.

kwa hiyo inamaana nachoandika sio HITIMISHO. Madhumuni ni uchokozi ili MTU afikirie tu kitu na kama akifikiria tofauti kwangu poa.

Pia utagundua kila nacho andika asilimia zaidi ya tisini kiko na lebo ``UjingaBUSARA´´ ni kiwa namaanisha karibu kila nachoandika huwa nacheza kati ya UJINGA na BUSARA na inategemea tu na msomaji ni nini anapata . Akipata ujinga kwangu sawa na akipata BUSARA kwangu sawa.

Na kama hata kwenye BLOGU yangu hii ikiwa umewahi kunisoma mahali kibao. Nakiri mie nishawahi kuokokoka na nimekulia katika mazingira ambayo lazima kabla ya kwenda kulala ni kusoma BIBLIA na kusali ndio watu watawanyike kwenda kulala ambako bado wakati mdogo mama alikuwa anakuja mpaka huko chumbani kuhakikisha najua kusali kabla ya kulala! Mama ambaye mpaka leo nikiaongea naye tu lazima atasema usimsahau Mungu wako.


Jumapili yangu ilikuwa inaanza na Sunday schoo, na nimeimba kwaya sana tu mpaka ikageuka hobi na ndio maana mpaka siku hizi naimba kwaya bado.

Ndio,...
... nilishakuwa Muislamu pia na mpaka leo Korani nasoma .


Kwa kifupi najaribu kusema sidharau WALOKOLE au watu wa dini yoyote KIIMANI.

Tatizo la MIMI na wewe kuwa kama tunapingana ni kwakuwa NACHOANDIKA wewe hukichukulia kama ndio hitimisho la nachosema.

Tunachopingana ni kwamba wewe unaamini kuna kweli ya aina fulani ambayo ndio kweli na mimi naamini labda KWELI hutegemea jinsi mtu alivyojifunza nini ni kweli!


Na kingine nafikiri ni IMANI ambayo kwa mfano wewe hunukuu BIBLIA kama kweli tupu na mimi mara kadhaa huwa napandisha hoja kuwa kuna uwezekano BIBLIA hata kitafsiri labda ilichakachuliwa .


Na wewe huandika sana ukizingatia kuwa ukweli ni kuwa kuna MUUMBA na mimi mara nyingi huweka room katika niandikacho kwa wasioamini kuna MUUMBA waonyeshe nao maringo yao.

Kwa kifupi vigezo na misingi nitokayo na stori huwa inatofautiana nawe kwa kuwa kimisingi imani na jinsi unisomavyo ,..
... huwa unatokea katika mtazamo tofauti na nahisi hilo ni moja lifanyalo nikiandika kitu huwa kinapingana na jinsi uaminivyo kitu!


Naamini BIBLIA imekujengea sana jinsi ya kutafsiri mambo kitu ambacho inasababisha mtu kama nikiandika kwa kukwepa mitego fulani ya KIBIBLIA ingawa nakutumia maneno kama WALOKOLE waswahilina na maneno kama hayo nahisi unahisi nashambulia kitu!.

Nakunukuu``KILA TUNAPOPATA UWEZO WA KUIMULIKIA DUNIA, KUYIONYESHA UKWELI NA MAMBO HALISI YA MAISHA YA BINADAMU, KUYIELIMISHA, KUYIONYESHA UPENDO, KUPIGANIA HAKI, KUJITOA MHANGA NA MAMBO YOTE YALE KUMFANYA BINADAMU AENDELEE NA USTAARABU´´ -mwisho wa nukuu.

Haki ya nani ndicho nachofanya kivyangu hapa bloguni kama utaniuliza mimi!:-(

Sema staili yangu labda haifanani na waungwana wafanyavyo!:-(

Na kuhusu ukichaa,...
... haki ya nani kuna watu kibao wanafikiri sina akili nzuri hata kwa kigezo cha staili yangu hapa bloguni!:-(

Samahani lakini kama huwa nakukwaza!
Na samahani kama huwa sieleweki1

Ila kama huwa nakufanya uwaze kitu basi kwangu madhumuni ya kuandika hapa huwa imetimia!:-(

Unknown 10:31 pm  

"Labda kuna MAMBO ni mpaka UYAISHI ndio utajua".

Goodman Manyanya Phiri 6:29 am  

@Mkuu Simon

Poa!!

Nilikuwa nakuchokoza tu! Mimi nawe Kulwa na Doto!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP