Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MOJA kwa MOJA kama ya MTU ya kutoka UTOTONI mpaka UKUBWANI!

>> Tuesday, June 28, 2011

Ni moja kwa moja,..
....kama chakula kisafirivyo kutoka Mdomoni kwenda kule CHOONI


Moja kwa moja,...
...kama asubuhi ibadilikavyo moja kwa moja kufikia yale ya USIKUNI.

Swali:

  • SI unajua ingawa kuna wafikiriao kuwa kuna ambayo hayaendi MOJA kwa moja kwa kuwa wanadhani DUNIANI kuna mpaka yale yapigayo ZIGIZAGA, ...
.... lakini labda bado ukweli ni kwamba labda yote uyajuayo kunajinsi tu ambavyo yako MOJA kwa MOJA hata kama ni kijinsi yagusavyo kitu FULANI?

Na bado ni MOJA kwa MOJA,...
... hata kama KIENDACHO MOJA KWA MOJA  ni matapishi kwa kuwa hata hayo  ukiyachorea mstari wa safari yake  waweza kustukia yalitoka moja kwa moja tumboni kabla hayajamtokea MTU puani!:-(

Swali tena:
  • Kwani unafikiri kama  kuna wadhaniao  kuna vizungukavyo na sio kwenda MOJA kwa MOJA basi  hilo ni kweli?

  • Hudhani kuwa labda kunauwezekano asiyeona kuwa kila kitu kina enda moja kwa moja kutoka sehemu moja mpaka nyingine kama mwanga wa tochi utokavyo kwenye tochi mpaka kummulika panya chini ya kitanda,...
... labda huyo  hajatanua tu jinsi ya kuliangalia SWALA?:-(

Ndio,...
... labda vidhaniavyo haviendi moja kwamoja,..
....hivyo havijapigiwa mstari  au tu kikuangaliwa kuna arukaye vigezo kuwa labda wakati anafikiri kuna vipikavyo kona ,...
... labda wakati huo bado anaviangalia MOJA kwa MOJA!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na si lazima ulielewe MKUU!:-(



Hebu moja kwa moja Keziah Jones Muafrika anizinguaye sanal tu aingilie kati JUMANNE yangu akianza kukuna  kwa :-African Spacecraft



Keziah Jones  anyuke - Where's Life



Keziah Jones  anong'one kuhusu - Beautiful Emilie




Au Keziah Jones amalizie tu kwa ndude- Rhythm Is Love

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP