Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mwisho wa SIKU aishie na WEWE ni WEWE mwenyewe!

>> Thursday, June 02, 2011

Kwa hiyo,...

...... NI wewe uishiye na YALIYO YAKO,...
.... kitu kifanyacho wengine WASEMAYO kuwa yana asilimia kubwa sana ya KUBUNIA kuwa:
  • WEWE  ni nani
  • WEWE unawaza nini kikweli ukiwa kimya
  • WEWE ni kweli una roho nzuri au ni viini MACHO tu
... na kadhalika kadhaa za WATU  kufikiria wanayajua YAKO na yakuhusuyo WEWE.:-(

Swali:
  • Si unajua ndani ya siku hata kama unaishi na watu kwa kawaida ni mambo machache sana kuhusu hao uishinao au kufanyanao kazi  huwa kwa usahihi katika WAWAZACHO huwa kwa usahihi unastukia?

Ndio,...
.... labda yaliyo YAKO mawazoni,...
.... kwa asilimia kubwa ni WEWE mwenyewe uyajuayo ,..
.... kwa hiyo WENGINE wasemayo  kuhusu WEWE labda hayo sio WEWE.:-(

Swali:
  • AU?
Ndio,...
... kila mtu atakufa kivyake !:-(

NI wazo tu hili MHESHIMIWA na usikonde!:-(

Hebu AURELIO MARTINEZ arudishe tena dozi ya muziki wa Garifuna kwa - Yalifu



Au hebu SANTANA ahamishie pembeni kidogo kwa-Black MAGIC WOMAN



3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

isaackin 3:10 am  

ha ha haa mkuu kweli mnakua hamjuani lakini kuna watu wanakujua mpaka ulichokula jana usiku.lakini mwisho watakuacha baada ya kukufwatilia sana na baadae utaishi wewe mwenyewe.watu si watu
mkuu

Goodman Manyanya Phiri 5:16 am  

Hatuna uhakika mawazo yetu yanajulikana kwa watu wengine au la. Uhakika lakini tunao kwamba watu wawili wanaweza wakalala usingizi na kuota ndoto moja barabara kwa usiku huohuo. Sasa kama ndoto ni mawazo ya usingizini...mmmmmmh!

Simon Kitururu 6:44 am  

@Isaackin:Watu si WATU na hilo yasemekana ndio UBINADAMU aisee!:-(

@Mkuu Goodman: Swala la watu wawili kuota ndoto moja likiwekwa kwenye darubini linaweza kukatalika hata kisheria kwa hisia zangu kwa kuwa NAAMINI kuna watu hufananisha hata bukta nyekundu na nyeupe ZISIZOFANANA kisa zina mfuko nyuma kimshono uliofanana!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP