Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Sherehe za uzinduzi wa kituo cha uwekezaji(TCI) jijini Mbeya

>> Thursday, October 27, 2011

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu akikata utepe kuzindua ofisi ya kituo cha uwekezaji (TCI) nyanda za juu kusini mjini Mbeya.
 Jengo la TCI Mkoani Mbeya

Akizindua ofisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Mbeya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu alisema ofisi hiyo ni muhimu katika kusaidia wajasiriamali na wawekezaji wa mikoa ya Ruvuma, Iringa Rukwa na Mbeya kuitumia kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali ya uwekezaji.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIC, Balozi Elly Mtango.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Raymond Mbilinyi alisema Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimkaribisha waziri Mary Nagu alisema mkoa wake unazo fursa nyingi zikiwemo za kilimo katika Bonde la Mbarali na maeneo mengine, ufugaji, uvuvi katika ziwa Nyasa, utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo na uchimbaji wa makaa ya mawe katika eneo la Kiwira.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa kituo cha uwekezaji jijini Mbeya kutoka Kushoto Mbele ni Mrs Kadyanji na anaefuatia ni Mrs. Yunge na wajasilia mali wengine.
Picha zote na Mbeya yetu Blog


Na nimetumiwa HABARI na PICHA na:
WADAU wa MBEYA YETU Blog.

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP