Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kitu SAHIHI kilichofanyika KWA USAHIHI KABISA nacho NDICHO kwa WENGINE huzalisha pia MWANAHARAMU!

>> Wednesday, June 01, 2011

Ndio,...
.... MWANAHARAMU ni toto  lililozaliwa kutokana na kitendo SAHIHI,...
.....kilichofanyika kwa USAHIHI tu ndio maana kuna aliyepata MIMBA ,....
......na ni  JAMII tu kutokana na MUUNDO wa JAMII husababisha  kuna toto laitwa  la NJE/haramu ki MWANA.:-(

Swali:
  • SI umeshastukia KITENDO sahihi kikifanyika kiusahihi katika muda na mazingira JAMII ifikiriayo sio sahihi  kiwezavyo kufanya hata watu wenye akili kwenye jamii kufikiria hicho ni kigezo kuwa KITENDO kilichofanyika kwa USAHIHI matunda yake  sio SAHIHI?



Ndio,...
..... labda kuna MENGI yaaminikayo SIO SAHIHI ,...
..... hufanyika kwa usahihi kabisa,...
... na kiyageuzayo kuonekana sio SAHIHI ni jinsi tu BINADAMU walivyojifunza kufikiria JAMBO!

Swali:
  • SI unajua MWANAHARAMU kwa kawaida ni mtoto wa kawaida tu na wala hana LEBO kuwa ni MWANAHARAMU kama huchimbi  undani wa alivyozaliwazaliwa na kustukia kuwa alizaliwa nje ya NDOA ?
  • Na si unajua labda hata SIASA YA UJAMAA ni sahihi na  ni MUDA tu na MAZINGIRA  bila kusahau ilivyokuwa inafikiria JAMII ndio kilichogeuza ZIDUMU FIKIRA SAHIHI za SIASA YA UJAMAA kuonekana sio sahihi?
Ndio,...
....USAHIHI na USIO USAHIHI,...
.... mara kibao vigezo vyake ni vile walivyojitungia tu  WANAJAMII kutokana na MILA na DESTURI hata zisizo na kichwa wala miguu kama zitachunguzwa ,....
..... na ndio maana  USAHIHI mwingine katika JAMII ni  wa wasichana kukeketwa KIDUDE  na wavulana kukatwa jando  ,...
....na YOTE hayo kama tu jinsi ya KUSTUKIA  ni nani MWANAHARAMU,...
.... yahitaji  UCHUNGUZI  wa YASIYOWAHUSU.:-(


Ndio,...
.... hili ni WAZO TU na ruksa kutolielewa!:-(


Hebu moja kwa moja turudi HONDURAS  studio kwa Mhonduras AURELIO na na SENEGALI kwa Msenego Youssou N'dour wanafanyia kazi kibao tamutamu cha AURELIO MARTINEZ ....-Lubara Wanwa



Aurelio abakipekee katika mdinyo- Laru Beya



Au tu Aurelio arudie tu - Lubara Wanwa


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 9:03 pm  

MKuu kwanini mwanaharam ?je huyo alitokea kwanza au kuna tendo lilifanyika kwanza!

Rachel Siwa 10:54 pm  

Mimi nawaza kwanini watoto waitwe wanaharamu? Sababu wao hawausiki na uo uharamu, kama mzazi amepata mimba yake nje ya ndoa ni yeye si mtoto wake, sasa yeye si mwanaharamu ni mtoto kama watoto wengine.

Simon Kitururu 3:36 pm  

@Mkuu M3 na Da Rachel: Mmmh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP