Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda AFRIKA tunakosea wa KUMHESHIMU!

>> Monday, June 13, 2011

Na labda,...

... ndio MAANA waheshimiwa WETU Afrika kwa kawaida HAWATULETEI MTUNO lawalawa tamutamu KUNOGA   ,...
....na labda hata HAWAFANYI tuheshimike kama WAAFRIKA hata kwenye vyoo vichafu vya KICHINA.:-(


Swali:
  • AU?
KAMA unaweza RUKA sehemu ifuatayo kwa kuwa mteremko wake inabidi utulie.:-(


Na STAILI ya kujifunza nini ni cha KUHESHIMIKA,...
.... nakumuadimaya MTU,...
.... labda NDIO kwa msaada wa ELIMU NDOGO hata ya KIKATA JANDO ifanyayo AFRIKA TUWE NA wababaikao kirahisi  WENGI kitu kifanyacho labda,...
 ...MWENYE HAYA kiuzito GUNIA   yenye afya ya mtuno wa KISIMI labda hayachukuliwi SIRIASI na waliojifunza kisimi kizuri ni kile kilicho KEKETWA au tu kunywea ,..
...kitu kifanyacho AHESHIMIWAYE ni YULE mwenye YALE hata kama kiujazo ni bakuli na kikisimi hakuna kilicho NYWEA ,...

... kitu kiaminishao BAADHI kuwa labda na LABDA sio WEWE mwenye HAYA,...
....na ndio maana mpaka HESHIMA za ombaomba haziendi kwa Mheshimiwa wa kiombaomba yule MHESHIMIWA MATONYA na zaenda MPAKA kwa MHESHIMIWA Rais KIKWETE kwa kuwa wakati MHESHIMIWA KIKWETE anaenda kuomba  kama tu alivyokuwa anafanya NYERERE kisiri,..
....huwa anatumia NDEGE kama USAFIRI kama alivyokuwa anafanya Rais MKAPA tu  Tanzania.:-(




Swali:
  • Au?

  • Si mpaka leo labda kiheshima za kuombaomba medali astahiliye ni MHESHIMIWA mzee MATONYA na sio Rais MKAPA?



  • Kwani umestukia labda AFRIKA na sio TANZANIA TU labda hatujastukia ni nani wa KUMHESHIMU na ndio maana kuna waheshimuo SHIMO na sio TUNDU hasa ukizingatia katika kuvuja labda TUNDU hubania kidogo ugawaji hata wa UKE kuliko SHIMO?
Rudi UKIPENDA  kwa kuwa kuanzia hapa ni rahisi kuelewa.


Labda AFRIKA tunakosea wa KUMUHESHIMU,...
.... kwa kuwa siku hizi wenye busara ndio INASEMEKANA  tufikiriao ni WASHAMBA!.


Ndio,..
..hili ni WAZO tu MHESHIMIWA!
Jumatatu NJEMA!:-(

Hebu twende Senegali ili AFRICANDO waingilie kati kwa -Yay Boy



Africando washikeshike mshawasha kwa - La Musica En Verite




Au tupitie tena KAMERUNI na MALI ili MANU DIBANGO  na Salif KEITA wabadilishe chupi kwa bukta -Emma




Nipo,...













Au tu ngoja  R. Kelly aweke  nukta kwa-Radio Messege

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) 5:15 am  

Baba Mtakatifu - Pengine inabidi tujiulize, kuna vigezo vyo vyote vinavyotumiwa katika kumheshimu mtu? Tunamheshimu mtu kwa ajili ya madaraka yake hata kama ni fisadi na "nondo mla watu". Je, tunamheshimu mtu kwa ajili ya umri wake kama ilivyo kawaida yetu Waafrika? Je, ni kweli tunatofautisha heshima na uoga? Ni Kweli Mobutu, Bokassa, Banda, Amin na "vichaa" wengine wa Afrika waliheshimiwa au waliogopwa tu? Akina Bongo Jr, Nguema na wanasiasa wengine wa Afrika ambao kimsingi ni chanzo (au kiendelezi) cha umasikini na matatizo yetu mengine ni kweli wanaheshimiwa au wanaogopwa tu kwa vile ni matajiri wa kutupwa na wanamiliki nguvu za dola? KAti, kama wanaheshimiwa, wanaheshimiwa kwa sababu gani? Je, Mwalimu Nyerere aliheshimiwa au aliogopwa? Mzee Rukhsa je? JK?

Umemgusia Ben. Kwangu mimi, pamoja na matatizo yake yote, Ben nadhani ni rais ambaye alikuwa ana uoni na angalau alijua Tanzania yetu ilikokuwa inatakiwa kwenda. Alikabidhiwa nchi iliyovurugika na Mzee Rukhsa na aliweza japo kuonyesha njia; na ni wazi kwamba J.K alirithi nchi iliyokuwa na neema pengine kuliko rais mwingine ye yote katika historia fupi ya nchi yetu.

Kama wanasiasa hawa wanaogopwa basi hili ni jambo jema kwani utafika wakati ambapo waogopaji hofu yao itakwisha. Tumeshaliona hili kule Misri, Tunisia na kwingineko. Moyo wa uhuru na tamaa ya kujikomboa ya binadamu kamwe haizimwi; na kama inazimwa ni kwa muda tu. Na hawa "waheshimiwa" wanatambua hivyo...

Mtakatifu - Nimerudi!!!

Goodman Manyanya Phiri 10:40 am  

Wanaheshimika WOTE kabisa, viongozi wetu Barani kote. Tatizo ni moja: wao sio waaminifu.

Kabla ya kuchaguliwa, wanatuahidi ardhi nzima na mbingu yake!

Baada ya kuchaguliwa wanakwenda kumsikiliza Malkia wa huko Wingereza watekeleze lipi na waache lipi katika ka ahadi zao kwetu.

Wajapan, haohao Wachina, na nchi nyingi za mashariki walikataa kuabudu nchi za Ulaya; na wakaendeleza mifumo yao ya kuwaamini wananchi wao. Ndio, bei ya uhuru wao ilikuwa kubwa sana... mara hapa wanateseka kiuchimi...mara wanashambuliwa hata kwa mabomu ya NUCLEAR.


...Lakini waone walivyokuwa na nguvu leo za kiuchumi na kujitegemea!

Uchumi au pesa (TENA YAKO SIO YA KUAZIMWA na IMF) ndiyo HESHIMA halisi ya kiongozi, Mkuu Kitururu!!!

emu-three 1:32 pm  

Heshima ya mtu itategemea sio umri tu, ukubwa, au uheshimiwa, lakini nini anachokifanya katika jamii. Nimeshangaa mzee wa miaka 50 anamwita kijana, `mzee' kwasababu ni bosi wake ofisini, je hii ni heshima.
'Mzee naomba kamkopo kidogo..nina shida, mzee tafadhali..' huyu anayezumgumza hivi ni mzee wa miaka 50 anambembeleza bosi wake wa miaka 27...! Ni kwa nyongeza tu mkuu!

Simon Kitururu 3:16 am  

@Papaa Masangu: Karibu sana tena maana ulipotea Mkuu!:-(

@Mkuu Goodman: DUH!

@M3:Nyongeza yako imetuna aisee!

Goodman Manyanya Phiri 2:04 am  

@M3

Ninavyoelewa mimi neno "Mzee" lina maana nyingi kuliko tu mtu mwenye umri mkubwa au mwenye familia na watoto wengi.


Mwalimu wangu wa Kiswahili For Beginners 1992 huko Ilala Dar alisema ni sahii kabisa kumuita Bosi wako "Mzee".


Alisema "Mzee" ni sawasawa na neno la Kiingereza: "Sir". Na Mzungu hakosei anapomwuliza mwanaye : "Did you go to school today, Sir?"


Niambie basi kama mwalimu wangu wa Kiswahili alinipoteza niende nikadai ada! Sasa hivi nimechacha ile mbaya tena!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP