MFUMO huweza kumgeuza NYERERE kuwa KIKWETE na KIKWETE kuwa NYERERE!:-(
>> Monday, June 27, 2011
Pamoja na UMUHIMU wa nguvu na akili za MTU BINAFSI,...
.... kwenye MFUMO UFANANAO hata ukiwa na watu wawili tofauti mpaka kiakili na kiitikadi kama Rais OBAMA na Rais BUSH,.......katika MFUMO uleule unaweza kukuta matokeo ya watu hao WAWILI wawazao tofauti YAKAFANANA kama tu hayatakuwa ni YALEYALE.:-(
Swali:
- Si unajua ni kwanini ili UINGEREZA iendelee kubakia UINGEREZA ileile -pamoja na kubadili MAWAZIRI WAKUU ili kuendeleza mkao uleule serikali kwa kawaida hufuata MFUMO uleule wenye MAMALKIA na WAFALME watokao katika familia ileile?
- Na si unajua kama MFUMO ni MZURI hata kiongozi mjinga anaweza asifanikiwe kufanya UJINGA?
Ndio,...
....katika mfumo bora unaoeleweka hata kwa NG'OMBE,...
.... yasemekana HUFANYA ni vigumu kwa ng'ombe hao kupotea ZIZI,...
... kama tu silabasi nzuri iwezavyo kuongoza MWALIMU asiyejua cha kufundisha aweze kuchagua kufundisha kwa wanafunzi yenye MANUFAA!:-(Hebu DE LA SOUL watulize kwa-Baby PHAT
Ndio ,...
... bado niponipo bado yani!:-(
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mfumo, mfumo...mkuu hapa umenipa wazo la kutafakari kuwa huko Arabuni na jamii yake kuna maandamano ya kuondoa `mfumo wa ufalme'...sasa huko uingereza vipi...maana naona kama ni mfumo uleule wa usultani...au kwa vile kuna `waziri mkuu anachaguliwa kidmokrasia? nimewaza tu mkuu!
Kitururu: Hapa umenigusa, nchini kwetu Tanzania mifumo kuanzia ya elimu na ya uongozi hainabudi kuangaliwa upya kama kuna nia ya dhati ya kuleta maendeleo.
@Mkuu M#: Ukichunguza kiitwacho ni DEMOKRASIA kinachofanya MAREKANI iitwe ni nchi ya DEMOKRASIA labda kikibadilishwa jina sio DEMOKRASIA hicho.:-(
@Mkuu Malkiory: Yani umenena Mkuu!
Post a Comment