Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama KUFA kwa ANDUNJE kwa kukabwa kwa BAHATI MBAYA na MWIBA WA DAGAA bado ni MIPANGO ya MUNGU!:-(

>> Sunday, June 19, 2011

Tahadhari : WAZO limepinda!:-(


Kama kufa kwa MTU,...
... ni mipango ya MUNGU,...

SWALI:
  • ...si akifa MTU hata kwa kupigwa roba na jambazi lililotokea CHOO cha migombani-SI LABDA  inatakiwa siye WAAMINIO MUNGU tuamini  hayo  ya KUFA kwake  MPENDWA   MTU tumpendaye labda bado ni MAPENZI TU ya MUNGU?:-(

Ndio,...
.... yasemekana MAPENZI ya MUNGU labda ni vigumu kwa BINADAMU kuyaelewa na ndio maana  ingawa kuna watesekao walalahoi ,...
....kwa KIBINADAMU kuna MAFISADI hata wale wasio amini MUNGU ndio ionekanao neema za BWANA  MUNGU zifanyao MABIBI zao WANAMEREMETA!:-(

Swali:
  • AU?

Ndio,...
...labda MAPENZI ya MUNGU -si labda kama unaimani ya KUTOSHA labda inabidi ikukubalishe kuwa mpaka LABDA ,...
.....kwa wamuaminio MUNGU hata wale wabakwao uchochoroni kuwa kwao uchochoroni wakati huo ambako KUBAKWA kwao kulifanikiwa labda uwepo wao huko ni MAPENZI ya MUNGU?

Swali zaidi lenye kibiongo:
  • Kwani unadhani ulipo sasa hivi ni kwa mapenzi yako IMEWEZEKANA uko hapo au ni kwa MAPENZI ya MUNGU?

Ndio,...
.....labda MAPENZI ya MUNGU hata kama UNAIMANI  na MUNGU,...
.... kibinadamu  unaweza kujikuta UMEKUFURU hata KIMAWAZO tu!:-(



NAENDELEA KUWAZA hili swala.....
Na ni  wazo tu hili MHESHIMIWA binadamu na hasa wewe uwezaye kukwazika nalo !:-(
Bwana asifiwe!



Hebu ghafla Curtis Mayfield akumbushie ~ Freddie is Dead



 Al Green arudie- People Get Ready




Al Green atekenye pia -How can you mend a broken heart



Curtis Mayfield aingilie tena kati kwa -Pusherman





Kabla Curtis Mayfield haja-Move on UP


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 8:35 pm  

Mkuu Simon, Tafuta maandishi matakatifu yenye imani ya Wayahudi (nafikiri wanaita kitabu chao Tora hivi kama sikosei) utapata hadithi ya Ayubu mule. Labda nikurahisishie kwa kukushauri utafute Biblia ya Wakrestu utakipata hata mule kitabu chake Ayubu. Ni hadithi kiboko sana ili kukujibu, Mtakakatifu Simon! Nenda soma mwenyewe lakini nataka unuse kidogo ili upate hamu kwani wewe kwa ku nusa-nusa vitu maarufu sana na hapo utanaswa tu! Na yote maandishi nimeyapata na kunukuu ninavyopenda kutoka Ukurasa 550 wa “the Holy Bible in Kiswahili, Union Version, Published as Biblia , Maandiko Matakatifu, Published jointly by Bible Societies of Tanzania and Kenya 1977, “Kitabu Cha Ayubu”.


1. Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.


2. Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti watatu.

3. Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng’ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki. ....


6,7,8,9,10. Ilikuwa , siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. Bwana akamwuliza Shetani....Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Wewe hukumzingira kwa ukingo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.


11 Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.


12 Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako...Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana...







MWISHO WA KU NUKUU BIBILIA (na kumradhi kwa makosa labda katika ku nukuu). SOMA BASI ZAIDI JINSI WATOTO WA HUYU AYUBU WALIVYOKUFA KIKATILI KWA RUHUSA YA MUNGU NA MAMBO MENGINE NIMEKWAMBIA SOMA MWENYEWE. KIFUPI, KAMA WEWE NI MWANAE SHETANI LAZIMA WATOTO WAKO WATAMEREMETA TU, LAKINI UKIWA SIMON WA KIBIBLIA USISHANGAE WATOTO WAKO WAKIVAA VIRAKA.... LAKINI SIO LAZIMA NA USISHTUKE, MKUU!

Mzee wa Changamoto 3:09 am  

Duh!!!

Simon Kitururu 8:59 pm  

@Mkuu Goodman: DUH!

Ila sasa kama mtu haamini BIBLIA kama kitabu kitakatifu inakuaje hapo?

@Rasta Mubelwa: Karibu tena Mkuu maana nahisi unanitenga sikuhizi Mkuu!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP