Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NGUMI kurindima ILALA Oktoba16

>> Wednesday, October 05, 2011


ZAIDI ya mabondia 42 wanatarajia kushiriki katika mashindano ya mchezo wa ngumi yanayotarajiwa kufanyika Oktoba16 mwaka huu Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha wa Klabu ya Ashanti ya Ilala, Rajabu Mhamila, 'Super D' alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha Klabu 12 kutoka katika maeneo mbalimbali.

Alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kufanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala.

Super D alisema kuwa mashindano hayo yana lengo la kuendeleza kuhamasisha mchezo wa ngumi nchini ikiwa ni pamoja na muendelezo wa mchezo huo unanaofanywa na Kinyogoli Foundation.

“Tumeandaa mashindano ya ngumi ambayo yatashirikisha vijana mbalimbali na lengo letu ni kuhamasisha mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuuendeleza ili uweze kutuletea faida hapo baadaye”
-alisema.

Kocha huyo alisema kuwa vijana watakaoshiriki watakuwa katika uzito mbalimbali kuanzia Unyoya mpaka uzito wa juu.

Alisema kuwa pia wanatarajia kushirikisha mabondia wa kike kutoka katika klabu hizo hizo.

Aliongeza kwa kusema kuwa wanahitaji wadau mbalimbali wajitokeze kuwasaidia mahitaji mbalimbali ya vijana ikiwemo maji kwa ajili ya mchezo huo kwa siku hiyo wenye nia ya kutaka kusaidia au kushiriki kwa kuchangia chochote wanaweza kuja katika ukumbi wa mazoezi uliopo Amana Ilala au kufika Ashanti Boxing club.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na Kocha Mkongwe;
Habibu Kinyogoli kwa simu 0655928298  .

Au unaweza kuwasiliana na ;
Super D Boxing Coach kwa simu O713,0787-406938 
Email: superdboxingcoach@gmail.com

Wadau mbalimbali mnakaribishwa.

--

'Super D'

Photojournalist at Majira, Business Times
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania



--
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania


Nimetumiwa na:
Superdboxing coach

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP