Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Unachokiona hata baada ya kumvua MTU nguo KWA MACHO lakini sio KIFIKIRA!

>> Monday, June 20, 2011

Unachokiangalia KAMA sicho UNACHOKIFIKIRIA,...
.....LABDA huoni KITU!

Swali:
  • Unabisha?


Labda UNACHOFIKIRIA wakati unaona kitu ,...
....ndicho UKIONACHO vizuri aisee!:-(

Swali:
  • Si unajua kila siku barabarani  ni mengi uyaelekezeayo MACHO lakini huyaoni kwa kuwa UFIKIRIACHO ni kitu kingine?

Na  MTU ANAVYOFIKIRIA wakati anaangalia kitu,....
...... yaweza kuwa ndicho kipofuacho na kufanya  MTU asikione vizuri ANACHOANGALIA,....
.... kwa kuwa  kama unavyofikiria kuna misingi  mavi ya KUKU ni kinyesi,....
.... unaweza kutoona kinyesi  HICHO cha kuku KIRAHISI kama bonge la MBOLEA!:-(


Swali:
  • Si unafahamu MBOLEA ya mavi ya kuku ukiiangalia tu kama KINYESI ni vigumu kustukia mkao wake wa duka la mzungu liwazi KIMBOLEA?
  • Kwani WATU wanavyofikiria hujagundua ndicho kisababishacho wengi hawaoni hata MCHUMBA mzuri  KWAO aliye mbele za macho yao kisa wafikiriacho hupofua jinsi ya kumuona kuwa kimwana ingawa SANGARA wamo hana na anamatege kwa mbaali ila KITABIA ,akili lukuki na mambo mengine yote mengine  ni MAKSI mia kwa mia kikufaa kuwa MCHUMBA?

Ndio,...
.... unavyofikiria LABDA hupofua hata ni nini UNAKUMBUKA na kukiamini,...
... tukiachilia mbali ukweli LABDA hufanya unachokiangalia kilete maana tofauti KWAKO ile ya KUTOLETA MAANA  ,...
.... wakati kwa wengine hicho KINA MAANA:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

Hebu Winard Harper apige ngoma.
Dr Billy Taylor afundishe muziki ...
...halafu tu ...

Dr Billy Taylor 's Trio wakati Billy Taylor akiwa kwenye piano, Chip Jackson kwenye bass na  watupigie
-  Caravan.
Au tu Papa Wemba aingilie kati na kusawazisha kwa -Show Me The Way

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP