Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa MPENZI ambaye bado unayempenda sio MIMI!:-(

>> Sunday, June 26, 2011

Yawezekana MAPENZI ni safari,...
.... na apendwaye kwanza ni yule wakufanyia MAZOEZI !:-(

Kwa hiyo labda SIRI ni;...
....labda MJANJA si yule apendwaye mwanzo,...
... ingawa kwa asiyependwa MWANZONI  huweza kufikiria kuna wengine ndio waliomuondolea bikira  hata ya PENDO.:-(

Kwa hiyo labda PENDA tu wengine mwanawane PENDA!

Lakini  kuna uwezekano utakaye mpenda MWISHONI ndiye wako ambaye utampenda mpaka mwisho wa siku ,...
... na hapo ni kama kuna SIKU ambayo mtu huweza kuishiwa uwezo wa KUPENDA!:-(

Swali:
  • SI unajua  apendwaye ushahidi uko moyoni tu  hata kama aambiwaye ANAPENDWA kwa SAUTI   ya MDOMO wa MTU na mwenye mpaka PETE kama ushahidi kuwa ANAPENDWA labda  si yule apendwaye kwa dhati kutoka MOYONI?
  • Unafikiri ni muhimu KUPENDWA au KUPENDA?

Ndio,...
... MPENZI ambaye bado si wangu,...
.... labda penda tu kwanza hao wengine,...
... ilimradi wa MWISHO kumpenda ikiwezekana basi  itakuwa ni furaha yangu kama huyo akiwa MIMI!:-(

Swali:
  • Lakini mpenzi  MTARAJIWA hivi unaweza kuwapenda hao wengine harakaharaka ili uwe wangu kabla hujazeeka?

Wako,...
... ni mie mpenzi wako ambaye BADO hujastukia kuwa unanipenda kwa kuwa sasa hivi unahangaikia KUPENDA mtu mwingine.:-(

Ni mimi ,...
...yule LIMBUKENI wa PENZI na mwenye UMIMI kidogo kama udhaifu wangu ambao hujitokeza kidogo kwenye MAPENZI na wakati alengwaye kimapenzi ni WEWE ndio maana nasubiria kupendwa na wewe MPENZI mtarajiwa !.:-(

Haya ngojea mie niendelee kukupiga chabo kwa siri huku nikisubiria zamu yangu!:-(

BaiBai  basi kwa sasa  ewe TOTOZ zuri lenye macho ya GOLOLI, mashavu kama KITUMBUA , tako Mchina, Kujichubua fulu mia kwa mia, mwendo kama BATA,..
... DUH ngojea NISIMWAGE mchele kwenye KUKU lukuki ili nisije nikafanya mpaka wabaya wangu wajue nakuongelea WEWE KIPENZI  mwenye kijambo harufu ya BAMIA -ewe KIPENZI mtarajiwa- na kuniharibia gia!:-(

-----------------------------------____________________--------------------------------------------

NIMEACHA wazo MHESHIMIWA,...
... na ni ruksa kulitemea KOOZI wazo hili  lenye kibiongo cha kinyeo POHHH!:-(


Na tukiacha UTANI:
  • SI unajua hapa DUNIANI kuna sababu wako wapendao MABIKIRA kwa sababu mojawapo ya kutaka tu MABIKIRA  ni wao kujisikia WAMEPENDWA kwanza?

  • Kwani unafikiria kuna umuhimu  katika orodha ya waliowahi kupendwa uwe mtu wa KWANZA kama hata kama ni wa mwisho wakati unampenda mtu PENZI lilikuwa ni la kweli?


NI WAZO TU hili MHESHIMIWA!:-(

Hebu Tupac arudie -The King of Sorrow



Na Bilal arudie - Soul Sista

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP