Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ASANTE SIRI kwa kufanya mengine YA MHESHIMIWA kuwa siri ingawa kuna wenye hamu ya kumchungulia!:-(

>> Friday, January 07, 2011

[Tahadhari: Wazo limepinda!:-(]


Kwa kuwa BINADAMU wote ni dhaifu,....
...... yeyote ambaye ni BINADAMU  ANAYEHESHIMIWA labda kuna ambayo tu yasingekuwa SIRI,....
..... mwenye kuheshimiwa  ASINGEHESHIMIWA HIVYO,...

... au angalau aheshimiwaye kwa tako labda HESHIMA yake ingepungua SIRI YAKE ingejulikana kuwa pamoja na uzuri WOTE wa tako bado MHESHIMIWA ni tabia yake kupendelea zaidi kuvaa chupi chafu makusudi!:-(


Swali :
  • SI unajua labda kuna mpaka RAIS WA NCHI  au tu MKUU wa kitengo cha afya za pua AHESHIMIWAYE na WACHUKIAO MAKAMASI  ambaye kwa siri labda hupenda kulamba kamasi?

Kuna SIRI,....
..... labda ndizo zitunzazo mpaka NDOA za watu WENGINE  ustukiao HAWANAFURAHA na fulu kudokoa nje  ,....
.... lakini JITU  limke au tu hata  LIMME  halimuachi .:-(


SIRI,....
...inaweza kuwa ndio inasaidia mpaka KISA  CHA ni kwanini dini haziachwi na hata wenye wasiwasi  kuwa labda MUHUBIRI katika aongeleayo ya MUNGU anapiga bao nje,....
..... kwa kuwa bado ya MUNGU NI SIRI YA MUNGU na kwa kujitutumua na akili za KIBINADAMU  bado utakuta kuna maeneo PAMOJA NA UJUAJI bado BINADAMU mwenye akili atakuwa tu angalau siku nyingine na kutokuwa na uhakika na-  KIHISIA kuwa  kuna uwezekano anachemka hakumuachi.:-(


Swali:
  • AU?
  • SI unajua lakini labda MTU hana siri kama akiitacho siri  HUYOHUYO muhusika ni kwa kuwa tu kaacha tu kufikiria kuwa YEYE hicho kidude anakijua?


Na siri,....
....ni mamalao,.....
......na ndio maana linamchezo wa kuzaa kitu AMBACHO LABDA WALA SIO SIRI  hata kama kuna ambaye kwa kukosa umakini hastukii.:-(





Asante SIRI,.....
.... kwa kuwa kuna WAHESHIMIWA  hata sijui kwanini lakini ningependa kutojua SANA MAMBO YAO hasa yasiyogusa MAENEO yaliyonifanya NIWAHESHIMU ili nisije kuwakosea HESHIMA  BURE kwa kuwa KUWAHESHIMU ni moja ya kinifanyacho nijipime kuwa BADO NAHESHIMA na pia SIJUI KWANINI  TU ila pia hata kama KUNA MENGINE  KUJUA kusingenifanya nishushe heshima bado asante kwa kunifanya nisijue  kwa UHAKIKA kuwa  nao wanapiga punyeto, wanadokoa mboga jikoni kwa kuhofia kukosa minofu mikubwa mezani KWA KUWA BABA WATOTO huing'ang'ania ikifika mkekani au tu wanapenda mbuzi  na kuku kimapenzi KWA VITENDO  yafananayo na ya MKE na MUME na twawaheshimu kwa kuwa kuna KITU tu  hatustukii!:-(


Tukumbuke tu lakini kuwa TATIZO LA SIRI,...
... kirahisi hugeuza  hata WAHESHIMIWA tufikiriao wako huru  kuwa watumwa wa kuficha yote yahusiananayo na wakitafsricho kuwa ni siri hata kama siye wala HATUSTUKII.:-(

Na labda ni ndio kuwa ni shauri ya  SIRI,...
.... wengi WANAHESHIMIWA kwa kuwa tu mengi WENYE HESHIMA hawastukii!:-(





NI WAZO TU HILI Mheshimiwa!
Ijumaa na WIKIENDI Njema!

Hebu tumpate Nat KING COLE arudishe ustaarabu hapa kijiweni kwa kitu -LOVE



Hebu binti yake Nat King Cole kwa jina Natalie Cole aingilie kati kwa -This will be an everlastin' love



Au tu Glenn Miller amalizie kwa-In the Mood

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) 4:09 pm  

Mtakatifu. Umenikumbusha jamaa mmoja Mhafidhina wa dini fulani hivi nilimsikia akiunguruma huku akidai kwamba Yesu Asingeweza na hawezi kuwa Mwana wa Mungu kwa sababu ya mambo aliyokuwa akiyafanya sirini.

Sitaki kuchokoza watu hapa nisije nikatangaziwa "fatwa". Siri sirini ati!

Yasinta Ngonyani 4:16 pm  

Siri:-(

Faith S Hilary 4:22 pm  

Hahahahahaaaaaa!!! Halafu kweli eh? Wakati nasoma hii nikawa natafakari watu wengi ambao ni "waheshimiwa" mpaka Queen of England (or UK) akanijia akilini...na wengine wengi tu ila ndio siri yangu mwenyewe...haha! Simon you amuse me!

Serina 9:14 pm  

Mziki murwa kama kawaida...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP