Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NGOJEA tubinyebinye mahusiano yaitwayo - ``URAFIKI!´´

>> Friday, January 28, 2011

Tukiangalia kiitwacho ``URAFIKI´´,...


....LABDA kuna sababu katika URAFIKI  kuna watokeao kuwa/ kuitwa ma- BEST FRIENDS aka MARAFIKI BOMBA,...
..... na  kunaoitwa ``MARAFIKI ´´ kijina tu!:-(

Na URAFIKI  ni neno pana ,...
.....kiasi kwamba limejumuisha mambo mengi mpaka WATU HUSAHAU  kuwa ,...
.... kuna aina nyingi za URAFIKI mpaka  yawezekana ,...

...UADUI labda ni aina moja wapo tu ya URAFIKI,....


.... kama tungeachilia mbali TAFSIRI kama HIZI  kikipengele kwa ung'eng'e  :

``Friendship is a personal relationship shared between each friend for the welfare of other, in other words, it is the relationship of trust, faith and concern for each other feelings. It is a relationship of mutual caring and intimacy among one another. A friend is one who knows you as a person and regards you for what you are and not what he or she is looking in a good friend. Best friend is one who accepts the good as well bad qualities of his friend and also takes an initiative in correcting and mending them. Friendship is a distinctive kind of concern for your friend, it is a relationship of immense faith and love for each other. ´´kutoka hapa

Yenye tafsiri kwa lugha fasaha :``UFRENDI ni uhusiano wa wadau ambao hata kama mambo sio BIYE bado  wanapeana shavu  kisela kwa lugha nyingine  -ni uhusiano wa wadau ambao WAKO TAITI YANI ile KINOMA , kuaminiana freshi, kusikilizia  maswala ya mdau AMBAYE  mambo sio mswano kinaeleweka YANI . Ni uhusiano  ambao mtu hananoma yani na mipangilio ya mtu mwingine  katika kukamatia hata ambayo si kila MCHIZI  anaona ni freshi  .

Mtu ambaye  anamchukulia MDAU  freshi tu vilealivyo na sio kumzingua kwa kuwa anahisi mdau kuna mambo ajichanganyayo nayo sio BAB kubwa  kiufrendi - yani ukienda mbele sendema MDAU yuko TAITI tu na wewe na UKIRUDI nyuma SENDEMA tu  kama kawa ingawa kiadoadao anaweza pia kuwa anatonya kiadoado  mtonyo kwa FRENDI kuwa  kuna maswala ni NOMA  yani kujipinda nayo KWA SANA kwa kuwa yaweza sababisha asali kuingia CHUMVI chumvini yani.´´


.....kwa kuwa labda neno RAFIKI ,...
... laweza kuwa ni miongoni ya maneno ya KISWAHILI ambayo hutumiwa hovyo kuliko yote hata katika kuashiria yasipofaa kutumika,...
....kwa kuwa kuna  yafikiriwayo afanyaye ni RAFIKI wakati ni adhaniwaye ni  ADUI ambaye ndiye bingwa wakumfanyia MTU .:-(

Swali:
  • Kwani huhisi kuwa LUGHA ya kiswahili inamapungufu sana ya maneno na pia WATUMIAJI wakiswahi  huzinguka na maneno  sana tu YA KISWAHILI  ndio maana unaweza kukuta pahitajipo  kutumika neno MWIZI kuna waridhikao  kutumia tu neno FISADI?

Samahani!
Ngojea basi tuanze tena UPYA kuangalia hiki kitu kiitwacho  ``URAFIKI  !´´




Mbinyo wa kwanza kimtazamo:


 Kama una marafiki wawili ,....
.....labda  WEYE  una urafiki wa aina MBILI,....
..... na kama una marafiki sita ,...
.... weye unaurafiki wa aina SITA!:-(


 Kama una MARAFIKI mademu hao ni marafiki zako tofauti kabisa na MARAFIKI zako wa KIUME.


Na  labda ni tatizo kama MTU atajaribu kutaka neno URAFIKI,....
.....liwe na maana moja kwa kuwa hakuna MTU mwenye marafiki wawili SAWA.

Na rafiki wako wa KIKE  hawezi kuwa sawa na rafiki wako wa KIUME,....
.... hasa tukizingatia kuwa  inajulikana kuwa kwa kawaida  HATA kwa sababu za KIBAOLOJIA,...
..... wanaume na wanawake ni tofauti ,...
... na JINSI wanaume waingiavyo kitu kichwakichwa KATIKA kufikiria kitu  ni tofauti na jinsi ya WANAWAKE katika ndude hiyohiyo wakaavyo mkao wa kukidadavua.

Swali:
  • Unabisha?




Mbinyo wa pili kimtazamo:




Na kama wewe ni MZAZI,...
.... labda jaribu kuwa MZAZI na sio RAFIKI kwa watoto wako,....
.... kwa kuwa mwisho wa siku ni MZAZI ahitajikaye kwa watoto wake na sio RAFIKI.


Na kama wewe ni MZAZI ,...
... kamwe MTOTO wako sio rafiki yako hata kama ni neno URAFIKI ndio  mnaita  mahusiano yenu  na ndio mmechagua  KUAMINI.

Na ingawa  kuna wadaio kuwa ni bomba WAZAZI  kutafsiri ni URAFIKI MAHUSIANO YAO NA WANAO aka watoto wao,....
......tatizo hujitokeza kwa kuwa wengi hawatofautishi URAFIKI ni nini kitu kiwezacho fanya URAFIKI wadaio watoto na wautambuao watoto ni ule waufananishao na urafiki wao na watoto wenzao kitu kiwezacho kufanya ,...

.... MZAZI aitwaye kuwa ni rafiki na watoto wake kuwa ni yule ambaye,....
.... labda  kuna kitu kama MZAZI anakiruka ili watoto wamfananishe na marafiki zao kitu ambacho madhara yake yapo tu.

Swali:
  • Unabisha?
  • Unauhakika na neno URAFIKI linamaanisha nini?






Ngojea tupate hoja kwa kutazama mahusiano ya MBWA na moja ya wamiliki MBWA ulaya katika mbenjuo wa hoja:

Katika tembea tembea zangu nchi za MAGHARIBI mara KEDEKEDE nimekutana na familia ambazo zinawafuga MBWA na kuwa na mahusiano na hao MBWA kama vile hao MBWA ni BINADAMU.

Na utakuta wengi wawachukuliao MBWA kama vile BINADAMU  mwisho wa siku hujikuta wanatafuta mpaka MAKOCHA wa MBWA aka DOG BEHAVIOR SPECIALISTS kisa hao MBWA wanawashinda kitabia. Utakuta nyumbani kwa MTU lakini ni MBWA katawala na  kama MBWA hataki mlale kitanda kimoja basi ndio itakuwa hivyo,...
....na kama MBWA hataki wageni basi wageni MWIKO hapo nyumbani na vikorokocho vingine kibao,...
...kisa tu MBWA mmnyama ambaye kazoea kuwa na KIONGOZI  hata katika kundi la MBWA kachukua nafasi yake ya uongozi katika kundi  na kuwa PACK LEADER aka kiongozi wa kundi la MBWA.:-(

Lakini kuna njia ya kuwa na urafiki na MBWA bila kugeuza mahusiano ya MTU na MBWA yawe sawasawa na ya MTU na MBWA.


Tukirudisha boli kwa watu ,...



Na labda MZAZI awe MZAZI kwa mtoto na urafiki  wa MZAZI na MTOTO ubakie kuwa ule wa MZAZI kubakia MZAZI MLEZI na mtoto  abakie kutafuta uzazi wa mzazi na sio kufikiria ni POA kwa kuwa MZAZI  mambo zake yanafananafanana na ya marafiki zake.

Swali:
  • Na si nilishaongelea uwezekano wa  HAKUNA mtu MWENYE MARAFIKI ambaye ana urafiki na watu wawili tofauti ambao uko sawa?


HITIMISHO kimbinyo:

Kama ilivyokuwa BINADAMU wote ni sawa lakini si sawasawa,...
.... tukumbuke kuwa kila RAFIKI  ni tofauti ,...
.... na labda neno lenyewe ``URAFIKI´´ linamapungufu kwa kuwa labda mpaka UADUI ni aina tu ya URAFIKI hasa kama UADUI  wako na mtu ndio unakusaidia  katika YAKO ya kupiga hatua mbele hata kama ni kwa KUJIHAMI .:-(




LUGHAA!
NI WAZO TU HILI LA CHAPUCHAPU  libinyalo hapa na pale KIMBINYO chapchap tu MHESHIMIWA  na usikonde kama kunaeneo halijabinya sana HASA KUTOKANA na LUGHA nitumiayo HAPA  kuhangaika sana na nachofikiria!:-(
Ijumaa na WIKIENDI NJEMA MHESHIMIWA yani!


Hebu KRS 1 apige krosi gemu kwa -A FRIEND






KRS 1 aingizie kitu katika- You Must Learn




Au tu Jeru DA Damaja atulize tu boli  kwa - Ya Playing Yourself

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 10:00 am  

Mkuu kama ulivyosema kuwa kiswahilii kama lugha ina mapungufu yakukamilisha maana ya kitu au jambo. Maneno yake hayatoshelezi, labda kwasababu lugha yenyewe imejengwa na maneno ya wengine...lakini najiuliza nani wa kuitutumua hii lugha ili ijitosheleze kimaneno...maana neno kama rafiki ulivyolidadavua linaweza likamfanya hata adui kuwa rafiki...sasa je TUFANYEJE?
Labda tusubiri wafadhili...nawaza tu mkuu, kwani hata kufagia sasa hivi, hata uasafi wetu, haufanyiki mpaka wafadhili...kazi hiyooo mkuu! Mhhh nawaza tu!

chib 6:01 pm  

Huo ni mtizamo wa Mt KATIKA MANTIKI YA URAFIKI. Lakini ninavyojua kinyume cha rafiki ni adui.

Simon Kitururu 7:42 pm  

@M3: Watakaotutumua lugha nadhani ni waandishi kama wewe! AU?

@Mkuu CHIB:

Lakini ........

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP